Kila mwaka Jeshi la Polisi Tanzania hutangaza ajira mpya kwa vijana waliohitimu masomo yao na wenye sifa zinazostahili. Mwaka 2025 haukuwa tofauti. Tangazo la majina ya walioitwa kwenye usaili wa Jeshi la Polisi limekuwa likisubiriwa kwa hamu na mamia ya waombaji kote nchini.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Walioitwa Kwenye Interview Jeshi la Polisi Tanzania 2025
Ili kuangalia majina ya walioitwa kwenye usaili wa Polisi, fuata hatua hizi:
Tembelea Tovuti Rasmi ya Jeshi la Polisi:
https://www.polisi.go.tzNenda kwenye sehemu ya Matangazo au Ajira
Kawaida tangazo huwekwa kama “Orodha ya Walioitwa Kwenye Usaili wa Polisi 2025”.Pakua PDF ya orodha ya majina
Mara nyingi hutolewa kwa muundo wa PDF kulingana na mikoa au kanda.Tafuta jina lako kwa kutumia namba ya mtihani au jina la mwisho.
Angalia Tarehe na Mahali pa kufanyia usaili.
Download Majina Katika PDF Hapa
Kumbuka: Usitumie vyanzo visivyo rasmi kama mitandao ya kijamii bila uthibitisho kutoka kwenye tovuti ya serikali au magazeti yenye weledi.
Vitu Muhimu vya Kwenda Navyo Kwenye Interview ya Jeshi la Polisi
Kabla ya kuelekea kwenye usaili, hakikisha umebeba nyaraka zifuatazo:
Barua ya Mwito wa Usaili (printed copy kutoka tovuti ya Polisi)
Cheti cha kuzaliwa au affidavit
Nakala halisi na fotokopi ya vyeti vya elimu (form IV/VI, diploma, degree n.k.)
Cheti cha matokeo (statement of results siyo rasmi)
Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA
Picha ndogo (passport size) – angalau 2
Vyeti vya afya kutoka hospitali ya serikali (kama vimeombwa)
Daftari na kalamu kwa ajili ya kuandika chochote kinachohitajika
Nyaraka nyingine yoyote iliyotajwa kwenye tangazo
Kumbuka kuvaa mavazi rasmi na nadhifu yanayoheshimu taasisi ya Jeshi.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)
1. Majina ya walioitwa kwenye usaili wa Polisi 2025 yametoka lini?
Majina hutangazwa mara baada ya mchujo wa maombi kukamilika, mara nyingi ndani ya wiki 2–4 baada ya mwisho wa kupokea maombi. Angalia mara kwa mara kwenye tovuti ya Polisi.
2. Je, kama sijakuta jina langu, ina maana sikuajiriwa?
Ndiyo. Ikiwa jina lako halipo kwenye orodha, ina maana haukupita kwenye mchujo wa awali. Unaweza kujaribu tena wakati ajira mpya zitakapotangazwa.
3. Usaili wa Jeshi la Polisi unahusisha nini?
Kuna vipengele vya usaili wa mdomo (oral interview), usaili wa maandishi, vipimo vya afya, na majaribio ya nguvu za mwili (physical fitness test).
4. Je, wanafunzi wa mwaka wa mwisho wanaruhusiwa kuomba?
Hapana. Waombaji wote wanapaswa kuwa wamemaliza masomo yao na kuwa na vyeti halisi.
5. Naweza kuomba bila kitambulisho cha NIDA?
Kwa sasa, NIDA ni moja ya vigezo muhimu vya utambulisho. Hakikisha umejisajili na kupata namba angalau.