Namba ya NIDA (National Identification Number) ni kitambulisho muhimu kwa raia wa Tanzania. Inahitajika kwa shughuli mbalimbali kama kufungua akaunti ya benki, kupata leseni ya udereva, usajili wa laini ya simu, na hata kuomba ajira. Ikiwa unahitaji kupata namba yako ya NIDA haraka, kuna hatua unazoweza kuchukua ili kurahisisha mchakato huu.
Umuhimu wa Namba ya NIDA au NIN
Namba ya NIDA ni muhimu kwa sababu:
- Inakutambulisha rasmi kama raia wa Tanzania.
- Inahitajika kwa huduma za serikali na sekta binafsi.
- Ni sharti la usajili wa laini za simu na huduma za kifedha.
- Inahitajika kwa ajira na shughuli zingine za kiuchumi.
Njia za Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka
Kupata Namba ya NIDA kwa Kutumia Simu ya Mkononi
Kwa sasa, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imerahisisha mchakato wa kupata Namba ya Kitambulisho cha Taifa kupitia simu ya mkononi. Hii inamaanisha kuwa huna haja ya kutembelea ofisi za NIDA mara kwa mara; badala yake, unaweza kufuata hatua chache kupitia simu yako na kupata Namba yako ya NIDA papo hapo. Ifuate hatua hizi:
- Piga *152*00#: Kwa kutumia simu yako ya mkononi, piga namba hii ili kuanza mchakato wa kupata Namba ya NIDA.
- Chagua Namba 3 (Ajira na Utambuzi): Baada ya kupiga namba hiyo, utaletewa menyu ambapo utachagua namba 3 ambayo inahusisha huduma za Ajira na Utambuzi.
- Chagua Namba 2 (NIDA): Kwenye menyu inayofuata, chagua namba 2 kwa ajili ya huduma zinazotolewa na NIDA.
- Ingiza Majina Yako Matatu: Andika majina yako matatu kama yalivyo kwenye fomu yako ya usajili wa NIDA. Mfano: Dan John Sele.
- Ingiza Namba ya Simu: Andika namba ya simu uliyotumia wakati wa kujisajili na NIDA, mfano: 07XXXXXXX.
- Thibitisha Taarifa Zako: Hakikisha taarifa zote ulizojaza ni sahihi kisha thibitisha kwa kubonyeza “Kubali”.
Huduma hii inapatikana kwa watumiaji wa mitandao ya simu ya Airtel na Vodacom.
Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka Mtandaoni
Kuangalia namba ya NIDA mtandaoni ni njia rahisi na ya haraka ya kuhakikisha unapata namba yako bila kuhitaji kwenda ofisi za NIDA. Pia, inakupa uhakika wa kuwa na namba yako popote ulipo, kwa kutumia tu kifaa chako cha kielektroniki kama simu au kompyuta.
Ili kukagua namba yako ya NIDA mtandaoni, unahitaji kuwa na taarifa zifuatazo:
- Jina Kamili: Hakikisha unajua jina lako la kwanza na la mwisho kama lilivyo kwenye nyaraka zako za usajili.
- Tarehe ya Kuzaliwa: Tumia muundo wa tarehe (DD-MM-YYYY).
- Majina ya Mama: Ingiza jina la kwanza na la mwisho la mama yako kama lilivyoandikwa kwenye nyaraka zako za usajili.
- Muunganisho wa Mtandao: Unahitaji kuwa na muunganisho thabiti wa intaneti ili kufanikisha mchakato huu.
Fuata hatua hizi chini ili kuangalia namba yako ya NIDA mtandaoni:
- Fungua Tovuti Rasmi ya NIDA; Kwa kutumia kivinjari chako cha intaneti, fungua tovuti rasmi ya NIDA kupitia kiungo hiki: NIDA.
- Tafuta Fomu ya “Fahamu Namba Yako (NIN)“; Baada ya kufungua tovuti ya NIDA, tafuta sehemu inayosema “Fahamu Namba Yako (NIN)” kwenye upande wa kushoto wa tovuti. Sehemu hii itakupeleka kwenye fomu ambayo unahitaji kujaza taarifa zako.
- Jaza Taarifa za Usajili; Kwenye fomu hiyo, jaza taarifa zako kama zinavyoonekana kwenye nyaraka zako za usajili: Hapa utatakiwa kujaza , Jina la Kwanza, Jina la Mwisho, Tarehe ya Kuzaliwa, Jina la Kwanza la Mama na Jina la Mwisho la Mama
- Thibitisha Uhalisia Wako; Kwa usalama, utatakiwa kuingiza namba za usalama au maneno unayoona kwenye picha ili kuthibitisha kuwa wewe ni binadamu na si roboti. Kisha bonyeza kitufe cha “TUMA” ili kutuma taarifa zako.
- Pata Namba Yako ya NIDA: Endapo umejaza taarifa zote kwa usahihi, namba yako ya NIDA itaonekana kwenye skrini. Hakikisha unaandika au kuhifadhi namba hii mahali salama kwa matumizi ya baadaye.
Njia Mbadala za Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka
Kwa wale ambao wanataka kujua kama namba yao ya NIDA imeshatoka au wanakumbana na changamoto katika kupata namba kwa njia ya simu, kuna njia mbadala unazoweza kutumia:
Piga Simu kwa Kituo cha Huduma – Unaweza kupiga simu moja kwa moja kwenye kituo cha huduma kwa wateja cha NIDA. Nambari za kituo cha huduma ni:
- 0752 000 058
- 0687 088 888
- 0777 740 006
- 0677 146 666
Tembelea Ofisi za NIDA – Kwa wale ambao wanapendelea kufuatilia taarifa zao kwa njia ya ana kwa ana, unashauriwa kutembelea ofisi za usajili za NIDA zilizoko karibu na wewe.
Kupata namba ya NIDA ni muhimu kwa kila raia wa Tanzania kwa kuwa kitambulisho hiki kinatumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali na binafsi. Kwa kutumia njia zilizotajwa hapo juu, unaweza kupata namba yako ya NIDA kwa haraka na urahisi zaidi. Kama unakutana na changamoto yoyote, usisite kuwasiliana na NIDA kupitia nambari za simu au tovuti yao rasmi.
Kwa Mawasiliano Zaidi:
- Simu: 0759 102010, 0765 201020, 0673 333444, 0800758888
- Barua Pepe: nida.tanzania@nida.go.tz
- Tovuti: nida.go.tz