Katika kila uhusiano wa kimapenzi, kuna nyakati ambapo mmoja huhisi haja ya kulalamika au kueleza jambo lisilomfurahisha. Kulalamika siyo tatizo – jinsi unavyosema ndilo huamua kama mtatatua tatizo au kuanzisha ugomvi.
SEHEMU YA 1: KWA NINI KULALAMIKA NI MUHIMU KATIKA MAHUSIANO?
Malalamiko ni njia ya kuonyesha hisia zako unapohisi huzuni, kutosikilizwa au kutopewa kipaumbele. Badala ya kubeba manung’uniko moyoni, ni bora kusema – lakini kwa lugha itakayojenga, si kubomoa.
SEHEMU YA 2: MANENO YA KULALAMIKA KWA UPENDO (MFANO)
💔 Malalamiko kuhusu muda
“Naumia unapokuwa bize sana hadi hunipatii hata dakika chache za mazungumzo.”
“Sijui kama unanijali kama zamani, maana si kama awali tulivyokuwa tukiongea mara kwa mara.”
💔 Malalamiko kuhusu mabadiliko ya hisia
“Naona kama mapenzi yamepungua siku hizi, unanizungumzia kwa baridi tofauti na zamani.”
“Naumia kila nikiona mimi pekee ndiye ninayejitahidi kufanikisha uhusiano huu.”
💔 Malalamiko kuhusu kutotendewa haki
“Ningependa tufanye maamuzi pamoja, si kila mara ni wewe tu unaeamua kila kitu.”
“Si vizuri kuahidi vitu na kutotimiza. Inaniumiza kila mara napoamini halafu sivioni vitendo.”
💔 Malalamiko kuhusu kuumizwa kihisia
“Maneno yako yanauma. Najua hukusudia, lakini ningependa tuwe waangalifu zaidi.”
“Nilitegemea kuwa sehemu salama kwako, lakini lately naona nimekuwa mtu wa kulalamikiwa tu.”
💔 Malalamiko ya upweke au kutengwa
“Wakati mwingine najisikia kama vile mimi si kipaumbele tena kwako.”
“Ningependa unishirikishe zaidi katika maisha yako, si vizuri kujisikia kama mgeni.”
SEHEMU YA 3: JINSI YA KUTOA MALALAMIKO BILA UGOMVI
Anza kwa kusema unavyohisi, si kumshambulia
Badala ya: “Wewe huwa hunijali!”
Sema: “Ninajisikia kupuuzwa ninapokukosa bila mawasiliano.”
Tumia “mimi” badala ya “wewe”
Mfano: “Mimi huhisi huzuni nikikosa muda wa kutosha na wewe.”
Badala ya: “Wewe hutaki kutumia muda na mimi!”
Onyesha nia ya kujenga, si kulalamika tu
“Ningependa tuangalie namna ya kuboresha mawasiliano yetu. Unaweza kunisaidiaje hapo?”
Sikiliza na yeye pia
Baada ya kusema yako, mpe nafasi ya kusema upande wake. Malalamiko yenye mafanikio ni yale yanayokuwa na mazungumzo ya pande zote mbili.
SEHEMU YA 4: MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA (FAQs)
Ni wakati gani mzuri wa kulalamika kwa mpenzi?
Wakati mpo peke yenu, mmepoa kihisia na mko tayari kusikilizana. Epuka kulalamika katikati ya hasira kali.
Je, kulalamika kunaweza kuharibu uhusiano?
Siyo kulalamika ndiko kunaharibu, ni namna unavyolalamika. Ukilalamika kwa kuonyesha lawama na kejeli, ndivyo huleta matatizo. Lakini ukilalamika kwa upendo, huleta suluhisho.
Je, kila malalamiko lazima yajibiwe au kufanyiwa kazi?
Ikiwa ni malalamiko ya msingi na ya kweli, basi ndiyo. Uhusiano mzuri hujengwa kwa kusikilizana na kuheshimiana.