Kwa wanaume wengi, changamoto ya kurudia tendo la ndoa baada ya kufika kileleni ni jambo la kawaida. Baada ya mshindo wa kwanza, mwili huingia katika kipindi cha kupumzika kinachojulikana kama refractory period, ambapo inakuwa vigumu kwa mwanaume kuwa tayari tena kwa raundi ya pili. Hata hivyo, kuna njia kadhaa za asili na za kitabibu zinazoweza kusaidia kufupisha muda huu ili uweze kurudia bao la pili kwa haraka zaidi.
Mbinu Za Kurudia Bao La Pili Kwa Haraka
Kufanya Mazoezi Mara kwa Mara
Mazoezi ni njia bora ya kuongeza stamina na kuboresha mzunguko wa damu, mambo yanayochangia uwezo wa mwanaume kurudia tendo kwa haraka.
Mazoezi mazuri kwa nguvu za kiume:
Squats – Husaidia kuongeza mtiririko wa damu kwenye eneo la nyonga.
Kegel exercises – Husaidia kuimarisha misuli inayodhibiti mshindo.
Cardio (kukimbia, kuruka kamba, kuendesha baiskeli) – Huongeza stamina kwa ujumla.
Jinsi ya kufanya: Fanya mazoezi haya mara 3-4 kwa wiki kwa matokeo bora.
Kula Lishe Bora
Chakula unachokula kina athari kubwa kwenye uwezo wako wa kurudia bao la pili kwa haraka. Vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume ni pamoja na:
Parachichi – Lina mafuta mazuri yanayosaidia kuongeza nishati.
Karanga na mbegu za maboga – Zina zinki (zinc) ambayo husaidia uzalishaji wa testosterone.
Ndizi – Ina enzyme iitwayo bromelain inayoongeza stamina.
Samaki wenye mafuta (Tuna, Salmon, Mackerel) – Zina Omega-3 inayosaidia mzunguko wa damu.
Tangawizi na asali – Huongeza msukumo wa damu kwenye uume na kuongeza stamina.
Jinsi ya kutumia: Hakikisha unajumuisha vyakula hivi kwenye mlo wako wa kila siku.
Kupunguza Muda wa Refractory kwa Dawa Asili
Baada ya mshindo wa kwanza, mwili huingia katika kipindi cha kupumzika (refractory period), ambacho kinaweza kudumu kutoka dakika chache hadi saa kadhaa. Kuna dawa za asili zinazosaidia kufupisha muda huu, kama vile:
Maca root – Hii ni mimea inayojulikana kuongeza stamina na kupunguza muda wa kupumzika baada ya mshindo.
Mabuyu – Husaidia kuongeza nguvu na kuupa mwili nishati ya kurudia tendo kwa haraka.
Tangawizi – Huongeza mtiririko wa damu na kuongeza stamina.
Jinsi ya kutumia:
Changanya kijiko cha asali na juisi ya tangawizi, kunywa mara moja kwa siku.
Ongeza maca powder kwenye smoothie au maji.
Kupunguza Msongo wa Mawazo na Wasiwasi
Wasiwasi na msongo wa mawazo vinaweza kusababisha mwanaume kushindwa kurudia tendo haraka. Njia bora za kupunguza msongo wa mawazo ni pamoja na:
Kusikiliza muziki wa kupumzika
Kufanya meditation na mazoezi ya kupumua
Kufanya mazoezi mara kwa mara
Jinsi ya kufanya: Tafuta njia bora ya kupunguza msongo wa mawazo kila siku ili kuboresha uwezo wako wa kimapenzi.
Kupumzika vya Kutosha na Kulala Vizuri
Usingizi wa kutosha husaidia mwili wako kutengeneza homoni za testosterone ambazo ni muhimu kwa nguvu za kiume.
Vidokezo vya kuboresha usingizi:
Lala masaa 7-9 kwa usiku.
Epuka simu au TV saa moja kabla ya kulala.
Kunywa maziwa ya moto au chai ya chamomile kabla ya kulala.
Kunywa Maji ya Kutosha
Mwili unahitaji maji ya kutosha ili kuweka mzunguko wa damu katika hali bora na kuhakikisha mwili unafanya kazi vizuri.
Jinsi ya kufanya: Kunywa angalau glasi 6-8 za maji kwa siku.
Soma Hii :Tiba YA ASILI ya kuchelewa kufika KILELENI
Kutumia Mbinu Sahihi Wakati wa Tendo la Ndoa
Njia unayotumia wakati wa tendo la ndoa inaweza kusaidia kuongeza muda wako na kukufanya uwe tayari kwa raundi ya pili haraka.
Kubadilisha mikao ya tendo – Jaribu mikao tofauti ambayo inapunguza msisimko wa haraka.
Kufanya mapenzi kwa utaratibu – Epuka kuharakisha mwendo ili kuzuia uchovu wa mapema.
Kucheza na mwili wa mpenzi wako kabla ya kuanza raundi ya pili – Badala ya kungoja hadi uume usimame, endelea kumshika na kumnyegesha mpenzi wako ili kurejesha msisimko.
Kutumia Virutubisho vya Asili
Baadhi ya virutubisho vya asili vinaweza kusaidia kuongeza stamina na kupunguza muda wa refractory period, kama vile:
Ginseng – Husaidia kuongeza nishati na kuamsha mwili kwa haraka.
L-arginine – Amino acid inayosaidia kuongeza mtiririko wa damu kwenye uume.
Zinc supplements – Husaidia uzalishaji wa testosterone.
Jinsi ya kutumia: Chukua virutubisho hivi chini ya ushauri wa daktari.
Kutumia Njia ya “Start-Stop”
Hii ni mbinu inayohusisha kusimamisha msuguano kwa muda mfupi unapohisi unakaribia kufika kileleni, kisha kuendelea baada ya msisimko kushuka. Hii husaidia kupunguza uchovu na kuweka mwili katika hali nzuri ya kuendelea na raundi nyingine haraka zaidi.
Jinsi ya kufanya:
Unapokaribia kufika kileleni, simama kwa sekunde 10-30 kisha uendelee.
Rudia mara kadhaa hadi utakapohisi umejizuia vya kutosha.