Kupenda au kuvutiwa na mwanamke aliyekuzidi umri si jambo geni. Kwa wengi, wanawake wakubwa wanavutia kwa sababu ya ukomavu wao, uzoefu wa maisha, na uelewa wa mahusiano. Ikiwa unataka kumvutia na kumshawishi mwanamke mkubwa kuliko wewe (maarufu kama ‘mshangazi’ kwa muktadha wa mtaani), unapaswa kutumia mbinu za kipekee zinazojikita kwenye heshima, ukomavu, na uelewa wa kihisia.
Njia rahisi ya kumtongoza mwanamke aliekuzidi umri
Thamini kile ambacho anakupatia
Kama unataka kujua jinsi ya kutongoza wanawake wakubwa kiumri, basi unapaswa uthamini kile ambacho anacho. Kwa lugha nyingine ni kuwa unapaswa kusimamisha fikra zako za kuangalia miaka yake au mikunjano ya uso wake, na uanze kufikiria mambo ambayo anaweza kugawa na wewe ikiwemo mapenzi. Wanaume wengi hudhania kuwa wanawake wadogo ndio huwa na ujuzi ikija na maswala ya mapenzi lakini huwa si ukweli.
Muonyeshe heshima
Wakati unapojifundisha jinsi ya kumtongoza mwanamke mkubwa, weka kwa akili yako kuwa atataka kupewa heshima zake zaidi ya vile wanawake wadogo utakavyowapatia. Hii ni kwa sababu ana experience ya juu zaidi ya maisha. Na kwa sababu ambazo zitategemeana na yeye, mwanamke aina hii anaweza kuwa asiwe huru kufunguka na kukueleza maisha yake ya zamani ama kukufungukia kuhusu maisha yake.
Muonyeshe kuwa wewe ni classy, mjanja na usiyesomeka
Kama unataka kujua jinsi ya kuwatongoza wanawake wakubwa waliokupita umri, basi ni jambo la muhimu kabisa kuhakikisha kuwa unakuwa mjanja na kuwa na tabia za kukomaa. Wanawake wakubwa tayari wanaexprerience ya kuwa na deti ambazo zilikuwa mbaya awali, so kama unataka kumshawishi mwanamke ambaye ni mkubwa wako kiumri vizuri, basi utahitajika kupandisha gemu yako iwe ya juu.
Kimsingi, wanawake wakubwa hawatakuwa interested na wanaume wenye nyege ambao wanashindwa kumaintain gumzo la kawaida mara kwa mara.
Usijionyeshe
Kuonyesha vitu unavyomiliki ama kuonyesha ujuba wako hakutakusaidia kutongoza wanawake waliokupita umri. Siku hizi wanawake wanapenda kupata nafasi ya kuonekana kuwa wana madaraka flani, so mwanamke atapoteza interest na wewe haraka sana kama utaanza kujidai na kuringa kuhusu idadi ya wanawake ambao umefanya nao mapenzi ama idadi ya magari unayomiliki. Kama umevalia suti ya kushonesha ama una Mercedes ya gharama si lazima umwambie kuvihusu kwani atajionea yeye mwenyewe. Badala yake msifu na kumpongeza kwa mambo aliyofanikiwa kufanya. Hii ni njia rahisi ya kuweza kuwatongoza wanawake waliokupita kiumri na wakakukubali kirahisi.
Jiamini
Njia nyingine rahisi ya kutongoza mwanamke aliyekupita umri ni kwa kuonyesha kuwa unajiamini kwa kila kitu unafanya au kuzungumza. Wanawake aina hii huwa kwa kawaida wanapenda wanaume ambao wanauwezo wa kutatua tatizo lolote ambalo watarushiwa usoni mwao. So, kama wewe ni mwanaume ambaye hujafikia kiwango cha kujiamini , basi ni wakati wako wa kuchukua hatua ya kuhakikisha ya kuwa unajenga ujiaminifu wa kuweza kuongea na wanawake.
Yaweke mapenzi yawe ya hali ya juu
Kama unataka kumshawishi mwanamke aliyekushinda kimiaka vizuri, unafaa kuhakikisha kuwa unaweka mapenzi yawe juu. Hii inamaanisha kuwa, ijapokuwa hatakuwa na tabia za kama wanawake walio wadogo, unapaswa humchukulia kama mwanamke mdogo. Mnunulie chokoleti, maua na zawadi ndogo ndogo mara moja au nyingine. Msifu wakati amevalia nguo nzuri ama anapopendeza mnapotoka out. Mambo haya madogo madogo ambayo unamsifia mwanamke yatamfanya mwanamke kuwa na furaha na atapendezwa na wewe.
Soma Hii :Connection za Bongo telegram group Links
Usitaje kuhusu utofauti wa miaka yenu
Na lile jambo muhimu la kuzingatia wakati wa kujifunza kutongoza wanawake waliokupita umri ni: kutotaja tofauti ya miaka yenu. Hata kama haujiskii huru na kuwa na yeye mara ya kwanza, hupaswi kuzungumzia swala hili. Ama unaweza kuharibu nafasi yako ya kumtongoza. Badala yake makinika na mambo ambayo yanahusiana nyote wawili, kama vile kuongea kuhusu mambo mnayopenda au kuongea kuhusu filamu.
Kuwa na Ukomavu wa Kutosha
Wanawake wakubwa wanapendelea wanaume wenye ukomavu wa kimawazo. Kuwa na malengo maishani, kuonyesha uwajibikaji, na kuwa na mazungumzo yenye maana kutakufanya uonekane kama mtu anayejua anachotaka maishani. Epuka tabia za kitoto au mchezo usio na mpango.
Fanya Vitendo Vinavyoonyesha Uanaume Wako
Wanawake wakubwa wanapenda wanaume wanaojua wajibu wao na wenye uwezo wa kujitegemea. Kuwa mtu anayechukua hatua na si wa kuzungumza tu. Hakikisha unajitahidi kuwa na mipango thabiti maishani mwako na unajali maendeleo yako.
Kuwa Muaminifu na Asiye na Nia ya Kifedha
Wanaume wadogo mara nyingi huonekana kuwa wanawatafuta wanawake wakubwa kwa ajili ya maslahi ya kifedha. Kama kweli unataka uhusiano wa dhati, thibitisha kuwa unamfuata kwa sababu ya hisia zako za kweli na si kwa sababu ya manufaa ya pesa.
Jali Muonekano Wako
Wanawake wakubwa wanapenda wanaume wanaojitunza. Hakikisha unavaa vizuri, una harufu nzuri, na unaonekana nadhifu kila wakati. Muonekano wa kuvutia unaongeza mvuto wa mwanamume kwa mwanamke yeyote, bila kujali umri.
Kuwa Na Subira na Usilazimishe Mambo
Mahusiano haya yanaweza kuwa magumu kwa sababu ya mtazamo wa jamii na fikra za mwanamke mwenyewe kuhusu tofauti ya umri. Kama anahisi wasiwasi, mpe muda na usimlazimishe. Kuwa mvumilivu na mwonyeshe kuwa unamheshimu na uko tayari kuwa naye kwa njia sahihi.