Kutokwa damu kipindi cha ujauzito ni hali ambayo wanawake wengi wanakutana nayo, lakini ni suala ambalo linapaswa kushughulikiwa kwa umakini mkubwa. Ingawa si kila kutokwa damu ni dalili ya tatizo kubwa, baadhi ya hali zinazohusiana na kutokwa damu wakati wa ujauzito zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa mama na mtoto.
Kumbuka:
Kutokwa na Damu katika mwezi wa kwanza wa Ujauzito, endapo ikiwa inafanana na siku ya Hedhi kabla ya kupata Ujauzito ijapokuwa Damu zinatoka kidogo na kwa siku chache huwa inatokana na Mimba baada ya kutungwa inapojishikiza kwenye Mji wa Uzazi.
Endapo hutokana na Hali hii Mimba inaposhikiza kwenye Mji wa Uzazi huwa ni hali ya kawaida unahitaji kwenda hospitali kwani si rahisi Mjamzito kugundua kuwa ana hiyo Hali bila usaidizi wa Daktari.
Unapo tokwa na Damu kipindi cha Ujauzito hata kama huna maumivu unatakiwa kwenda hospitali upewe Matibabu na vile vile hutakiwi kushiriki Tendo la Ndoa badala yake muda mwingi utatumia kulala na utatembea tuu unapokwenda haja na kuoga basi hii ni kwa Wajawazito wote wanaopata Dalili za kutokwa Damu wakati wa Ujauzito haijalishi umri gani wa Mimba.
Kuvuja damu katika awamu za mwisho wa ujauzito husababishwa na nini?
Kuvuja damu katika awamu za mwisho za ujauzito au kuvuja damu kabla ya kuzaa mara nyingi husababishwa na kuvuja damu kutoka kwa plasenta, ingawa kuna visababishi vingine vichache vinavyotokea katika uterasi au sehemu zingine za mfumo wa uzazi. Kwanza, tutaorodhesha visababishi hivi kwa ufupi, kisha kufasili kwa kina kuhusu plasenta kujitenga kutoka pembezoni mwa uterasi, privia ya plasenta na kupasuka kwa uterasi, kwa sababu hizi ni hali zinazohitaji huduma ya dharura ili kuokoa maisha.
- Kutengeka kwa plasenta: hali hii hutokea iwapo plasenta itatengeka kabla ya wakati (mapema sana) kutoka kwenye sehemu yake ilipojibandika kwa kawaida katika thuluthi mbili juu ya uterasi.
- Privia ya plasenta: hali hii hutokea wakati plasenta imejibandika katika sehemu ya chini sana ya uterasi, ikikaribia seviksi sana, au hata kuifunika.
- Kupasuka kwa uterasi: hali hii inaweza kutokea iwapo leba itadumu kwa muda mrefu au leba itazuiliwa, ambapo uterasi huraruka au kupasuka baada ya majaribio mengi ya kusukuma fetasi.
- Kupasuka kwa vena ya varikosi katika eneo la uke: hii hutokea iwapo vena imejipinda na kupanuka. Hivyo basi, uterasi inaweza kujeruhiwa kwa urahisi na kuvuja, hasa katika leba na kuzaa.
- Utetelezi mkuu: ute uliochanganyika na damu unaotoka ukeni kuashiria mwanzo wa leba huitwa utetelezi; wakati mwingine, kizibo hiki cha ute kinapotoka kinaweza kufuatiwa na uvujaji mkubwa wa damu unaoitwa utetelezi mkuu, ambao hukoma peke yake bila usaidizi wowote. Hata hivyo, mama anapaswa kupendekezewa rufaa kila wakati.
Je Mara baada ya Mimba kuharibika natakiwa kufanya nini ili nipate Mtoto na nijifungue salama?.
Mambo ya kufanya ni kama:
1. Tambua kitu gani kimefanya Mimba kuharibika na ukiondoshe hicho kitu endapo kimegundulika. Kumbuka si lazima kuwe na sababu zinazojulikana wakati mwingine unaweza usipate sababu ya Mimba yako kuharibika maana inaweza kutokea tu.
2. Pata Matibabu stahiki kulingana na umri wa Mimba ilipoharibika lakini pia kulingana na Hali yako kiafya na Kimwili.
3. Unahitaji kutumia njia ya Uzazi wa Mpango kwa muda wa Miezi sita kama huna haraka ya kupata Ujauzito endapo unaharaka na Ujauzito unaweza kusubiri mpaka Miezi Mitatu ndipo upate Ujauzito mwingine.
4. Kipindi cha kusubiri kabla ya kupata Ujauzito utahitaji kutumia mlo kamili, Vitamini mfano folic acid na Madini Chuma na kuujenga Mwili wako kwa ajili ya kujiandaa na kubeba Mimba nyingine.
5. Unahitaji kujilinda na kuepukana na Magonjwa ya zinaa mfano Gono, kaswende na UKIMWI.
Jinsi ya kushughulikia mwanamke anayevuja damu katika awamu za mwisho za ujauzito
Ukitambua kwamba mwanamke anavuja damu na unashuku kuwa ana plasenta iliyotengeka, privia ya plasenta, uterasi iliyopasuka, au kuvuja damu kufuatia visababishi vingine, chukua hatua hizi:
- Usimchunguze ukeni
- Tathmini kwa haraka hali zote za mwanamke, pamoja na dalili muhimu: mrindimo, shinikizo la damu, pumzi na halijoto, baini kama ameparara, ana uchovu, kizunguzungu, na kuchanganyikiwa.
- Ukikisia kuwa ana mshtuko, anza matibabu haraka iwezekanavyo kwa kumdungia viowevu vya Chumvi ya Kawaida au mchanganyiko wa kiowevu cha laktesi ya Ringer ndani ya mishipa. (Utajifunza jinsi ya kufanya hivi katika somo la nadharia katika Kipindi cha 22 na kuukuza ustadi wako katika mafunzo ya kiutendaji.)
- Hata ikiwa hakuna ishara za mshtuko, utilie mshtuko maanani huku ukiendelea kutathmini hali ya mwanamke kwa kuwa inaweza kubadilika ghafla. Ikiwa mshtuko utatokea, chukua hatua zilizoelezwa hapo juu.
- Kwa haraka, watafute watu wakusaidie, wajulishe kuhusu uzito wa hali hiyo na utekeleze mpango wa kushughulikia matatizo ambao uliandaa wewe na mwanamke kama sehemu ya utunzaji maalum katika ujauzito (Kipindi cha 15 cha Moduli hii). Kwa mfano, watafute wanakijiji wakusaidie kumsafirisha haraka hadi kituo cha juu cha afya; hakikisha kuwa watu wenye afya njema wameandamana naye ili kumtolea damu iwapo atahitaji.
Je nikiwa na Ujauzito nahitaji kufanya mazoezi gani?.
Endapo wewe ni Mjamzito huhitaji mazoezi makubwa mfano kukimbia au kuruka ruka sana zaidi ya kutembea tembea na kufanya shughuli ndogo ndogo za nyumbani kama kupalilia maua,kulima Mboga Mboga, kufagia, kuosha vyombo na kufanya mazoezi ya kunyoosha viungo katika kipindi cha Ujauzito wako.