Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kupitia Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imetangaza nafasi mpya za kazi kwa Watanzania wenye sifa stahiki. Tangazo hili limetolewa tarehe 12 Septemba 2025 na linahusu jumla ya nafasi tano (05) kama ifuatavyo:
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi II – Nafasi 3
Majukumu ya kazi
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali.
Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao.
Kutunza kumbukumbu, miadi na ratiba za vikao/safari.
Kutafuta na kusambaza majalada.
Kuandaa dondoo na vifaa vya vikao.
Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
Sifa za mwombaji
Awe amehitimu Kidato cha Nne.
Awe na Stashahada ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili.
Awe amefaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika.
Awe na ujuzi wa matumizi ya kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, Publisher).
Mshahara: TGS C kwa mwezi.
2. Dereva Daraja II – Nafasi 2
Majukumu ya kazi
Kukagua gari kabla na baada ya safari.
Kuwapeleka watumishi katika safari za kikazi.
Kufanya matengenezo madogo ya gari na usafi.
Kusambaza nyaraka na kutunza taarifa za safari.
Sifa za mwombaji
Awe amehitimu Kidato cha Nne.
Awe na leseni ya Daraja C au E na uzoefu wa mwaka 1 bila ajali.
Awe amehudhuria mafunzo ya udereva (Basic Driving Course – VETA au chuo kinachotambuliwa).
Mshahara: TGS B kwa mwezi.
Masharti ya Jumla
Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18–45.
Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba.
Maombi yaambatane na CV, vyeti vya elimu/taaluma vilivyothibitishwa, barua ya maombi, anuani na majina ya wadhamini watatu.
Vyeti vya “Result slips” havitakubalika.
Waombaji waliostaafu au walioko serikalini hawaruhusiwi bila kibali maalum.
Mwisho wa kutuma maombi: 25 Septemba 2025.
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya kielektroniki kupitia mfumo wa ajira: 👉 https://portal.ajira.go.tz
Download Tangazo la kazi katika PDF File

