Sabuni ya mche, au sabuni ya kipande, ni moja ya bidhaa maarufu za usafi zinazotumika kila siku. Kutengeneza sabuni ya kipande nyumbani au kama biashara ni njia nzuri ya kuanzisha biashara yenye manufaa na kujenga bidhaa zenye ubora wa asili.
Viungo Muhimu vya Kutengeneza Sabuni ya Mche (Sabuni ya Kipande)
(I)CAUSTIC SODA
(II)MAFUTA YA NAZI,MISE,MBOSA AU MAWESE AU YA NYONYO
(III)MAJI
(IV)PAFYUM
(V)HYDROGEN PEROXIDE
(VI)CHUMVI KWAAJILI YA KUIFANYA SABUNI NZITO NA ISIISHE HARAKA
Vifaa Unavyohitaji Kutengeneza Sabuni ya Mche
Kutengeneza sabuni ya kipande kunaweza kuwa rahisi ikiwa utakuwa na vifaa sahihi. Hapa ni baadhi ya vifaa vya muhimu:
- Chombo cha chuma au kauri (kwa ajili ya kuchanganya viungo na lye)
- Chombo cha kutengeneza sabuni (Moldi) – inaweza kuwa moldi ya plastiki au chombo cha chuma kinachoweza kutoa umbo la kipande cha sabuni
- Glovu za kinga (kwa ajili ya usalama wakati wa kushughulika na lye, ambayo ni kemikali kali)
- Kijiko cha mchanganyiko (au mikono yako) kwa kuchanganya viungo
- Thermometer (kama inahitajika, ili kupima joto la lye na mafuta)
- Pamba au brashi kwa ajili ya kupamba sabuni na kuipa muundo wa kipekee
Soma Hii :Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga
Hatua za Kutengeneza
HATUA YA KWANZA;
Loweka caustic soda kilo tatu kwenye maji lita 9 na unapaswa kutumia chombo cha bati na sio cha plastic.Koroga kwa muda wa dakika 15 na acha kwa muda wa siku 5.
HATUA YA PILI;
Chagua aina ya mafuta mojawapo ambayo umeyapata na anza kuchanganya sasa.Changanya caustic soda1 na mafuta lita 1 na nusu.changanya na gryceline vijiko viwili vya chakula.pafyumu kijiko kimoja cha chai.chumvi kijiko kimoja cha chakula.koroga kwa pamoja na uweke kwenye umbo na sabuni itakuwa tayari