Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » Jinsi Ya kujisajili NIDA online
Makala

Jinsi Ya kujisajili NIDA online

Jinsi Ya kujisajili nida online, pamoja na Kujaza form ya NIDA online haya makala yatajumuisha kila kitu unachopaswa kujua kuhusu usajili wa nida mtandaoni Kitambulisho cha taifa NIDA.
BurhoneyBy BurhoneyMarch 22, 2025No Comments8 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
Jinsi Ya kujisajili NIDA online
Jinsi Ya kujisajili NIDA online
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

NIDA (National Identification Authority) ni taasisi inayohusika na usajili wa vitambulisho vya taifa nchini Tanzania. Sasa, unaweza kujisajili kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa kupitia mtandao kwa urahisi zaidi.

Mahitaji Muhimu Kabla ya Kujiandikisha au Kufanya usajili mtandaoni

Kabla ya kuanza mchakato wa kujiandikisha mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA, ni muhimu kuhakikisha unaviandaa na kuvichunguza vyema vielelezo vyote vinavyohitajika. Hapa kuna orodha ya mahitaji muhimu ambayo kila mwombaji anapaswa kuwa navyo kabla ya kuanza mchakato wa usajili:

  1. Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji
  2. Nakala ya cheti cha kuzaliwa / kiapo cha mzazi mmoja.
  3. Kama uraia wa mwombaji ni wakurithi: thibitisha kwa nakala ya cheti cha kuzaliwa au nakala ya kitambulisho cha Taifa cha mzazi mmoja.
  4. Kama uraia wa mwombaji ni wa kujiandikisha, thibitisha kwa nakala ya uraia wa kujiandikisha (Dossier Number) ya mwombaji.

Kwa kuhakikisha unakuwa na nyaraka hizi kabla ya kuanza mchakato wa kujiandikisha, utaweza kufanya mchakato huu kwa urahisi na kwa ufanisi zaidi. Hii itasaidia kuepusha ucheleweshaji wowote katika kupata kitambulisho chako cha taifa kutoka NIDA.

 Mambo Muhimu ya Kuingia Wakati wa Ujazaji Fomu

Wakati wa mchakato wa kujiandikisha mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA, kuna mambo kadhaa muhimu ambayo kila mwombaji anapaswa kuzingatia ili kuhakikisha usajili unakamilika kwa urahisi na ufanisi. Hapa chini ni masuala ya msingi ambayo yanapaswa kufuatiliwa

  1. Mwombaji anatakiwa kuwa na anuani ya barua pepe ambayo ataitumia kujisajili na kupokea kiunga kitakachomuwezesha kukamilisha usajili wake.
  2. Mwombaji anatakiwa kuwa na nyaraka zisizopungua mbili zitakazotumika kuthibitisha utambulisho wake. Mfano wa nyaraka hizo ni; Cheti cha kuzaliwa n.k.
  3. Mwombaji anatakiwa kufanya “scanning” ya nyaraka zake na kuziweka katika muundo wa PDF (usiozidi kurasa moja kwa kila kiambatisho) au picha katika muundo wa JPG au PNG.
  4. Ni muhimu Mwombaji kujaza Namba yake ya simu ya mkononi.
  5. Mwombaji anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa endapo amezaliwa Mwaka 1980 na kuendelea. Aidha, endapo Mwombaji amezaliwa kabla ya mwaka 1980 anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa au “Affidavit”.
  6. Kwa Waombaji wenye majina mengine; ni vyema kuandika majina hayo ili endapo ikatokea uhitaji wa kurekebisha majina yake iwe rahisi kutambulika.
  7. Mwombaji anatakiwa kufahamu majina ya Baba na Mama yake mzazi.
  8. Mwombaji ambaye ana Namba za Utambulisho (NIN) za wazazi wake; anatakiwa kuweka viambata halisi (kwa wazazi waliokwishapata vitambulisho vya Taifa).
  9. Mwombaji anatakiwa kujua namba ya Nyumba, Mtaa na kata anayoishi.
  10. Kwa Watanzania walioko nje ya Nchi, wanatakiwa kupata uthibitisho wa ukaazi katika Nchi husika kutoka kwa Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ili kujaza sehemu ya makazi, Mtaa/Kata kwa usahihi.
  11. Endapo Mwombaji amepata vyeti vya Shule, Namba ya mlipa kodi (TIN) na Kadi ya mpiga kura; ni vyema kuambatanisha.
  12. Mwombaji anatakiwa kujaza Fomu kwa usahihi na kuhakikisha viambata vyake na taarifa alizo jaza katika mfumo hazikinzani na taarifa nyingine, kama vile taarifa za Shule au Biashara.
  13. Mwombaji anatakiwa kujaza taarifa zake kwa usahihi, na kuchapisha taarifa hizo katika fomu na kwenda kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa napoishi kwa ajili ya kugongewa Mhuri na Saini ya Mwenyekiti wa Mtaa wake.
  14. Mwombaji anatakiwa kufika katika Ofisi ya NIDA iliyoko kwenye Wilaya yake ya makazi akiwa na fomu iliyokamilika (Fomu iliyogongwa Mhuri na kuwekwa Saini ya Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa), pamoja na nakala ngumu za viambatisho vyake alivyopakia katika mfumo wakati wa usajili kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili.
  15. Kwa Mwombaji ambaye anahitaji kupata maelezo ya ziada; asisite kufika katika ofisi ya NIDA iliyopo karibu.

Kwa kuzingatia mambo haya muhimu, utakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa katika mchakato wa kujisajili mtandaoni na kupata kitambulisho chako cha nchi kupitia NIDA bila matatizo yoyote. Hii itakusaidia kujiimarisha zaidi katika jamii na kupata huduma mbalimbali zinazohitaji kitambulisho cha taifa.

Hatua za Kujisajili Mtandaoni

Kujisajili mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA ni mchakato rahisi unaofuata hatua kadhaa ambazo kila mwombaji anapaswa kuzifuata ili kuhakikisha wanafanikiwa katika kupata kitambulisho cha taifa. Hapa kuna hatua za kina za kujisajili:

1. Tembelea Tovuti ya Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa NIDA (https://eonline.nida.go.tz/)

Hatua ya kwanza ni kutafuta tovuti rasmi ya NIDA. Hakikisha unatumia tovuti iliyo sahihi ili kuepuka tovuti za udanganyifu.

2. Fungua Akaunti

Mara baada ya kufika kwenye tovuti, bofya kwenye kitufe cha “Jisajili au Create Account” au tumia linki https://eonline.nida.go.tz/Account/Register ili kupata fomu ya usajili. Jaza maelezo muhimu yaliyoombwa, ikiwa ni pamoja na barua pepe na nenosiri. Na hakikisha nenosiri linakidhi vigezo vilivyowekwa.

3. Thibitisha Barua Pepe

Baada ya kujaza fomu ya usajili, utapokea barua pepe ya uthibitisho. Fungua barua pepe hiyo na fuata kiungo kilichomo ili kukamilisha mchakato wa ufunguzi wa akaunti yako.

Soma hii :Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka

4. Jaza Fomu ya Maombi

Baada ya kuthibitisha akaunti yako, ingia kwenye mfumo kwa kutumia akaunti yako. Kisha, jaza fomu ya maombi ya kitambulisho cha taifa. Hakikisha unajaza maelezo yote kwa usahihi na ni muhimu kuzingatia viambatanisho vyako.

5. Tuma Maombi

Mara baada ya kumaliza kujaza fomu na kuangalia kwa makini taarifa zako, tuma maombi yako. Utapokea ujumbe wa kuthibitisha kuwa maombi yako yamepokelewa.

6. Tembelea Ofisi ya NIDA

Baada ya kutuma maombi, chukua fomu iliyochapishwa pamoja na vielelezo vyako vya uthibitisho na tembelea ofisi ya NIDA iliyoko katika eneo lako. Hakikisha unaelewa na kufuata taratibu zinazohitajika ili kukamilisha usajili wa alama za biometria.

7. Ufuatiliaji wa Maombi

Baada ya kukamilisha hatua za usajili, unaweza kufuatilia maendeleo ya maombi yako kupitia mfumo wa mtandaoni. Mfumo huu utakuwezesha kujua hali ya maombi yako na muda unaokadiriwa kukamilika.

Kwa kufuata hatua hizi kwa umakini, unaweza kufanikiwa kwenye mchakato wa kujisajili mtandaoni na kupata kitambulisho chako cha NIDA bila usumbufu mkubwa.

4 Fomu ya maombi ya kitambulisho cha NIDA kwa maombi ya kawaida

Ikiwa unapendelea utaratibu wa kawaida wa maombi ya kitambulisho cha utaifa utatakiwa kupakua na kujaza fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 1A: Jaza fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 1A kwa kalamu ya wino mweusi na kwa herufi kubwa. (Fomu inapatikana kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA, Wilayani/Serikali ya Mtaa na kwenye tovuti ya NIDA)

DOWNLOAD : fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa Namba 1A

Hakikisha una saini fomu yako ya maombi ya Utambulisho wa Taifa kwenye kipengele Namba 59/60 ama umeweka alama ya dole gumba iwapo hauna saini rasmi ama hujui kusoma na kuandika,

Gonga muhuri fomu yako ya Maombi ya Utambulisho wa Taifa kwenye Serikali ya Mtaa unakoishi kipengele namba 59/60 na kuandikiwa barua ya utambulisho wa makazi,

Ambatisha nyaraka zifuatazo, viambatisho hivi ni vya lazima:
i.   Cheti cha kuzaliwa,
ii.  Barua ya utambulisho wa makazi kutoka Serikali ya Mtaa unakoishi,
iii. Cheti cha kuzaliwa au Kitambulisho cha Taifa cha mzazi mmoja.

Ambatisha viambatisho vya ziada ulivyonavyo kati ya vifuatavyo:
i.  Vyeti vya Masomo-Msingi,Sekondari,Chuo,
ii.  Pasi ya kusafiria,
iii. Leseni ya udereva,
iv. Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN),
v.  Kadi ya bima ya afya,
vi. Kitambulisho cha mzanzibar mkaazi

Wasilisha fomu yako ya maombi kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA wilaya unakoishi kwa ajili ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia (kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole) ili kupisha hatua zinazofuata ziendelee.

Mavazi ya kuzingatia wakati wa Usajili: Ili picha ya mwombaji wa Utambulisho wa Taifa itoke katika ubora uliokusudiwa pindi unapowasilisha fomu ya maombi kwenye ubalozi husika kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole, unashauriwa kutovaa nguo; nyeupe, kijivu, bluu mpauko, pinki au nguo za kung’aa, jezi, nguo zenye nembo, michoro au maandishi, kofia aina yoyote na kutopaka hina viganjani ili alama za vidole zisomeke kirahisi,

Hatua mbalimbali za usajili na utambuzi wa watu:-
i.  Ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili,
ii. Uhakiki wa awali wa fomu za maombi,
iii. Uingizaji wa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta,
iv. Kuthibitishaji taarifa za mwombaji zilizo katika mfumo wa kompyuta,
v.  Uchukuaji wa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki,
vi. Utengenezaji wa Daftari Kuu la Taarifa za Watu,
vii. Uhakiki wa mwisho,
viii.Uchapishaji, uhakiki wa ubora na Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Ufafanuzi wa mambo msingi hitajika kwa baadhi ya hatua za usajili tajwa hapo juu;

Usajili – Ujazaji wa fomu (biographic data)

Mwombaji wa Kitambulisho Raia, Mgeni ama Mkimbizi anatakiwa kufika katika kituo/ofisi ya usajili na vivuli (Copy) ya nyaraka za kutambulisha makazi, uraia na umri wake kama ilivyoainishwa hapo juu katika kipengele cha mahitaji ya kila kundi wakati wa usajili.

Uchukuaji alama za kibaiolojia

Hatua hii ya Usajili inajumuisha upitiaji wa taarifa za mwombaji katika mfumo, uchukuliwaji wa alama za vidole, picha na utiaji wa saini ya kielektroniki ambapo kuna mambo msingi ya mwombaji kuzingatia ambayo ni;

Kwa ajili ya ubora na mwonekano mzuri wa picha mwombaji unashauriwa kutovaa nguo nyeupe, pinki, kijivu, bluu mpauko au nguo zenye rangi za kungaa sana. Kutovaa kofia ya aina yoyote wakati wa kupiga picha, au kupaka hina viganjani wakati wa uchukuaji wa alama za kibaiolojia.

Ili kurahisisha zoezi hili, mwombaji unaombwa kufika kwenye ofisi/kituo cha usajili na nyaraka halisi (original) za kuthibitisha uraia na umri wake mathalani, cheti cha kuzaliwa, pasipoti, vyeti vya elimu ya msingi na sekondari, leseni ya udereva, kitambulisho cha bima ya afya, kitambulisho cha mpigakura na kitambulisho cha mzanzibar mkazi.

Ugawaji Vitambulisho vya Taifa

Mwombaji anatakiwa kufika katika ofisi ya usajili katika wilaya husika ama kulingana na maelekezo/matangazo yanayotolewa katika eneo hilo ili kupatiwa kitambulisho chake kwa kuzingatia kuja na risiti maalumu aliyopatiwa na NIDA wakati alipokamilisha kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

 Msaada na Huduma kwa Wateja

Wakati wa mchakato wa kujisajili mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA, ni muhimu kujua jinsi ya kupata msaada na huduma kwa wateja, Kwa maelezo zaidi, tafadhali fika kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA Wilayani au wasiliana na NIDA kupitia Namba: 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006, 0677 146 666. Tovuti www.nida.go.tz, Barua pepe info@nida.go.tz, Facebook, Instagram, Twitter Nidatanzania

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Related Posts

Majina ya Form Six Waliochaguliwa Kujiunga na JKT Kwa Mujibu wa Sheria 2025

May 27, 2025

100+ misemo maarufu kuhusu maisha

May 25, 2025

Misemo ya dharau ya kuchekesha na ya kupost status

May 24, 2025

misemo ya kuchekesha kwenye magari

May 24, 2025

Misemo ya wahenga ya kuchekesha

May 24, 2025

Jinsi ya kusamehe na kusahau

May 24, 2025
Leave A Reply Cancel Reply

Latest Posts

Nafasi 135 za Kazi Kilombero Sugar Company Limited 2025

June 6, 2025

Nafasi  850 za Kazi Walimu Somo la Uchumi Daraja la IIIC MDAs & LGAs 2025

June 6, 2025

Nafasi 120 za kazi Walimu Somo la Fizikia Daraja la IIIC MDAs & LGAs 2025

June 6, 2025

Nafasi 700 za Kazi Walimu Somo la Biashara Daraja la III C MDAs & LGAs 2025

June 6, 2025

Nafasi za Kazi Halmashauri Mbalimbali Zilizotangazwa leo Ajira Portal 2025

June 5, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.