Kama Uliomba mkopo wa eimu ya juu na hukubahatika kuwa ni miongoni mwa waliopata mkopo weye aamu ya aali na aamu ya pili angalia Majina ya Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu HESLB 2025/2026 (Batch Three) Huenda ukawa ni miongoni mwa wanufaika katika awamu hii ya tatu.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu HESLB
Wanafunzi ambao walituma maombi ya mkopo wa elimu ya juu kupitia Dirisha la Tatu la maombi ya mkopo HESLB wanaweza kufuatilia majibu ya maombi ya mkopo HESLB kwa njia ya kupitia akaunti yao ya SIPA HESLB . Ili kuangalia kama umepata mkopo, fuata hatua hizi:
SOMA HII :Jinsi ya Kuangalia Status yako ya Mkopo HESLB 2025/2026
Fungua Tovuti ya HESLB: Tembelea tovuti rasmi ya HESLB au bonyeza moja kwa moja kwenye kiungo hiki https://olas.heslb.go.tz/olams/account/login.
Ingia kwenye Akaunti yako: Tumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilojisajili nalo wakati wa kuomba mkopo.
Mara Baada ya kuingia katika akaunti yako, Bofya Kitufe kilichoandikwa “SIPA” Kisho Bofya “ALLOCATION”

Chagua mwaka wa masomo. Baada ya kubofya “Allocation” Utapelekwa kwenye ukurasa mwengine ambapo unatakiwa kuchagua mwaka wa masomo (2024/2025) ili kuweza kuona kiasi cha mkopo ulicho pata.
Angalia Taarifa zako za Mkopo: Utaweza kuona kama umepewa mkopo na kiasi kilichopangiwa. Ni muhimu kufuatilia akaunti yako mara kwa mara ili kujua hali ya maombi yako. Mabadiliko yoyote yanayohusiana na mkopo yataonekana ndani ya akaunti yako ya SIPA.
Mwongozo kwa Wanafunzi Waliofanikiwa Kupata Mkopo
Kwa wanafunzi waliopangiwa mikopo, ni muhimu kufuata hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kwamba mikopo yao inatolewa kwa wakati na bila usumbufu. Baadhi ya hatua muhimu ni pamoja na:
- Kuhakikisha umekamilisha usajili wako chuoni.
- Kupeleka nakala za barua za mkopo na nyaraka nyingine zinazohitajika kwenye ofisi ya fedha ya chuo chako.
- Kuendelea kufuatilia akaunti yako ya mkopo kupitia mfumo wa mtandao wa HESLB.