Huduma ya kukopa salio inaruhusu wateja wa Vodacom kukopa salio la simu linaloweza kutumika kwa mawasiliano au internet, kisha kulipa baadae unapojaza fedha kwenye akaunti yako. Hii ni huduma ya kipekee ambayo inarahisisha mawasiliano, hasa wakati unapohitaji kufanya mawasiliano ya dharura lakini huna salio.
Vigezo na Sifa za Kutumia Huduma ya Vodacom Nipige Tafu?
Ili mteja aweze kunufaika na huduma ya Nipige Tafu kutoka Vodacom, kuna vigezo vichache vinavyotakiwa kuzingatiwa:
Usajili wa Alama za Vidole (Biometric Registration)
Namba ya simu ya mteja lazima iwe imesajiliwa kwa alama za vidole ili aweze kupata huduma hii. Usajili huu ni muhimu kwa sababu za kiusalama na kuhakikisha kuwa mteja ndiye anayeomba na kutumia mkopo.
Muda wa Matumizi ya Laini
Vodacom huzingatia muda ambao mteja amekuwa akitumia laini yake. Kadiri mteja anavyotumia laini yake kwa muda mrefu na kwa uaminifu, ndivyo anavyoongeza uwezekano wa kupata mkopo wa kiasi kikubwa zaidi.
Matumizi ya Muda wa Maongezi na Vifurushi
Vodacom pia huangalia historia ya matumizi ya muda wa maongezi na vifurushi vya intaneti ya mteja. Matumizi ya mara kwa mara na ya kutosha huongeza uwezekano wa mteja kupata mkopo.
SOMA HII: Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
Malipo ya Madeni ya Awali
Ikiwa mteja amewahi kukopa kupitia Nipige Tafu hapo awali, ni muhimu kulipa deni hilo kwa wakati ili kuongeza uaminifu wake na uwezo wa kukopa tena siku zijazo.
Jinsi Ya Kukopa Salio Nipige Tafu Vodacom (Menu Ya Kukopa Salio Vodacom)
Kukopa Salio Nipige Tafu Vodacom kupitia huduma ya Nipige Tafu ni rahisi na haraka. Fuata hatua hizi rahisi:
Ingia kwenye menu ya kukopa Salio Vodacom ambayo ni *149*01*99#. Hii ndio menu maalum ya kufikia huduma ya Nipige Tafu.
Chagua Kiasi Unachohitaji: Baada ya kupiga menu ya kukopa salio Vodacom, utaona orodha ya chaguzi mbalimbali ikiwemo “Nipigetafu”. Chaguo hili litakuonyesha kiasi cha mkopo unachostahili kupata kulingana na matumizi yako ya awali na vigezo vingine. Chagua kiasi kinachokidhi mahitaji yako ya sasa.
Thibitisha Ombi Lako: Baada ya kuchagua kiasi, thibitisha ombi lako la mkopo. Kumbuka kuwa Vodacom itakata kiasi ulichokopa pamoja na ada ndogo ya huduma kutoka kwenye salio lako utakapojaza tena muda wa maongezi. Hakikisha umeelewa ada husika katika eneo lako.
Pia unaweza kujua kiwango chako cha kukopa au deni lako la huduma ya Vodaco Nipige Tafu bila kuwasiliana na huduma kwa wateja. Kuangalia deni lako la Nipige tafu tafadhali fuata maelekezo yafuatayo;
1. Piga *149*01#
2. Chagua Nipige Tafu
3. Chagua salio la mkopo au kiwango cha mkopo.
Kumbuka: Hakikisha unalipa deni lako kwa wakati ili kiepuka usumbufu wa kukosa huduma hii.