Kupendwa na kupuuziwa na mtu unayempenda ni jambo linaloumiza. Wakati mwingine, watu wanaokuwa katika mahusiano hujikuta kwenye hali ambayo mmoja kati yao anajisikia kupuuzwa au kutopewa kipaumbele. Kama unapitia hali hii, usiharakishe kutoa lawama au kukata tamaa. Badala yake, kuna njia sahihi za kutegea na kuvuta tena attention ya mpenzi wako bila kumlazimisha au kumchosha.
Njia 10 za Kuteka Attention ya Mpenzi Wako Ambaye Anakupuuza
1. Jipende Kwanza
Penda nafsi yako, jithamini, na uweke nguvu zako katika kujiboresha. Mtu anayekuona ukijithamini, huchukulia pia kuwa wa thamani.
2. Acha Kumfuatilia Kupita Kiasi
Ukimpigia, ukimtumia jumbe mara kwa mara bila majibu – unajidhalilisha. Jitengue kidogo, mpe nafasi ya kukumiss.
3. Fanya Mabadiliko Chanya
Badilisha mtindo wa maisha – vaa vizuri, jali afya yako, kuwa na furaha. Wakati mwingine mabadiliko huleta mvuto upya.
4. Shughulika na Maisha Yako
Jihusishe na kazi, masomo, au biashara zako. Ukiwa bize na malengo yako, unatuma ujumbe wa kwamba hauko tegemezi kihisia.
5. Ongea kwa Ustarabu
Kama mnapata muda wa mazungumzo, zungumza naye kuhusu jinsi unavyojisikia bila kumlaumu. Mfano: “Nimehisi tuko mbali sana siku hizi, na ningependa tuwe karibu kama zamani.”
6. Usiwe Mrahisi Kupatikana
Ukijibu kila muda, kuwa wa haraka kila wakati, na kubembeleza bila kusikia sauti yake, unampa hisia kwamba hauko na thamani ya kupiganiwa.
7. Onesha Furaha Bila Yeye
Post picha zako ukifurahia maisha, bila ya kumuelekezea moja kwa moja. Hii humfanya ajulie ndani kimya kimya.
8. Jifunze Kumpa Nini Anakohitaji
Pengine anahitaji utulivu, muda wake binafsi, au msaada wa kihisia. Jifunze mahitaji yake badala ya kumshinikiza.
9. Usiweke Hasira Hadharani
Kupost ujumbe wa mafumbo kwenye WhatsApp au mitandao ya kijamii hakumfanyi arudi – bali kunampa sababu ya kukupuuza zaidi.
10. Jiulize Kama Mahusiano Haya Yanastahili Kazi
Baada ya juhudi zako, kama bado anakudharau, ni wakati wa kufikiria kama uhusiano huo una afya na thamani ya kuendelea kuupigania.
Soma Hii : Hatua 20 Za Kufuata Unapomtongoza Mwanamke
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Jinsi ya Kuteka Attention ya Mpenzi Anayekupuuza
1. Nifanye nini kama mpenzi wangu hajibu jumbe zangu kwa siku kadhaa?
Usiendelee kumwandikia. Mpe nafasi, na kwa wakati sahihi, mweleze kwa staha jinsi unavyojisikia. Kama hali itaendelea, chukua hatua za kujilinda kihisia.
2. Je, ni sawa kumblock ili kumvuta arudi?
Hapana. Kublock kwa lengo la kumkomoa kunaweza kuharibu zaidi. Badala yake, tulia na chukua muda wako kimya kimya; wakati mwingine “kujitenga” huleta nguvu zaidi.
3. Mpenzi wangu anasema yuko bize, lakini hana muda hata wa kunitumia ujumbe mmoja. Inamaanisha nini?
Mtu akiwa na nia ya kweli, huweza kuchukua hata sekunde 10 kusema “tupo pamoja” au “nitakutafuta baadae”. Ukiona hali ni ya kupuuzwa mfululizo, kuna jambo zaidi ya “ubize”.
4. Je, kumpigia simu sana kunaweza kumrudisha?
Hapana. Mfuatiliaji mwingi huleta kero. Badala yake, tumia ukimya kwa busara. Ukimya una nguvu kubwa kuliko kelele zisizosikilizwa.
5. Kuna muda sahihi wa kuacha kupigania mahusiano?
Ndio. Kama juhudi zako zote hazirudishwi, hupati heshima wala kipaumbele, basi ni wakati wa kujiuliza: Je, unajipenda vya kutosha kujiokoa?