Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ni chombo huru cha kikatiba kilichoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Tume hii ina jukumu la kusimamia na kuratibu uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani nchini Tanzania.
Jina la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mwenyekiti wa sasa ni Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele.
Majukumu ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ana majukumu yafuatayo:
Kusimamia na Kuratibu Uendeshaji wa Chaguzi: Kuhakikisha uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani unafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
Kusimamia Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura: Kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili waweze kushiriki katika uchaguzi.
Kuhakikisha Utekelezaji wa Sheria na Kanuni za Uchaguzi: Kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni, na taratibu zinazohusiana na uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.
Kuhamasisha Ushiriki wa Wananchi katika Uchaguzi: Kutoa elimu ya mpiga kura na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.
Kusimamia Uteuzi na Mafunzo ya Watendaji wa Uchaguzi: Kuhakikisha watendaji wa uchaguzi wanateuliwa kwa sifa stahiki na kupatiwa mafunzo yanayowezesha utekelezaji mzuri wa majukumu yao.
Kuhakikisha Uwiano wa Kijinsia na Uwiano wa Kijiografia katika Tume: Kuhakikisha uwakilishi wa pande zote za Muungano katika uongozi wa Tume, kwa mujibu wa Katiba na sheria husika.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na majukumu yake, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya INEC: www.inec.go.tz.