Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ni sehemu muhimu katika malezi ya vijana wa Tanzania. Lengo kuu la JKT ni kuwajengea vijana uwezo wa kiusalama, uzalendo, na kuleta mchango katika maendeleo ya taifa. Kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa, kila mwaka vijana wanaomaliza masomo ya sekondari wanahitajika kujiunga na JKT kwa mafunzo ya kijeshi na kitaifa. Hata hivyo, ili kufanya mafunzo haya kwa ufanisi, kuna orodha ya vitu muhimu ambavyo kila mwajiriwa anapaswa kuwa navyo.
Katika makala hii, tutajadili vitu vya kwenda navyo JKT kwa mujibu wa sheria, na umuhimu wa kila kimoja cha vitu hivyo ili kuwa na mafanikio katika mafunzo haya.
Vifaa vinavyohitajika Kwa Vijana wa Kujiunga na Mafunzo ya )JKT kwa Mujibu wa Sheria 2024 ni kama vifuatavyo
- Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni, iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
- T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest).
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
- Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Track suit ya rangi ya kijani au blue.
- Nyaraka zote zinazohitajika katika Udahili wa Kujiunga na Elimu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vya Kuhitimu kidato cha Nne nk.
- Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.