Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » YAJUE MAMBO YANAYOWAKERA SANA WANAUME KWENYE MAPENZI NA NDOA
Mahusiano

YAJUE MAMBO YANAYOWAKERA SANA WANAUME KWENYE MAPENZI NA NDOA

BurhoneyBy BurhoneyMarch 29, 2025No Comments3 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
YAJUE MAMBO YANAYOWAKERA SANA WANAUME KWENYE MAPENZI NA NDOA
YAJUE MAMBO YANAYOWAKERA SANA WANAUME KWENYE MAPENZI NA NDOA
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Katika uhusiano wa kimapenzi na ndoa, kila mmoja ana matarajio na mawazo yake kuhusu jinsi mambo yanavyopaswa kuwa. Ingawa wanawake mara nyingi hufikiria mambo fulani kuhusu mahusiano yao, kuna mambo mengi ambayo wanaume pia wanayatamani na kuyahisi kwa namna fulani. Wanaume, kama wanawake, wanahitaji kuheshimiwa, kutunzwa, na kujaliwa upendo katika uhusiano wao. Hata hivyo, kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kuwakwaza au kuwafanya wanaume kuhisi kutojali au kukerwa kwenye mapenzi na ndoa.

Mwanamke kukosa imani kwa mwanaume:

Kutokua na imani na mpenzi wako kunatafsirika kama vile kutojiamini wewe mwenyewe. Yupo na wewe sio kwa sababu hakuwaona hao wanawake wengine. Badala ya wewe kumhadaa kwa maneno ya kutomuonyesha unampenda, au kumchunguza chunguza sana, wewe wekeza katika kumpenda kweli kweli, muonyeshe kuwa hajakosea kukuchagua, fahamu anahitaji nini na umpatie vyote. Sio tuu tendo la ndoa, mwanaume anahitaji mambo mengi toka kwako. Je bado anajisikia kuwa wewe ni rafiki yule aliyekua nae wakati mnaanza mahusiano ? Je unaendelea kujipamba na kupendeza kama wakati ule mnaanza mahusiano ?

Mwanamke kutokuwa mshauri na wa karibu :

Biblia inasema mwanamke aliumbwa kama msaidizi wa mwanaume. Wanaume wengi hawapendi mwanamke ambaye sio mshauri. Jitahidi mjenge uwazi na utamaduni wa kuzungumza mambo yenu yawe ya kikazi , kibiashara , mahusiano na watu wengine au familia. Mfahamu vema mpenzi wako na ujitahidi kumpa ushauri kwa hekima na upendo mkubwa.  Kuna wanawake wengine hawajui hata wanaume zao wanafanya kazi gani, hawajui hata magumu wanayopitia na hata marafiki za wapenzi wao.

Mwanamke kupoteza nafasi yake ya umama kwa mwanaume:

Wanaume ni kama watoto wadogo, wanahitaji kujisikia yupo “mama” anayewalinda na kuwafanyia mambo. Ndio maana kwa mfano mwanamme kabla hajaoa na alikua akiishi mwenyewe anaweza kufanya vitu vingi yeye mwenyewe, ila akishaoa tuu hata soksi zake hajui wapi huwa zinakaa.

Hivyo basi usiache kumchukulia mwanaume wako kwa upole kama mmoja wa watoto wako hata kama ni profesa, au ni baunsa. Tambua utahitaji kumsaidia kufanya vitu vingi vidogo vidogo haswa vya nyumbani na vinavyomuhusu yeye mwenyewe. Mfano hakikisha unamkumbusha kunywa dawa kama mgonjwa, kupiga mswaki, kubeba wallet yake, na hata mikutano na dili alizonazo. Mfanye ajisikie ana msaada na mtu anayeweza kumsaidia kweli kweli.

Soma Hii :Vitu vya kuzingatia kwenye mahusiano

Mtunzie “uanaume” wake:

Wanaume kwa asili yao ni watu wa kutaka kutoa suluhu, ni watu wa kutaka kuwa wa msaada kwa wanawake wao. Wanahitaji kujisikia kuwa wanayo nafasi hiyo na unaheshimu na kuamini kuwa wao wanaweza.  Msifie mwanaume wako kila unapoweza, mshukuru anapokufanyia jambo , muonyeshe kweli unathamini na unajisikia furaha na kujivunia kuwa na mwanaume kama yeye. Usifie wanaume wengi, usimlinganishe mwanaume wako na wanaume wengine, na mwiko kumkashifu, kumsema ua kuonyesha dharau kwake na haswa haswa dharau kwake mbele ya watu wengine. Kuwa makini na utani wako kwake, usipitilize haswa kwa mambo ya msingi. Mfano mwanaume wako mpenzi anakufanyia kitu halafu wewe unaingiza utani kuwa mbona fulani kafanya zaidi kwa mpenzi wake.

Mwanammke kutoonyesha hisia wakati wa tendo la ndoa:

Baadhi ya wanawake hujikuta wanafanya tendo la ndoa na mpenzi kwa sababu tuu ni taratibu  ya maisha au kwa sababu wanadhani ndio jambo ambalo mwanamme analihitaji haswa haswa ni huyo mwanaume afike kileleni yaishe. Hata hivyo kwa mpenzi  wako wa kweli kweli, anahitaji zaidi tuu ya yeye kufika kileleni. Anahitaji akuone na kuhisi kweli kuwa nawe mwanamke unafurahia mapenzi.

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Related Posts

Raha ya ndoa ni nini wanandoa

June 25, 2025

DAWA YA KUMSAHAU MTU USIMUWAZE TENA

June 20, 2025

Jinsi ya Kumsahau Mpenzi Wako Aliyekuacha – Hatua 10 za Kuachilia na Kuendelea na Maisha

June 20, 2025

Dawa ya kuachana na mpenzi wako

June 20, 2025

Ukiachwa Ufanye Nini? – Hatua za Kupona, Kusimama na Kuendelea na Maisha kwa Amani

June 20, 2025

Namna ya kuachana na mpenzi uliyempenda

June 20, 2025
Leave A Reply Cancel Reply

Latest Posts

Nafasi 137 za Kazi Kutoka UTUMISHI – Taasisi Mbalimbali Juni 2025

June 13, 2025

Nafasi 83 za Kazi Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) June 2025

June 12, 2025

Nafasi za Kazi – NARCO (Kampuni ya Ranchi za Taifa) – Juni 2025

June 12, 2025

Majina ya Walioitwa kazini Ajira Portal Utumishi PSRS 2025 PDF Download

June 12, 2025

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI na Ajira Portal 2025

June 12, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.