Ajira Portal ni mfumo rasmi wa serikali ya Tanzania unaotumika kwa kutangaza na kushughulikia ajira katika sekta ya umma. Kwa mwaka 2025, Ajira Portal inaendelea kuwa njia kuu ya waombaji wa kazi kuwasilisha maombi yao serikalini. Ikiwa unatafuta ajira ya serikali au unahitaji kuelewa mchakato mzima wa kujiunga na kutuma maombi kupitia portal hii, basi makala hii imekufaa.
Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Kupitia Ajira Portal 2025
Kila siku, Ajira Portal hupokea na kuchapisha tangazo la nafasi mpya za ajira kutoka taasisi mbalimbali za umma kama:
Wizara mbalimbali (Afya, Elimu, Kilimo, Uchukuzi n.k.)
Halmashauri na Manispaa
Vyuo vya Serikali
Hospitali na vituo vya afya vya umma
Mashirika ya Umma
NAFASI 68 za Kazi Ajira Portal June 2025
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 9 POST
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 4 POST
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 4 POST
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 4 POST (Nyang’hwale)
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 5 POST (Biharamulo)
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 5 POST (Singida)
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 5 POST (Songea)
- OFFICE MANAGEMENT SECRETARY II – 2 POST
- ONBOARD ATTENDANT II – 2 POST
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 2 POST (Madaba)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 7 POST (Madaba)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST (Mvomero)
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 6 POST (Ushetu)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 5 POST (Tanganyika)
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 3 POST (Ukerewe)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 3 POST (Sumbawanga)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – 5 POST (Ukerewe)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 4 POST (Biharamulo)
Angalia tangazo kamili na mahitaji ya kila nafasi moja kwa moja kupitia tovuti ya Ajira Portal: https://portal.ajira.go.tz
Jinsi ya Kujiunga na Ajira Portal (Kujisajili)
Kama huna akaunti bado, fuata hatua hizi:
Fungua Tovuti Rasmi: Tembelea https://portal.ajira.go.tz
Bonyeza “Register” au “Jisajili”
Jaza taarifa zako binafsi: Jina, Namba ya NIDA, barua pepe, namba ya simu n.k.
Chagua jina la mtumiaji (username) na neno siri (password)
Thibitisha kupitia email utakayotumiwa
Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia email/username na password
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kazi Kupitia Ajira Portal
Ingia kwenye akaunti yako https://portal.ajira.go.tz
Jaza Profile yako kikamilifu:
Taarifa binafsi
Elimu
Uzoefu wa kazi
Lugha
Vyeti vya kitaaluma (upload)
Tafuta Nafasi ya Kazi unayotaka:
Nenda kwenye “Vacancies”
Tafuta kwa jina la kazi au taasisi
Soma Tangazo la Kazi kwa Umakini
Angalia sifa zinazohitajika
Kumbuka tarehe ya mwisho ya kutuma maombi
Bonyeza “Apply”
Thibitisha maombi yako
NB: Hakikisha profile yako imejazwa kikamilifu kabla ya kutuma maombi – profile incomplete = maombi hayatatumwa.
Jinsi ya Kurekebisha au Kurejesha (Reset) Password Ajira Portal
Je, umesahau password yako? Usihofu. Fanya yafuatayo:
Fungua tovuti ya Ajira Portal: https://portal.ajira.go.tz
Bonyeza “Forgot Password?”
Weka Email uliyosajili nayo
Utaona ujumbe: “A link to reset your password has been sent to your email.”
Fungua email yako, bonyeza link ya reset
Weka password mpya
Thibitisha password mpya kisha login tena
Ikiwa huoni email ya reset, angalia kwenye Spam/Junk Folder au subiri dakika chache.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
Jaza profile kwa ukamilifu kabla ya kuanza kutuma maombi
Hakikisha vyeti vyote viko katika mfumo wa PDF
Usitumie simu janja kutuma maombi ya ajira – tumia kompyuta kwa urahisi zaidi
Angalia Ajira Portal kila siku kwa nafasi mpya
Tuma maombi mapema usisubiri siku ya mwisho [Soma: Majina ya Walioitwa Kazini TRA 2025 PDF Download ]
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
Je, ninaweza kutuma maombi ya kazi zaidi ya moja kwa siku moja?
Ndiyo, unaweza kutuma maombi ya nafasi zote unazotimiza vigezo vyake.
Je, kuna gharama yoyote ya kutuma maombi kwenye Ajira Portal?
Hapana, huduma zote ni bure. Usitoe fedha kwa mtu yeyote.
Ajira Portal inaendeshwa na nani?
Ajira Portal inaendeshwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS).
Ninawezaje kujua kama maombi yangu yamepokelewa?
Utaona ujumbe *“Successfully Applied”* kwenye nafasi hiyo baada ya kutuma maombi.
Je, ninaweza kubadili taarifa kwenye profile yangu baada ya kutuma maombi?
Baada ya kutuma maombi, huwezi kubadili taarifa mpaka tangazo hilo lifungwe.
Nawezaje kujua nafasi mpya za kazi kila siku?
Tembelea [https://portal.ajira.go.tz](https://portal.ajira.go.tz) kila siku au fuatilia mitandao ya kijamii ya Sekretarieti ya Ajira.
Ajira Portal iko wazi muda gani?
Portal iko wazi masaa 24 kila siku. Maombi yanapokelewa hadi tarehe ya mwisho ya tangazo.
Ninahitaji kuwa na vyeti gani kabla ya kujiunga?
Cheti cha kuzaliwa, NIDA, vyeti vya kitaaluma (CSEE, ACSEE, Diploma, Degree n.k.), na pasipoti size photo.
Je, lazima niwe na cheti cha NIDA?
Ndiyo. Namba ya NIDA ni mojawapo ya mahitaji ya msingi ya kujisajili.
Ajira Portal inafanya kazi kwenye simu?
Ndiyo, lakini kwa utendaji bora zaidi, tumia kompyuta au laptop.