Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili wa mahojiano (oral interview) kwa ajili ya nafasi mbalimbali za kazi. Taarifa hii imetolewa rasmi tarehe 25 April 2025 kupitia tovuti ya TRA na mitandao ya kijamii.
Je, Matokeo ya Usaili wa Kuandika TRA 2025 Yanatoka Lini?
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Moshi Kabengwe, matokeo ya usaili wa kuandika uliofanyika tarehe 29 na 30 Machi 2025 yanatarajiwa kutangazwa tarehe 25 Aprili 2025. Hii ni baada ya kuwasilishwa na mshauri elekezi tarehe 23 Aprili 2025.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Walioitwa Kwenye Oral Interview TRA 2025
Ili kuangalia majina ya walioitwa kwenye usaili wa mahojiano:
Tembelea tovuti rasmi ya TRA: www.tra.go.tz
Nenda kwenye sehemu ya “Matangazo” au “Habari” na tafuta tangazo lenye kichwa “Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili wa Mahojiano 2025”.
Pakua orodha ya majina katika mfumo wa PDF na tafuta jina lako kwa kutumia namba ya usajili au jina kamili.
Vitu au Nyaraka Muhimu za Kwenda Nazo Kwenye Usaili wa Mahojiano TRA
Waombaji walioitwa kwenye usaili wa mahojiano wanatakiwa kwenda na nyaraka zifuatazo:
Barua ya mwaliko wa usaili (Interview Invitation Letter).
Nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) au hati ya kusafiria.
Vyeti halisi vya elimu (Original Academic Certificates).
Cheti cha kuzaliwa (Birth Certificate).
Nakala ya vyeti vya taaluma au mafunzo maalum yanayohusiana na nafasi uliyotuma maombi.
Soma Hii : Taarifa Kwa Umma kuhusu Matokeo ya Usaili wa Kuandika Ajira za TRA
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili wa Mahojiano TRA 2025
1. Je, nitajulishwa vipi kama nimeitwa kwenye usaili wa mahojiano?
TRA hutuma taarifa kupitia barua pepe kwa waombaji waliochaguliwa na pia hutangaza majina kwenye tovuti yao rasmi.
2. Nifanye nini kama jina langu halipo kwenye orodha ya walioitwa?
Ikiwa jina lako halipo, inawezekana hukukidhi vigezo vya awali. Unaweza kuwasiliana na TRA kwa maelezo zaidi au kusubiri matangazo ya nafasi nyingine zijazo.
3. Je, kuna mafunzo au maandalizi maalum ya kufanya kabla ya usaili wa mahojiano?
Inashauriwa kufanya maandalizi ya kutosha kwa kupitia maswali ya usaili wa awali, kujifunza kuhusu majukumu ya nafasi uliyotuma maombi, na kuwa na uelewa wa jumla kuhusu TRA na majukumu yake.
4. Je, usaili wa mahojiano utafanyika wapi?
Mahali pa usaili hutajwa katika barua ya mwaliko. Ni muhimu kusoma kwa makini barua hiyo ili kujua tarehe, muda, na mahali pa usaili.
5. Je, kuna ada yoyote ya kushiriki katika usaili?
Hapana, usaili wa TRA hauna ada yoyote. Kuwa makini na matapeli wanaoweza kudai malipo kwa ahadi ya kukusaidia kupata kazi.