Kuzungumza na mwanamke kwa mara ya kwanza kunaweza kuwa jambo la kusisimua lakini pia la kutia wasiwasi, hasa kama unamtamani au unataka kumvutia. Mafanikio ya mazungumzo hayo hutegemea sana aina ya maneno unayosema, sauti yako, na jinsi unavyojiamini.
Lengo kuu la mazungumzo ya kwanza si kumvutia kwa nguvu, bali kufungua mlango wa kujuana na kujenga hali ya kuaminiana na kuelewana.
Maneno ya Kusema Unapokutana na Mwanamke Mara ya Kwanza
1. Salamu ya Kawaida lakini yenye Haiba
Mfano: “Habari, samahani… naweza kuzungumza na wewe kwa dakika moja?”
Maneno haya huonyesha adabu na heshima, bila kulazimisha.
2. Pongezi (Compliment) ya Kistarabu
Mfano: “Nimevutiwa na tabasamu lako, linavutia sana.”
Epuka pongezi za kimwili kupita kiasi kama “figure yako ni kali” kwani zinaweza kumkera.
3. Swali Linalofungua Mazungumzo
Mfano: “Ulikuwa unasubiri rafiki, au uko tu kwenye mapumziko?”
Maswali haya hufungua mlango wa mazungumzo bila kumwekea presha.
4. Onyesha Maslahi kwa Yale Anayosema
Mfano: “Kweli? Unaipenda sana kazi yako? Inakufanya uhisi vipi?”
Wanawake hupenda mwanaume anayesikiliza na kuonyesha kuwa anajali anachosema.
5. Eleza Kidogo Kuhusu Wewe
Mfano: “Mimi naitwa ___, nafanya kazi ya ___. Nilikuona na nikahisi ni vizuri niseme ‘hi’.”
Kujiwasilisha kwa uhalisia hufungua mlango wa kuaminika zaidi.
Mambo ya Kuepuka Kusema Mara ya Kwanza
“Una mtu?” – Inaweka presha na kuonekana kama unamlenga moja kwa moja kwa mahusiano.
Maneno ya Kimahaba ya Haraka Sana – Mfano: “Wewe ni mrembo wa ndoto zangu.” (Too much, too soon!)
Kujiingiza kwa Mdomo Mrefu Sana – Mazungumzo ya upande mmoja hupoteza ladha.
Swali la Mapato/Mahusiano ya Kifamilia Haraka Sana – Haya ni mambo ya binafsi yanayohitaji muda kujadiliwa.
Soma Hii: SMS Ambazo Mwanamke Hapaswi Kumtumia Mwanaume
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Maneno Ya Kusema Unapozungumza Na Mwanamke Mara Ya Kwanza
1. Ni nini ninapaswa kusema ili nianze mazungumzo bila kumkera?
Salamu ya kawaida, pongezi ya staha au swali la kirafiki linaweza kuanzisha mazungumzo bila kukera.
2. Je, ni sawa kutoa pongezi kuhusu muonekano wake mara ya kwanza?
Ndiyo, lakini iwe ya kistaarabu. Mfano: “Una mtindo mzuri wa mavazi” ni bora kuliko “umetokelezea vibaya.”
3. Vipi kama naogopa au siwezi kupata maneno sahihi?
Ni kawaida kuhisi wasiwasi. Jipumzishe, zungumza kama vile unazungumza na rafiki mpya. Mazoezi husaidia.
4. Ni muda gani unapaswa kuchukua kwenye mazungumzo ya kwanza?
Usichukue muda mrefu hadi kumchosha. Ikiwezekana, acha mazungumzo yakiwa bado yana ladha – litamsisimua kutaka kukuona tena.
5. Je, napaswa kumuomba namba ya simu kwenye mazungumzo ya kwanza?
Ndiyo, kama mnaelewana vizuri na kuna “chemistry,” unaweza kumuomba kwa staha: “Ningependa kuendelea na mazungumzo haya siku nyingine, naweza kupata namba yako?”