Nywele ni taji la mwanamke – na hakuna mtindo unaoonyesha ubunifu, haiba, na utambulisho wa Kiafrika kama rasta. Kutoka kwenye box braids hadi butterfly locs, mitindo ya rasta imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya wanawake wanaopenda muonekano safi, rahisi kutunza, na unaodumu kwa muda.
Box Braids (Rasta za Mstatili)
Huu ni mtindo maarufu sana unaoweza kuvaliwa kwa wiki 3 hadi 6. Nywele husukwa kwa sehemu za mstatili na huweza kuwa ndefu au fupi.
Kwa nini zipendwe?
Rahisi kutunza
Zinaweza kufungwa mitindo mingi: buns, ponytail, half-up-half-down
Zinapatikana kwa rangi tofauti (unaweza changanya rangi mbili au zaidi)
Knotless Braids
Toleo la kisasa la box braids – lakini bila “kidude” kwenye kiwanja cha nywele. Zinakuwa laini zaidi na hazivuti nywele zako.
Faida:
Haziumi unapomaliza kusuka
Nzuri kwa wale wenye ngozi ya kichwa laini
Zinaonekana natural sana
Passion Twists
Mitindo ya twist yenye muonekano wa curly na free-flowing. Ni laini, nyepesi na ya kupendeza sana.
Zinapendelewa kwa:
Harusi, matukio rasmi na vacation vibes
Wanawake wanaopenda muonekano wa asili na urahisi wa kutunza
Butterfly Locs
Locs zenye muonekano “messy” kwa makusudi – zinatengeneza style ya boho-chic.
Kwa nini ni trending?
Hazihitaji kuwa perfect – hiyo ndiyo charm yake!
Zinadumu hadi wiki 6–8
Nzuri kwa wale wanaopenda mitindo ya artistic na ya kipekee
Faux Locs / Distressed Locs
Zinatoa mwonekano wa dreadlocks bila kujitolea kwa kudumu. Faux locs huvaliwa kama protective style pia.
Unazivaa wapi?
Kazini, sherehe, au hata likizo
Zinapatikana kwa urefu tofauti – short bob hadi waist length
Bohemian Braids / Boho Rasta
Mchanganyiko wa braids za kawaida na curly strands zinazowachanganyika. Mtindo wa uhuru na ubunifu.
Tip:
Ongeza shanga au accessories ndogondogo kama pete au vitambaa vya nywele kuipa rasta zako uzuri zaidi.
Soma Hii :Aina za Rasta za Darling na Bei Zake
Cornrows / Lines (Mtindo wa Mistari)
Rasta zinazobandwa moja kwa moja kichwani. Ni classic na pia zipo kisasa – unaweza kuchanganya na curls au kushonea wig juu yake.
Perfect kwa:
Wanawake wa kazini
Wasichana wa shule
Workout au lifestyle ya active
Ushauri wa Kutunza Rasta:
Funga kichwa chako usiku kwa kitambaa cha silk au satin
Tumia mafuta ya ngozi ya kichwa angalau mara 3 kwa wiki
Epuka maji mengi kama rasta zako si synthetic water-friendly
Safisha scalp kwa njia ya kufuta na pamba safi au dry shampoo
Je, Unahitaji Rasta?
Rasta nyingi hizi hupatikana katika brand maarufu kama:
X-Pression
Nunaat
Angel na zingine nyingi
Picha za Misuko Ya Nywele Za Kisasa
….