JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetoa rasmi Ratiba ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) kwa mwaka 2025, ambao unatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo mwezi Oktoba. Mitihani hii ni hatua muhimu kwa wanafunzi wa darasa la nne katika kupima kiwango cha maarifa waliyojifunza kwa kipindi cha miaka minne ya elimu ya msingi.

Tarehe Rasmi za Mitihani:

  • Jumatano: 22 Oktoba 2025

  • Alhamisi: 23 Oktoba 2025

RATIBA KAMILI YA MTIHANI WA SFNA 2025

NECTA Ratiba ya Mtihani wa Taifa Darasa la nne (SFNA) 2025

Siku ya Kwanza – Jumatano, 22 Oktoba 2025

MudaNamba ya SomoSomo
2:00 – 3:30 JioniS09 / S09ESayansi / Science
3:30 – 4:30 JioniMapumziko
4:30 – 6:00 JioniM08 / M08EHisabati / Mathematics
6:00 – 8:00 JioniMapumziko
8:00 – 9:30 UsikuA06 / A06EJiografia na Mazingira: Sanaa na Michezo / Geography and Environment: Arts and Sports

Siku ya Pili – Alhamisi, 23 Oktoba 2025

[Soma: Kozi Bora Za Kusoma Chuo Kikuu Tanzania Zenye Ajira Nyingi 2025/2026 ]

MudaNamba ya SomoSomo
2:00 – 3:00 JioniL01Kiswahili
3:00 – 4:00 JioniMapumziko
4:00 – 5:00 JioniL02English Language
5:00 – 5:30 JioniMapumziko
5:30 – 6:30 JioniL03 / L04 / L05French Language / Lugha ya Kiarabu / Lugha ya Kichina
6:30 – 8:00 JioniMapumziko
8:00 – 9:30 UsikuA07Historia ya Tanzania na Maadili

Maelezo Muhimu kwa Wazazi, Walimu na Wanafunzi

  • Watoto wote wanapaswa kuwasili shuleni mapema kabla ya muda wa mtihani.

  • Hakikisheni wanafunzi wamepata usingizi wa kutosha usiku kabla ya mtihani.

  • Vifaa vya lazima kama penseli, kalamu na rula viandaliwe mapema.

  • Walimu wahakikishe kuwa wanafunzi wanajua vizuri utaratibu wa mitihani na ratiba husika.

Ushauri kwa Wazazi

  1. Watie moyo watoto — Waambie kuwa wanachohitaji ni kufanya juhudi na kuamini uwezo wao.

  2. Wape mazingira ya utulivu nyumbani — Epuka kelele au mambo yanayoweza kuwatoa kwenye mwelekeo wa kusoma.

  3. Wakumbushe kula chakula bora — Hasa vyakula vinavyosaidia uwezo wa kufikiri kama samaki, karanga na matunda.

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Share.

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Leave A Reply