Tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume limekuwa changamoto kwa wanaume wengi – vijana kwa wazee. Sababu kuu huwa ni msongo wa mawazo, lishe duni, uchovu wa mwili, matumizi ya pombe au sigara, pamoja na magonjwa ya mfumo wa damu au homoni.
Kwa bahati nzuri, kuna njia nyingi asilia zinazoweza kusaidia kurejesha nguvu za kiume na kuimarisha misuli ya uume – mojawapo ikiwa ni kupitia Juice ya asili.
Faida za Juice ya Kuimarisha Misuli ya Uume
Juice ya asili inaweza kusaidia kwa:
Kuongeza mzunguko wa damu kwenye uume
Kuimarisha misuli ya uume (corpora cavernosa)
Kuongeza stamina na nguvu wakati wa tendo
Kuboresha afya ya moyo (ambayo inaathiri moja kwa moja uwezo wa kusimamisha vizuri)
Kuchochea uzalishaji wa homoni ya testosterone
JUICE YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME – RECIPE YA ASILI
Viambato Muhimu:
Tangawizi mbichi – kipande kimoja kidogo
Ndizi mbivu (1) – kwa ajili ya nguvu na virutubisho
Parachichi (½) – huongeza mafuta mazuri kwa uzalishaji wa homoni
Asali mbichi (kijiko 1) – huchangamsha damu na kuongeza msisimko
Mdalasini (½ kijiko cha chai) – huongeza nguvu na kasi ya damu
Juisi ya limao (tone chache) – huongeza uwezo wa kusafisha mwili
Maji ya uvuguvugu/glasi ya maziwa ya moto – ya kuchanganyia
JINSI YA KUTENGENEZA:
Safisha viambato vyote vizuri.
Katakata tangawizi na parachichi vipande vidogo.
Tumbukiza viambato vyote kwenye blender – ndizi, parachichi, tangawizi, mdalasini, asali, na maji au maziwa.
Saga hadi mchanganyiko uwe laini.
Mimina kwenye glasi, kisha kunywa asubuhi kabla ya kifungua kinywa au saa 1 kabla ya tendo.
JUICE HII INAVYOFANYA KAZI
Tangawizi na mdalasini: Huchochea mzunguko wa damu, hasa kwenye sehemu za siri
Ndizi na parachichi: Hutoa nguvu, potasiamu, na mafuta mazuri kusaidia homoni za kiume
Asali: Hutoa nishati ya haraka na kuchochea mfumo wa fahamu
Juisi hii inasaidia kuimarisha misuli ya uume kwa kuongeza oksijeni na damu katika eneo hilo
MATUMIZI SAHIHI
Kunywa glasi moja kila siku kwa wiki 2 hadi 3
Epuka pombe, sigara, na vyakula vyenye mafuta mengi wakati unatumia
Fanya mazoezi ya mwili angalau mara 3 kwa wiki (kama squats, kegel exercises, na kutembea kwa miguu)
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA
Je, juice hii inafaa kwa wanaume wa umri wowote?
Ndiyo, inafaa kwa wanaume wa rika zote isipokuwa walio na matatizo ya kiafya maalum (mf. presha, kisukari – washauriwe kwanza na daktari).
Inachukua muda gani kuona mabadiliko?
Wanaume wengi huanza kuona tofauti ndani ya siku 3 hadi 7, hasa kwa matumizi ya kila siku na lishe bora.
Naweza kuchanganya juice hii na dawa za kuongeza nguvu?
Ikiwa ni dawa asilia, unaweza. Lakini kwa dawa za hospitali (kama Viagra), ni vyema kushauriana na daktari kwanza.