Yesu Kristo ni mmoja wa watu mashuhuri zaidi katika historia, lakini swali la sura yake halisi limekuwa mjadala kwa karne nyingi. Hakuna picha halisi ya Yesu iliyopatikana, kwani hakukuwa na teknolojia ya upigaji picha katika nyakati zake, na maandiko ya Biblia hayaelezi kwa kina muonekano wake wa kimwili. Hata hivyo, tafiti mbalimbali za kihistoria, kisayansi, na kisanii zimejaribu kuleta taswira inayoweza kuakisi sura yake halisi.
Maelezo ya Biblia Kuhusu Muonekano wa Yesu
Biblia haielezi moja kwa moja jinsi Yesu alivyoonekana, lakini kuna maandiko yanayoweza kutoa mwanga fulani. Katika Isaya 53:2, Yesu anaelezewa kuwa “hakuwa na umbo wala uzuri wa kutuvutia.” Hili linaweza kumaanisha kuwa hakuwa na sifa za kipekee za kimwili ambazo zingemtofautisha na watu wa kawaida wa wakati huo.
Utafiti wa Kisayansi na Kihistoria
Watafiti wa historia na wanasayansi wamejaribu kubaini muonekano wa Yesu kwa kuzingatia sifa za Wayahudi wa Karne ya Kwanza huko Mashariki ya Kati. Mnamo mwaka 2001, wataalamu wa uhalifu na watafiti wa anatomy walitumia teknolojia ya kompyuta kuunda picha inayowezekana ya mtu wa Kiyahudi wa wakati huo. Picha hiyo ilimwonyesha mtu mwenye ngozi ya kati (si nyeupe wala nyeusi), nywele fupi zilizochafuka, na ndevu nene, tofauti na picha nyingi za Yesu zilizochorwa katika sanaa ya Magharibi.
Taswira ya Yesu Katika Sanaa
Kwa karne nyingi, wasanii wamemchora Yesu kwa mtindo wa tamaduni zao. Katika sanaa ya Magharibi, Yesu mara nyingi ameonyeshwa akiwa na ngozi nyeupe, nywele ndefu, na macho ya samawati, lakini hii ni tafsiri ya kitamaduni zaidi kuliko kihistoria. Katika sanaa ya Kikristo ya Kati na Mashariki, Yesu anaonyeshwa na nywele za giza na ngozi ya kati.
Turini ya Turin (Shroud of Turin)
Turini ya Turin ni kitambaa chenye alama za mtu aliyesulubiwa, ambacho baadhi ya watu wanaamini kuwa kilifunika mwili wa Yesu baada ya kifo chake. Ingawa hakuna uthibitisho wa kisayansi wa moja kwa moja kwamba ni cha Yesu, picha inayotokana na kitambaa hicho imekuwa moja ya sura zinazodhaniwa kuwa za Yesu.
Je sura halisi ya Yesu ilikuwa ipi ?
Kila mtu anamtambua Yesu.
Uso wake umechorwa zaidi ya nyuso zote duniani, na anatambulika kila mahali na wasanii wa Kizungu kama jamaa aliyevaa kanzu, ana kidevu kirefu sawa na nywele.
Lakini je, alikuwa anafanana hivi kweli ?
Huenda ikawa sivyo.
Kwa kweli sura hii inayotambuliwa huenda ilibuniwa karne nne baada ya kuzaliwa kwake , nyakati za Ufalme ya Byzantium.
Usanii wa wakati huo ulikuwa usanii elezi tu, sio ya uhalisi.
Usanii huo ulifanya kwa taswira ya ufalme wa kirumi, tunavayoona kwa mchiri wa kanisa la Santa Pudenziana iliyoko jijini Rome Utaliana.
Chanzo cha picha, Alamy
Wasanii wa Byzantino walimchora Yesu kama mdogo wake Zeus, mungu wa Kigiriki.
Huku miaka ikipita, leo hii sura yake imeundwa kwa miongozo ya awali na kutambulika kwa pamoja kama sura inayokubalike ya Yesu.
Lakini sura yake haswa ilikuwaje?
1. Nywele na Ndevu
Wakato wakristo wa zamani hakuwa wanamuonyesha kama Mungu, walieleza kuwa Yesu alikuwa tu binadamu kama mwengine, bila ndevu na mwenye nywele fupi.
Katika karne ya kwanza wakati wa Ufalme wa Ugiriki na warumi, wanaume walitakiwa kuwa na nywele fupi.
Hata wanafilosofia walinyoa nywele zao.
Kwa hivyo Yesu, kama mwana filosofia, huenda pia alikuwa na ndevu fupi, na pia huenda nywele yake haikuwa ndefu kama vile tunavyodhania.
2. Mavazi
Chanzo cha picha, Alamy
Wakati wa Yesu, mabwanyeye walivalia kanzu wakati wa sherehe maalum ili kuonyesha ukubwa wao .
Katika Biblia, Yesu pia aonya kwenye mafunzo yake, alipokuwa akifundisha, Yesu alisema,
“Jihadharini na walimu wa sheria”.
”Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu na kusalimiwa kwa heshima masokoni.”
Chanzo cha picha, Alamy
Pia wao hupenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa nafasi za he shima katika karamu.”
(Marko 12; 38-39).
Matamshi ya Yesu huaminika kuwa ya kweli kwenye vitabu vya Injili, kwa hivyo twaezang’amua kuwa Yesu mwenyewe hakuvalia kanzu.
3. Miguu
Miguuni Yesu huenda alivaa lapulapu.
Kila mtu alikuwa akivaa lapulapu wakati huo.
4. SURA
Yesu alikuwa Yahudi.

Kwa hivyo alifananaje kama myahudi mwenye miaka thelathini alipoanza kuhubiri kama ilivyonenwa katika kitabu cha Luka?
Mnamo mwaka wa 2001 mwanasayansi Richard Neave aliundia BBC umbo la mwana Galilaya, kwa kipindi kilichoitwa “Mwana wa Mungu.’
Hakusema ilikuwa sura yake Yesu.
Ila umbo hilo lilikuwa la kuwapa watu taswira ya mwanaume kama Yesu nyakati na karne aliyokuwa hai.