Jinsi ya Kupika Keki ya Happy Birthday (Recipe Kamili Hatua kwa Hatua)

Jinsi ya kupika keki ya happy birthday
Jinsi ya kupika keki ya happy birthday

Kutengeneza keki ya Happy Birthday nyumbani ni moja ya njia nzuri zaidi za kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa ubunifu na mapenzi. Keki hii huwa na muundo laini, rangi nzuri na icing tamu inayovutia macho. Hapa chini nimekuweka hatua kamili kuanzia mahitaji hadi upakuaji wa icing ili kupata keki maridhawa kama zile za bakery.

Mahitaji Ya Kupika Keki Ya Happy Birthday

Viambato vya Keki

  • Unga wa ngano – vikombe 2

  • Sukari – kikombe 1

  • Siagi laini – gramu 150

  • Mayai – 4

  • Baking powder – kijiko 1

  • Vanilla flavor – kijiko 1 cha chai

  • Maziwa – nusu kikombe

  • Rangi ya chakula (hiari)

Kwa Ajili ya Cream/Icing

  • Blueband/Butter – gramu 200

  • Sukari ya unga – vikombe 3

  • Vanilla flavor – kijiko 1 cha chai

  • Rangi za icing (kulingana na mapambo unayotaka)

Vifaa Vinavyohitajika

  • Oven au jiko la gesi lenye sehemu ya kuoka

  • Mixing bowl

  • Electric mixer au whisk ya mkono

  • Kopo la kuokea keki (round tin au square)

  • Parchment paper

  • Piping bags kwa ajili ya kupamba

Jinsi ya Kupika Keki ya Happy Birthday – Hatua kwa Hatua

1. Andaa Oven

Washa oven kwa 180°C ili upate joto la wastani linalofaa kuoka keki.

2. Andaa Kopo la Keki

Paka siagi sehemu za ndani za kopo, kisha tandaza parchment paper ili keki isishike chini.

3. Changanya Siagi na Sukari

Weka siagi kwenye bakuli, ongeza sukari kisha koroga hadi iwe nyepesi na laini.

4. Ongeza Mayai

Pasua mayai manne moja baada ya jingine huku ukikoroga ili yapangike vizuri kwenye mchanganyiko.

5. Ongeza Vanilla

Weka vanilla flavor kwa ajili ya harufu na ladha nzuri.

SOMA HII :  Jinsi ya Kupika Keki Kwenye Jiko la Mkaa (Hatua kwa Hatua Bila Oven)

6. Changanya Unga na Baking Powder

Katika bakuli lingine changanya unga na baking powder, kisha uanze kuongeza taratibu kwenye mchanganyiko wa siagi.

7. Weka Maziwa

Ongeza maziwa hatua kwa hatua ili kupata mchanganyiko laini usio mgumu wala mwembamba.

8. Ongeza Rangi (Hiari)

Ikiwa unataka keki yenye rangi ya birthday kama pink, blue au yellow, ongeza tone chache za food color.

9. Mimina Kopo la Kuokea

Mimina mchanganyiko kwenye kopo na ulevelishe juu kwa kutumia kijiko.

10. Oka

Weka kopo kwenye oven kisha oka kwa dakika 35–45.

11. Hakikisha Imeiva

Choma toothpick katikati ya keki. Ikiwa inatoka bila unga, keki imeiva.

12. Poa

Toa keki kwenye oven, iache ipoe kabisa kabla ya kupamba.

Jinsi Ya Kutengeneza Cream Icing

  1. Changanya butter au blueband hadi iwe laini.

  2. Ongeza sukari ya unga taratibu.

  3. Ongeza vanilla flavor.

  4. Gawa icing sehemu mbalimbali kama unataka rangi tofauti.

  5. Tumia piping bag kupamba juu ya keki.

  6. Andika “Happy Birthday” kwa icing yenye rangi tofauti.

About Burhoney 4806 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati