Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) nchini Tanzania imeanza rasmi huduma za abiria kati ya Dar es Salaam, Morogoro, na Dodoma. Huduma hizi mpya zimeboresha usafiri kwa kasi na ufanisi zaidi.
Ufahamu Kwa Ufupi Mradi wa Treni ya SGR
Mradi wa Standard Gauge Railway (SGR) ni zaidi ya reli tu; ni mageuzi makubwa katika mfumo wa usafiri na uchumi wa Tanzania. SGR ni reli ya kisasa yenye upana wa mita 1.435, kiwango cha kimataifa kinachokubalika na kutumika sana duniani kote. Upana huu wa reli huwezesha usafirishaji wa mizigo mizito zaidi kwa safari moja, na pia huruhusu treni kusafiri kwa kasi ya juu zaidi kuliko reli za kawaida.
Serikali ya Tanzania, kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), imeanzisha mradi huu ili kuunganisha mikoa mbalimbali na nchi jirani kama Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Reli hii itapita katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, na Katavi, na itakuwa na uwezo wa kupitisha treni za umeme zenye mwendo wa kilometa 160 kwa saa.
Ratiba Mpya ya Treni Za Mwendokasi SGR: Dar – Morogoro – Dodoma
Kwa mujibu wa ratiba mpya, kuna treni za aina mbili zinazotolewa: Haraka (Express) na Kawaida (Ordinary). Ratiba hizi zinajumuisha muda wa kuondoka na kufika kwa treni kati ya vituo vikuu vya Dar es Salaam (DSM), Morogoro (MOR), na Dodoma (DOM).
1. Treni ya Haraka (Express)
Treni za haraka zinajulikana kwa kasi yake na muda mfupi wa safari. Ratiba ya safari za Treni ya Haraka ni kama ifuatavyo:
- Kuondoka DSM (Dar es Salaam):
- Saa 12:00 Asubuhi
- Saa 11:15 Alfajiri
- Kuwasili Morogoro (MOR):
- Saa 1:40 Asubuhi kwa treni ya saa 12:00 Asbh
- Saa 1:12 Asubuhi kwa treni ya saa 11:15 Alfajiri
- Kuondoka Morogoro:
- Saa 1:45 Asubuhi
- Saa 1:17 Asubuhi
- Kuwasili Dodoma (DOM):
- Saa 3:42 Asubuhi kwa safari ya treni ya saa 12:00 Asbh
- Saa 2:53 Asubuhi kwa safari ya saa 11:15 Alfajiri
2. Treni ya Kawaida (Ordinary)
Treni za kawaida huchukua muda mrefu zaidi kutokana na kuacha katika vituo vingi njiani. Ratiba ya safari hizi ni kama ifuatavyo:
- Kuondoka DSM (Dar es Salaam):
- Saa 3:30 Asubuhi
- Kuwasili Morogoro (MOR):
- Saa 5:15 Asubuhi
- Kuondoka Morogoro:
- Saa 5:20 Asubuhi
- Kuwasili Dodoma (DOM):
- Saa 7:25 Mchana
Pia, kuna safari za kawaida kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam:
- Kuondoka DOM (Dodoma):
- Saa 8:10 Mchana
- Saa 11:15 Jioni
- Saa 12:55 Usiku
Safari hizi husababisha kufika Morogoro kati ya saa 10:15 Jioni hadi saa 2:51 Usiku, na kutoka hapo kuelekea DSM kwa nyakati tofauti kulingana na safari iliyochaguliwa.
Ratiba Mpya ya Treni ya Kawaida Dar es Salaam – Morogoro
Kwa wale wanaosafiri kati ya Dar es Salaam na Morogoro pekee, kuna huduma za treni za kawaida zenye ratiba ifuatayo:
- Kuondoka Morogoro (MOR):
- Saa 3:50 Asubuhi
- Kuwasili Dar es Salaam (DSM):
- Saa 5:40 Asubuhi
- Kuondoka DSM (Dar es Salaam):
- Saa 10:00 Jioni
- Kuwasili Morogoro (MOR):
- Saa 11:40 Jioni
Vitu vya Kuzingatia Kabla ya Kusafiri
- Fika kituoni mapema ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho.
- Hakikisha una tiketi halali ya kusafiria.
- Kumbuka kuzingatia kanuni na taratibu za usafiri wa reli.
Usiyopaswa Kufanya Wakati wa Kusafiri na Treni ya SGR
Ili kuhakikisha safari yako na treni ya SGR ni salama, starehe, na inafuata kanuni na taratibu, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
Vitu Visivyokubalika
- Mifuko ya plastiki
- Silaha za aina yoyote
- Chakula na vinywaji (isipokuwa vile vinavyouzwa ndani ya treni)
- Ndoo na mapipa
- Wanyama (wa kufugwa au wa porini)
- Mizigo yenye uzito unaozidi kilo 30 kwa daraja la biashara na kilo 25 kwa daraja la uchumi.
Usalama
- Usivute sigara ndani ya treni.
- Usiache mizigo yako bila uangalizi.
- Ripoti kwa wafanyakazi wa treni ikiwa utaona kitu chochote cha kutia shaka.