Kama unatamani Jina lako la biashara ndio liwe jina la kampuni yako yakupasa ufuate utaratibu huu hapa chini kuweza kubadilisha na kukamilisha usajili.
➡️ Hatua ya kwanza,utatakiwa kufunga jina la biashara. Jinsi ya Kufunga ni kama ifuatavyo
i) Ingia kwenye tovuti ya Brela,ingia sehemu ya majina ya biashara,nenda form za majina ya biashara, pakua form No.7 kisha uijaze
ii) Rudi kwenye akaunti yako ya ORS, kisha nenda sehemu ya kufunga jina la Biashara, utaulizwa sababu za kufunga jina la biashara jaza na upakue form ya majumuisho (Consolidated Form) ijaze kishaiweke kwenye mfumo pamona na ile form No.7
iii) Fanya malipo ya Tshs 15,000/= Tuu, maombi yako ya kufunga jina la biashara yatakuwa yamepokelewa.
➡️ Hatua ya Pili, Andaa katiba ya kampuni,na sehemu ya shughuli za kampuni mwanzoni ktk kifungu namba 3 utaandika kuwa kampuni itachukua madeni na mali ya jina la biashara ambalo lilikuwa na usajili nambali fulani.
Vitu vingine vya kuwa navyo nikama ifuatavyo
i) Katiba ya kampuni
ii) Anuani ya eneo kampuni ilipo
iii) Majina ya wanahisa na hisa zao
iv) NIDA za wakurugenzi na wanahisa
v) TIN za wakurugenzi
vi) Form ya Majumuisho
vii) Form ya maadili.
SOMA HII :Jinsi Ya Kufunga Biashara TRA
Kama unajina lako la Biashara na unatamani kulitumia kufungua kampuni, basi usisite kuwasiliana nasisi kwa maswali au msaada zaidi. Tupo kwaajili yako.