Kujua siku ambayo mwanamke ana uwezekano mkubwa wa kushika mimba ni muhimu kwa wale wanaotafuta kupata ujauzito au kuepuka mimba zisizotarajiwa. Siku hizi hujulikana kama siku za rutuba, ambazo ni zile zinazotangulia na kufuatia siku ya ovulation.
Yai kupevuka
Kwa wanawake wengi yai linapevuka siku ya 14 kwenye mzunguko. Japo kufanya tendo la ndoa wakati upo period au nyakati zingine ambazo siyo siku ya 14 siyo kigezo cha kutoshika mimba kwa aslimia mia. Bado mimba inaweza kuingia katika kipindi kingine mfano ukifanya tendo kipindi cha hedhi.
Unajuaje siku za hatari kushika mimba?
1. Kufuatilia Mzunguko wa Hedhi
Kujua mzunguko wako wa hedhi ni hatua ya kwanza. Mzunguko wa kawaida ni kati ya siku 21 hadi 35, lakini wastani ni siku 28. Ovulation hutokea takriban siku 14 kabla ya kuanza kwa hedhi inayofuata.
2. Kutumia Kalenda ya Ovulation
Kwa kutumia kalenda ya hedhi, unaweza kufuatilia mzunguko wako wa kila mwezi na kukadiria siku za rutuba. Ikiwa una mzunguko wa kawaida wa siku 28, basi ovulation hutokea siku ya 14, na siku zinazofaa kushika mimba ni kati ya siku ya 10 hadi 16.
3. Kupima Joto la Mwili la Asubuhi (Basal Body Temperature – BBT)
Joto la mwili huwa la chini kabla ya ovulation na huongezeka kidogo baada ya ovulation. Kwa kupima joto lako kila asubuhi kabla ya kuamka, unaweza kuona mabadiliko haya na kutambua siku zako za rutuba.
4. Kuangalia Mabadiliko ya Majimaji ya Kizazi
Wakati wa ovulation, majimaji ya uke huwa meupe, yanavutika kama yai bichi, na yanateleza zaidi. Hii ni ishara kwamba mwili uko tayari kwa ujauzito.
5. Kutumia Vipimo vya Ovulation
Vipimo hivi vinapatikana madukani na hupima viwango vya homoni ya luteinizing hormone (LH) kwenye mkojo. LH huongezeka sana saa 24-48 kabla ya ovulation, hivyo kupima kunaweza kusaidia kujua siku yako ya rutuba.
6. Kusikiliza Ishara za Mwili
Baadhi ya wanawake huhisi maumivu madogo upande mmoja wa tumbo (mittelschmerz) wakati wa ovulation. Dalili nyingine zinaweza kuwa kuongezeka kwa hamu ya tendo la ndoa na matiti kuhisi maumivu kidogo.
7. Kutumia Teknolojia na Programu za Simu
Kuna programu nyingi za simu kama Flo, Clue, na Ovia zinazosaidia kufuatilia mzunguko wa hedhi na kutabiri siku za rutuba kwa usahihi zaidi.
Je mimba yaweza kuingia kipindi cha hedhi?
Kwa wanawake wenye mzunguko mfupi yani siku 28 mpaka 30 kuna uwezekano wa kushika mimba hata ukifanya tendo wakati wa hedhi. Kutumia kinga kama kondomu bado ni njia ya uhakika zaidi ya kukuepusha kushika mimba usiyoitarajia. Soma zaidi kujua jinsi ya kupanga siku za kukutana na mme wake ili uepuke kushika mimba