Nafasi 137 za Kazi Kutoka UTUMISHI – Taasisi Mbalimbali Juni 2025

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, imetangaza nafasi mpya 137 za ajira katika taasisi mbalimbali za umma. Tangazo hili limetolewa rasmi tarehe 12 Juni 2025, na linahusisha ajira kutoka taasisi kama TEMESA, TANROADS, TPSC, LGTI, TICD, na TAA.

Ikiwa wewe ni Mtanzania unayetafuta kazi serikalini, fursa hii ni muhimu sana kuzingatia. Hapa chini tumekufupishia majina ya taasisi, idadi ya nafasi zilizotangazwa, pamoja na sifa za msingi.

1. Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency (TEMESA)

TEMESA imetangaza jumla ya nafasi 32 katika maeneo yafuatayo:

  • Engineer II (Marine) – 2 nafasi

  • Ferry Captain II – 15 nafasi

  • Technician II (Mechanical) – 15 nafasi

Sifa ni pamoja na Shahada au Diploma zinazotambulika katika fani husika na usajili wa kitaaluma (kwa wahandisi).

2. Tanzania National Roads Agency (TANROADS)

TANROADS imetangaza nafasi 81 katika kada mbalimbali:

  • Land Surveyor II – 2 nafasi

  • Valuer II – 2 nafasi

  • Weighbridge Officer II – 50 nafasi

  • Assistant Laboratory Technician II – 10 nafasi

  • Driver II – 15 nafasi

  • Receptionist II – 2 nafasi

  • Office Management Secretary II – 2 nafasi

Sifa zinatofautiana kulingana na nafasi lakini kwa ujumla ni Shahada, Diploma au Cheti na uzoefu (hasa kwa madereva).

3. Tanzania Public Service College (TPSC)

TPSC imetangaza 10 nafasi za Assistant Lecturers katika fani zifuatazo:

  • Mathematics/Statistics – 4 nafasi

  • ICT – 2 nafasi

  • Law – 2 nafasi

  • Procurement/Supplies Management – 4 nafasi

  • Communication Skills – 2 nafasi

Waombaji wanapaswa kuwa na Shahada ya Uzamili (GPA ≥ 3.8) na Shahada ya Awali (GPA ≥ 3.5).

4. Local Government Training Institute (LGTI)

LGTI inahitaji watumishi 3 katika nafasi zifuatazo:

  • Assistant Lecturer (Public Administration) – 1 nafasi

  • ICT Officer II (Programming) – 2 nafasi

SOMA HII :  Mfumo wa Kutuma Maombi ya Ajira Za TRA (TRA Recruitment Portal Login)

Sifa kuu ni Shahada ya Uzamili (kwa mhadhiri) na Shahada ya kwanza (kwa ICT Officer).

5. Tengeru Institute of Community Development (TICD)

TICD imetangaza 5 nafasi za Assistant Lecturers:

  • Sociology – 1 nafasi

  • Community Development – 3 nafasi (Tangazo la Marudio)

  • Social Work – 1 nafasi (Tangazo la Marudio)

Sifa ni Shahada ya Uzamili GPA ≥ 3.8 na Shahada ya kwanza GPA ≥ 3.5.

6. Tanzania Airport Authority (TAA)

TAA inahitaji 2 Assistant Aircraft Marshallers. Sifa ni Cheti katika Utawala, Rasilimali Watu, Takwimu, Biashara, au fani inayofanana.

BONYEZA HAPA KUTUMA MAOMBI

About Burhoney 4806 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati