Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji 2025

Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji 2025
Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji 2025

Jeshi la Uhamiaji Tanzania wametangaza Nafasi Mpya za kazi kwa Vijana wa kitanzania wanaokidhi Vigezo vya kulitumikia jeshi hilo ,Nafasi hizi zimetangazwa February 2025.

Hizi hapa Nafasi za Kazi kutoka Jeshi la Uhamiaji

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka niliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, natangaza nafasi za Ajira Mpya za Askari wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:-

SIFA ZA MWOMBAJI

  1. Awe ni raia wa Tanzania;
  2. Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
  • Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
  1. Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
  2. Awe na siha njema ya mwili na
  3. Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
  • Asiwe na Kumbukumbu au Taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;
  • Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;
  1. Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
  2. Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 22, Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Sita na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada/Stashahada ya Juu awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.
  3. Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote
  • Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la

MAOMBI YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE:

Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya Shahada/Stashahada ya Juu, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:-

SOMA HII :  Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI na Ajira Portal 2025

Mtaalamu wa Lugha za Kimataifa, Utawala, Sheria, Uhusiano, TEHAMA, Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi wa AC, Cyber Security, Brass band, na Mpiga chapa (Printer). Hizi hapa Nafasi za Kazi kutoka Jeshi la Uhamiaji

NAMNA YA KUFANYA MAOMBI:

MAOMBI yote ya Ajira yatawasilishwa kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni https://www.immigration.go.tz

About Burhoney 4807 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati