Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » Sifa na Vigezo vya Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania
Elimu

Sifa na Vigezo vya Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania

BurhoneyBy BurhoneyMarch 21, 2025Updated:March 21, 2025No Comments3 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
Sifa na Vigezo vya Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania
Sifa na Vigezo vya Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Jeshi la Polisi Tanzania kila mwaka Hutangaza Nafasi za kujiunga kulitumikia Jeshi hilo kwa Vijana wa Kitanzania wenye Sifa na Vigezo,Makala hii imekuorodheshea sifa zote unazopaswa kuwa nazo ili kuchaguliwa kujiunga kulitumikia jeshi la polisi.

Vigezo na sifa za kujiunga na jeshi la polisi

Vigezo na sifa za kujiunga na jeshi la polisi

Ili kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania mwombaji anatakiwa kutimiza sifa zifuatazo:

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 25 kwa waombaji wa kidato cha nne, sita, na astashahada.
  2. Au kati ya miaka 18 na 30 kwa waombaji wa shahada na stashahada.
  3. Waombaji wa kidato cha nne wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2018 hadi 2023 na wawe na daraja la I hadi IV, wenye daraja la IV wawe na alama 26 hadi 28.
  4. Waombaji wa kidato cha sita wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2018 hadi 2023 na wawe na daraja la I hadi III.
  5. Waombaji wa astashahada, stashahada, na shahada wawe wamehitimu katika fani zinazohitajika na Jeshi la Polisi.
  6. Wanaume wawe na urefu usiopungua futi 5 na inchi 8, wanawake wawe na urefu usiopungua futi 5 na inchi 4.
  7. Mwombaji awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA.
  8. Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  9. Pia, anatakiwa kuwa na afya njema ya kimwili na kiakili, iliyothibitishwa na daktari wa serikali.
  10. Aidha, mwombaji anatakiwa awe hajaoa/kuolewa na hana mtoto.
  11. Ni sharti pia kwamba hajawahi kutumia dawa za kulevya na yuko tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya polisi.
  12. Mwombaji hapaswi kuwa ameajiriwa na taasisi yoyote ya serikali.
  13. Zaidi ya hayo, anatakiwa kuwa tayari kufanya kazi za polisi popote nchini Tanzania, kujigharamia katika hatua zote za usaili, asiwe na alama za kuchorwa mwilini, na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
SOMA HII :  Chuo cha Ualimu Songea Teachers College Courses na Sifa za Kujiunga

SOMA HII : Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu

Mchakato wa Kutuma Maombi ya Kazi Jeshi la Polisi

Ili kuomba nafasi za kazi kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania, fuata maelekezo yafuatayo hapa chini.

Andika barua ya maombi

Mwombaji anatakiwa kuandika barua ya maombi kwa mkono wake mwenyewe (handwriting). Katika barua, ni muhimu kuhakikisha kuwa namba za simu za mwombaji zimeandikwa kwa usahihi. Barua hii itumwe kwa anuani ifuatayo:

Mkuu wa Jeshi la Polisi
S.L.P 961
DODOMA

Omba kupitia mfumo wa mtandaoni

Baada ya kutuma barua ya maombi, mwombaji anatakiwa kuwasilisha maombi yake kupitia mfumo wa ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL). Mfumo huu unapatikana kwenye tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi: ajira.tpf.go.tz

Ni muhimu kuzingatia kwamba hatua zote mbili, yaani kutuma barua ya maombi na kuomba kupitia mfumo wa mtandaoni, ni lazima zifuatwe ili maombi ya mwombaji yaweze kuzingatiwa.

Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

WhatsApp Group Join Now
Telegram Group Join Now

Related Posts

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Pwani (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 13, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Njombe (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 13, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Mwanza (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 13, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Mtwara (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 13, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Morogoro (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 13, 2025

Orodha ya Vyuo ya Ualimu Vilivyopo Mkoa wa Mbeya (Ngazi ya Cheti na Diploma)

November 13, 2025

Comments are closed.

Latest Posts

Majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Kusimamia Uchaguzi October 2025 :INEC Tume ya Taifa ya Uchaguzi

October 19, 2025

Majina ya Walioitwa kwenye Usaili kusimamia uchaguzi 2025 – INEC Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

October 12, 2025

Nafasi 70 Za Kazi Unitrans Tanzania Limited Madereva wa Malori 2025

September 17, 2025

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wilaya ya Karatu 2025

September 13, 2025

Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo 2025

September 13, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.