Ifahamike kwamba, mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa muda wote wa kipindi chake Cha ujauzito.
Hatoshauriwa au kuruhusiwa kushiriki tendo la ndoa Kama ujauzito wake unachangamoto Kama vile MIMBA kutishia kutoka, anaumwa, ameshonwa mlango wa kizazi, anatokwa na damu n.k.
Mitindo ya ufanyaji tendo la ndoa wakati wa ujauzito, hubadilika kadri MIMBA inavyokuwa kubwa.
Mitindo Bora zaidi Ni ile ambayo haitochosha Wala kuleta maumivu, vyema zaidi utumike mtindo wa ubavu ubavu, mwanamke kukaa kwa juu au dog staili.
Mjamzito anapaswa kuepuka mitindo ambayo itampa maumivu ya tumbo au kumchosha zaidi. Aepuke mtindo utakao mfanya alalie mgongo kwa muda mrefu, staili ya kulalia mgongo “kifo Cha mende” kinaweza msababishia mjamzito ashindwe kupumua vizuri na kumletea shida au staili ya kulalia tumbo inaweza mkandamiza mtoto na kumsabishia matatizo.
Ikumbukwe sio kila mwanamke atakuwa na Hamu ya kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito wake hivyo asilazimishwe kufanya hivyo Kama hayuko ridhaa.
Soma hii :Njia rahisi ya Kuitambua Siku ya Kubeba mimba
Staili Salama za Kufanya Mapenzi Wakati wa Ujauzito
Mwanamke Ameketi :
Mwanamke anaweza kuketi juu ya mumewe, hii inamruhusu kudhibiti kina na kasi.Hii ni staili nzuri kwa sababu inampa mwanamke udhibiti zaidi juu ya kina na jinsi anavyohisi. Hii pia hupunguza shinikizo kwenye tumbo lake.
Mwanamume Ameketi
Mwanamume anaweza kuketi kwenye kiti au kitanda huku mwanamke akiwa juu yake.Katika staili hii, mwanamume anakuwa kwenye kiti au kitanda, ambayo inasaidia kuondoa uzito kutoka kwa tumbo la mwanamke.
Mwanamke Kulala Kando:
Hii ni staili salama sana kwani inasaidia kupunguza shinikizo kwenye tumbo la mwanamke na inaruhusu urahisi katika kufanya tendo.
Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Kufanya Mapenzi
Ni muhimu kuzingatia mambo kadhaa ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto:
- Wasiliana na Daktari: Ni vyema kuzungumza na daktari kabla ya kuanza kufanya mapenzi ili kupata ushauri sahihi.
- Kusikiliza Mwili Wako: Ikiwa unahisi maumivu au discomfort yoyote, ni bora kusitisha shughuli hiyo.
- Kuepuka Staili Zenye Hatari: Staili ambazo zinahitaji mwanamke kulala tumboni zinapaswa kuepukwa kabisa.