AzamPesa ni huduma ya kifedha ya kidijitali inayotolewa na Azam Telecom, ikiruhusu watumiaji kufanya miamala ya kifedha kwa njia rahisi na salama. Kupitia AzamPesa, unaweza kutuma na kupokea pesa, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbalimbali, na hata kufanya malipo ya biashara. Ikiwa unataka kujisajili na kuanza kutumia AzamPesa, fuata mwongozo huu wa hatua kwa hatua.
1. Mahitaji ya Kujisajili na AzamPesa
Kabla ya kuanza mchakato wa usajili, hakikisha unakidhi vigezo vifuatavyo:
- Unayo laini ya simu ya Azam Telecom.
- Una kitambulisho halali kama vile:
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Pasipoti.
- Leseni ya udereva.
- Kitambulisho cha mpiga kura.
- Una simu ya mkononi inayoweza kutuma na kupokea USSD au programu ya AzamPesa ikiwa unatumia smartphone.
2. Hatua za Kujisajili na AzamPesa
Njia ya Kwanza: Kupitia Mawakala wa AzamPesa
Kwa wale wanaopendelea usaidizi wa ana kwa ana, AzamPesa ina mtandao wa mawakala waliopo nchi nzima ambao wanaweza kusaidia katika mchakato wa usajili. Hatua za kufuata ni:
1: Tembelea Wakala wa AzamPesa
Tafuta wakala wa AzamPesa aliye karibu nawe. Unaweza kupata orodha ya mawakala kupitia tovuti rasmi ya AzamPesa au kwa kuuliza kwenye vituo vya huduma.
2: Wasilisha Taarifa Muhimu
Mpe wakala namba yako ya simu na kitambulisho chako cha NIDA. Wakala atakusaidia kujaza fomu ya usajili.
3: Thibitisha Usajili
Baada ya kujaza fomu, utapokea OTP kwenye simu yako. Ingiza namba hiyo ili kuthibitisha usajili wako.
4: Usajili Umekamilika
Baada ya kuthibitisha, akaunti yako ya AzamPesa itakuwa tayari kwa matumizi.
Njia ya Pili: Kujisajili Kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja
- Piga simu kwa huduma kwa wateja wa AzamPesa kupitia namba yao ya msaada.
- Toa taarifa zako za usajili ikiwa ni pamoja na jina kamili, namba ya simu, na namba ya kitambulisho.
- Utapokea ujumbe wa uthibitisho kwenye simu yako.
- Weka PIN yako ya siri na uthibitishe usajili wako.
Soma Hii :Jinsi ya kujisajili katika mfumo NeST na Kuomba Zabuni
Njia ya Tatu: Kujisajili Kupitia Programu ya AzamPesa
- Pakua na sakinisha (install) programu ya AzamPesa kutoka Google Play Store au Apple App Store.
- Fungua programu na bonyeza sehemu ya “Jisajili”.
- Jaza taarifa zako binafsi na namba ya simu.
- Thibitisha usajili wako kwa kutumia msimbo wa OTP utakaotumwa kupitia SMS.
- Weka PIN yako ya siri ili kukamilisha usajili.
3. Jinsi ya Kutumia AzamPesa
Mara baada ya kujisajili, unaweza kuanza kutumia huduma za AzamPesa kwa urahisi kupitia simu yako.
Kupitia USSD (Simu za Kawaida)
- Piga 15008# kwenye simu yako ya mkononi.
- Chagua huduma unayotaka kutumia kama vile:
- Kutuma pesa.
- Kupokea pesa.
- Kununua muda wa maongezi.
- Kulipia bili mbalimbali.
- Fuata maelekezo na weka PIN yako ili kuthibitisha muamala wako.
Kupitia Programu ya AzamPesa
- Fungua programu ya AzamPesa kwenye simu yako.
- Ingia kwa kutumia namba yako ya simu na PIN yako.
- Chagua huduma unayotaka kutumia.
- Thibitisha muamala wako na utapokea ujumbe wa mafanikio.
Kujisajili Kupitia WhatsApp
Kwa wale wanaopendelea kutumia WhatsApp, AzamPesa imetoa njia rahisi ya kujisajili kupitia jukwaa hilo. Fuata hatua hizi:
1: Pata Kiungo cha Usajili
Tembelea kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za AzamPesa na upate kiungo cha “JISAJILI WhatsApp”. Bofya kiungo hicho ili kufungua chati ya WhatsApp moja kwa moja.
2: Anza Mchakato wa Usajili
Mara chati ya WhatsApp inapofunguka, tuma neno “Habari”. Kisha, chagua namba 1 kwa ajili ya “Kusajili namba” na tuma.
3: Ingiza Namba ya Simu
Andika namba yako ya simu na tuma.
4: Thibitisha kwa OTP
Utapokea OTP kupitia ujumbe mfupi. Ingiza namba hiyo kwenye chati ya WhatsApp ili kuthibitisha.
5: Thibitisha Namba ya NIDA
Ingiza namba yako ya NIDA na ujibu maswali machache ya uthibitisho.
6: Usajili Umekamilika
Baada ya hatua hizi, utapokea ujumbe unaothibitisha kuwa usajili umekamilika na unaweza kuanza kutumia huduma za AzamPesa.
Azam pesa huduma kwa wateja
Kama una maswali yoyote, tafadhali usisite kuwasiliana nasi.
Timu yetu ya huduma kwa wateja ipo tayari kukusaidia masaa 24.
Tafadhali jaza taarifa zifuatazo:
WhatsApp : +255677822222
Haile Selassie Rd. Plot 208
P.O. Box 2517, DSM, Tanzania.