JIUNGE NASI WHATSAPP
BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM
BOFYA HAPA
Tunapoingia katika mahusiano, tunatarajia furaha, upendo, na mshikamano, lakini mafanikio ya mahusiano hayaji kwa urahisi. Ili kujenga mahusiano imara na yenye furaha, ni muhimu kujua vitu vya kuzingatia ili kuepuka migogoro, kuimarisha uhusiano, na kufanikisha malengo ya pamoja.
Mwanzo wa Mahusiano
Msidanganyane(a)Mwambie mwenzi wako ukweli.
(b)Mwambie yale unayopenda na usiyopenda.
(c)Kuwa muwazi kwa mwenzi wako.
(d)Onyesha upo tayari kuachana na mambo yote uliyokuwa umeyazoea ambayo kwa sasa yanaweza bomoa uhusiano wenu.
Mfanye Mwenzako Ajisikie ni wa Muhimu
(a)Tenga muda maalumu wa kuwa naye.
(b)Onyesha unafurahia uwepo wake.
(c)Mnapozungumza jambo onyesha umakini kwa kumsikiliza na kuacha kila kitu.
(d)Usijifanye unajua kila kitu na kwamba yeye hajui.
(e)Hata anapokosea mwonye tu na kumuelekeza kwa upendo.
Usifanye Mambo Kwa Mazoea
(a)Kila siku ona ni fursa mpya ya kufanya jambo kwa ajili ya koboresha uhusiano wenu.
(b)Mfanyie jambo jipya ambalo hategemei kwamba utamfanyia.
(c)Usifanye jambo litakalomfanya ajione hana thamani tena kwako.
Usipende Kushikilia Mambo Kwa Mda Mrefu Bila Kusamehe
Anapokosea mweleze kwa upendo na umwambie umemsamehe.
Usiwe mtu wa kurudiarudia mambo kila anapokosea unakusanya makosa anapokosea tena unamkumbusha.
Kumbuka Aliwaacha Wengi Akaamua Kuwa na Wewe
Sasa usijifanye wewe ni mjanja kuliko wote.
Mwonyeshe yeye ni wa kipekee.
Usipende kila wakati kuelezea mambo ya mpenzi wako wa zamani.
Onyesha Hisia Za Kweli Kwake
Kumkumbatia mnapokuwa faragha.
Kumbusu na kumwambia maneno matamu,wengine husema maneno yanayovunja mifupa.
Mfano:Nakupenda wewe tu mpenzi wangu,hakika siwezi kukuacha mpenzi wangu, Unaniweza wewe tu mahabuba.
Mtosheleze
Husika na mahitaji yake ya kimwili na kihisia.Hakikisha anajisikia vizuri anapokuwa kwa kumtimizia mahitaji yake ambayo una uwezo nayo yale usiyoweza shaurianeni. Jambo analolipenda lipe kipaumbele. Tendo la ndoa au mapenzi yafanyike kwa usahihi na kwa kutoshelezana. “Watu wengi wakishazoeana tu wakazaa watoto basi wanaona tendo la ndoa siyo jambo la muhimu ni swala la dharura,na ndio utapata malalamiko mengi kwa wanandoa ama wapenzi wakisema zamani tulikuwa vizuri ila sasa amebadilika.”
JIUNGE NASI WHATSAPP
BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM
BOFYA HAPA