Mapenzi si uchawi, lakini mara nyingine maneno sahihi kwa wakati sahihi yanaweza kuwa kama uchawi. Mwanamke anapenda mwanaume anayejua kusema maneno yanayogusa moyo, si kwa sababu anatafuta kupewa kitu, bali kwa sababu anathamini uwepo wake.
Lakini kumbuka: Maneno mazuri yasiyoendana na matendo ni kama maua kwenye kaburi – mazuri lakini hayana uhai.
Siri ya Maneno Yenye Kuvutia Mwanamke
Yawe ya kweli, si ya kutaka tu kumshawishi.
Yawe ya heshima – usivuke mipaka hata kama unamvutiwa sana.
Yaonyeshe kuwa unaona uzuri wake wa ndani, si mwonekano tu.
Yawe ya wakati muafaka – usimwagiwe maneno kama anajisikia vibaya.
Yaambatane na tabia zako – maneno yako yafanane na matendo yako.
Maneno ya Kwanza ya Kumvutia Mwanamke
Kabla ya kumwambia mwanamke kuwa unampenda, anza kwa maneno ya kumfanya ajisikie special:
“Umeshindaje kuwa mzuri hivi? Mimi sikuwa nimeamini kuwa mwanamke kama wewe angeshatokea maishani mwangu.”
“Kila ninakukutana, nafurahi kwa sababu unaweza kunifanya nikacheka hata kwa shida zangu zote.”
“Sio kila siku nakutana na mtu anayenifanya nione dunia kwa njia tofauti. Wewe ndio huyo mtu.”
Maneno ya Kumwambia Anavyokupendeza
Mwanamke yeyote hutaka kusikia kwamba unamwona na kumthmini. Hapa kwa hapa kuna baadhi ya maneno ya kumfanya ajisikie mwenye thamani:
“Pengine hujui, lakini sura yako hunifanya nisahau kila kitu kibaya kilichonipita.”
“Sio tu sura yako, bali roho yako pia ni nzuri. Hiyo ndio sababu sina budi kukumbuka kila siku.”
“Kama ningepewa nafasi ya kuchagua tena, ningekuchagua wewe mara mia.”
Maneno ya Kimapenzi ya Kumpa Rahisi Yake
Ikiwa unataka kumfanya mwanamke ajisikie salama na kwenye mapenzi, tumia maneno haya:
“Najua sio kila siku tunaweza kuwa pamoja, lakini najua pia kuwa moyo wako unanikumbuka.”
“Hata kama dunia itanikataa, najua wewe utanikumbuka.”
“Siku moja nitakuja na pesa, lakini kwa sasa nina wewe, na hiyo inanitosha.”
Maneno ya Kumshtua na Kumfanya Ajaribu Upendo Wako
Wakati mwingine, mwanamke anahitaji kushtushwa ili ajue kwamba unaweza kumchukua kwenye mawazo yake:
“Kama ningekuwa na uwezo wa kukupa dunia nzima, ningekufanyia hivyo. Lakini kwa sasa, napenda kukupa moyo wangu.”
“Unajua nini? Mimi sio mwanamume wa kawaida… Kwa sababu nimekupa moyo wangu wakati wengine wanataka tu mwili wako.”
“Nimekutafuta kwa miaka mingi bila kujua. Sasa nimekupata, sitakuruhusu kwenda.”
Maneno ya Kufungua Mzigo wa Mapenzi
Ikiwa unataka kumwomba mwanamke mzigo au kumfanya ajue kuwa unataka kuwa naye kwa maisha yote, sema:
“Sitaki kuwa na mwingine isipokuwa wewe. Je, unaweza kunipa nafasi ya kukupa maisha mema?”
“Nimechoka kuwa peke yangu. Nataka uwe mke wangu na tuanze familia pamoja.”
“Kama upendo ni kosa, basi nimekosea vibaya kwako… Lakini sitaki kutengwa nawe milele.”
Soma Hii :Sms za kumshawishi mwanamke akupende
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Maneno ya Kumvutia Mwanamke
Je, wanawake wote huvutiwa na maneno matamu?
Wengi wao wanapenda maneno mazuri, lakini kinachogusa ni ukweli wa nyuma ya maneno hayo. Usiseme ili upate kitu – sema ili ajue unamthamini.
Je, maneno ya mapenzi yanasaidia hata kama hatujawahi kukutana ana kwa ana?
Ndiyo, lakini kwa kiasi. Hakikisha yanalingana na hatua ya mawasiliano yenu. Usikimbilie “nakupenda” kama bado mpo hatua ya “habari yako.”
Ninapojaribu kusema maneno mazuri anakaa kimya – nifanye nini?
Anaweza kuwa haelewi nia yako bado, au anasita kuamini. Mpe muda. Pia hakikisha maneno yako hayamletei presha au aibu.
Naweza kutumia mistari ya mapenzi kutoka mitandaoni?
Unaweza kuhamasika nayo, lakini ibadilishe iwe ya kwako. Mwanamke anaweza kuhisi kama mistari hiyo ni ya kudesa.
Maneno ya moyoni hushinda mistari yoyote ya mitandaoni.
Ni wakati gani sahihi wa kusema maneno ya kumvutia?
Wakati yuko relaxed, mpo katika mazungumzo ya kawaida au hata baada ya kumtia moyo. Usivunje mazungumzo ya maana kwa “babe una macho ya kupotezea watu” – subiri tone la mazungumzo lifae.
Maneno Ya Kweli Hugusa Moyo Wake
Kumvutia mwanamke kwa maneno si mchezo wa maneno mazuri tu – ni juu ya kuonyesha uhalisia wako, kumpa heshima, na kumthamini bila presha. Maneno yako yakitamkwa kwa uaminifu na moyo wa upendo, yanaweza kumfungulia milango ya hisia polepole.
Unaposema:
“Nathamini uwepo wako,”
hakikisha hata matendo yako yanamwambia vivyo hivyo kila siku.