JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Fahamu Jinsi ya kujiunga na NBC kiganjani App Ili kukurahisishia Maisha yako ya Kibenki ,Kupitia  NBC Kiganjani App utaweza kupata huduma kuitumia kuhamisha fedha, kununua Umeme na kuongeza wanufaika kwenye akaunti yako.

Jinsi ya Kujiunga na NBC Kiganjani

NBC Kiganjani inakupa uwezo wa kufanya miamala ya kibenki popote ulipo kwa kutumia simu yako. Ili kujiunga na huduma hii, fuata hatua zifuatazo:

  1. Tembelea Tawi la NBC: Kwanza, tembelea tawi lolote la NBC lililo karibu nawe. Utahitaji kujaza fomu ya maombi ya kujiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu. Kujisajili ni bure.
  2. Jaza Fomu ya Maombi: Jaza fomu ya maombi ya huduma za NBC Kiganjani. Fomu hii inapatikana pia mtandaoni kupitia NBC Mobile Banking.
  3. Pokea Ujumbe wa Uthibitisho: Baada ya usajili kukamilika, utapokea ujumbe wa uthibitisho kwenye simu yako ya mkononi. Ujumbe huu utaeleza kuwa huduma yako ya NBC Kiganjani imewezeshwa.
  4. Jinsi ya kuongeza mnufaika NBC Kiganjani

    1. Fungua App ya NBC Kiganjani kwenye kifaa chako
    2. Ingia
    3. Chagua ”Huduma Nyingine” chini kulia kwenye screen yako
    4. Chagua Wanufaika
    5. Chagua Ongeza Mnufaika mpya
    6. Chagua Nunua Muda wa Maongezi
    7. Ingiza Jina la Mnufaika
    8. Chagua Operator wa Mtandao (Zantel, Vodacom, Airtel, Halotel, TTCL iliyolipwa kabla, Tigo)
    9. Ingiza namba ya Simu ya mpokeaji
    10. Hakiki na Hifadhi Mnufaika
    11. Mteja atapokea OTP kupitia SMS
    12. Weka namba za siri zilizotumwa kupitia SMS
    13. Jinsi ya kununua umeme

      1. Fungua App ya NBC Kiganjani kwenye kifaa chako
      2. Ingia
      3. Chagua ikoni ya Lipa bili
      4. Chagua kampuni iliohifadhiwa
      5. Chagua Akaunti ya Kutolea na Ingiza Kiasi
      6. Bonyeza Endelea
      7. Hakiki Bili na Uthibitishe Malipo
      8. Screen ya Uthibitisho
      9. Pokea tokeni kupitia SMSScreen ya UthibitishoAnza Kutumia Huduma: Piga *150*55# kwenye simu yako ya mkononi na fuata maelekezo rahisi ili kuanza kutumia huduma za NBC Kiganjani.

        Jinsi ya kuhamisha fedha

        1. Fungua App ya NBC Kiganjani kwenye kifaa chako
        2. Ingia
        3. Chagua ikoni ya ‘Uhamisho’ chini ya screen
        4. Chagua Akaunti ya ndani ya NBC
        5. Chagua Mnufaika
        6. Chagua Akaunti ya kuhamisha fedha kutoka
        7. Chagua Sarafu
        8. Ingiza Kiasi
        9. Ingiza Kumbukumbu
        10. Bonyeza Endelea
        11. Thibitisha Uhamisho
        12. Screen ya Uthibitisho

        Soma Hii :Aina za Mikopo ya Benki ya NBC Riba na Makato yake

        Usalama wa Huduma

        Usalama umehakikishwa kwenye huduma za NBC Kiganjani. Kila muamala unahitaji Namba yako ya Siri, na ni muhimu kuhakikisha unatunza kwa usiri mkubwa namba hii ili kuepuka miamala isiyo halali.

        Kwa maelezo zaidi au msaada, unaweza kuwasiliana na NBC kupitia namba za huduma kwa wateja: +255 76 898 4000, +255 22 219 3000, au 0800711177 (bila malipo).

        Pia, unaweza kutuma barua pepe kupitia huduma ya wateja.Huduma ya NBC Kiganjani inakupa urahisi wa kufanya miamala ya kibenki kwa haraka na salama, popote ulipo.

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Share.

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Leave A Reply