Wanandoa Wengi ambao ni wazazi watarajiwa wamekuwa wakijiuliza swali hili maranying Je Tendo la Ndoa Kwa Mjamzito Mwisho Lini Kufanya?
JIBU: Mjamzito anaweza kushiriki Tendo la Ndoa kipindi chote cha Ujauzito wake kuanzia Mimba inapokuwa na wiki 1 hadi Mimba inapokuwa imekomaa na kipindi ambacho anaelekea kujifungua(Wiki 37 hadi 42), japokuwa kuna Mambo ambayo yanaweza fanya Mjamzito asishiriki tendo la Ndoa hata kama ana hamu au shauku ya kufanya Mapenzi au kushiriki Tendo ndo la Ndoa na mwenza wake.
MJAMZITO USISHIRIKI TENDO LA NDOA KAMA UNA SIFA HIZI.
Mama Mjamzito hatoruhusiwa kushiriki Tendo la Ndoa hata kama anapata hamu au shauku ya kufanya Tendo hilo katika kipindi cha Ujauzito ikiwa ana sifa au Mambo yafuatayo;
1. Kutokwa Damu Ukeni katika kipindi chochote cha Ujauzito.
2. Mimba Kutishia Kuharibika ktk kipindi cha Ujauzito.
3. Historia ya Mimba kuharibika mara kwa mara kabla ya Wiki 28 na nk,
4.Endapo Kondo la nyuma limejishikiza karibia na Mlango wa Uzazi na Mjamzito anatokwa na Damu.
5.Wakati mwingine Mjamzito anaweza asishiriki Tendo hilo kutokana na mabadiliko ya Homoni ambayo yanaweza kupelekea kujisikia vibaya, kutapika Mara kwa Mara hususani kipindi cha Miezi Mitatu ya mwanzoni, kupungua kwa hamu ya Tendo la Ndoa, Hata kama hana shida ambazo zimetajwa hapo juu.
JE MTOTO ALIYEPO TUMBONI ANAWEZA KUATHIRIWA KUTOKANA NA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA.
Endapo huna changamoto yoyote kati ya Tano zilizo tajwa hapo juu.
Unaposhiriki Tendo la Ndoa hata kama Mbegu za Mwanaume zikimwagwa kwenye Uke, Mtoto hawezi kuathiriwa. Hii ni kwa sababu Mtoto hulindwa na Kuta ngumu au Chupa imara inayo mzunguka lakini pia Mlango wa Uzazi huwa umefungwa vizuri na hauwezi kupitisha kitu chochote labda kama kutakuwa na Maambukizi ya vijidudu ambayo yamepelekea kupasuka kwa Chupa au kuchanika kwa Kuta zinazo mzunguka Mtoto.
UMUHIMU WA TENDO LA NDOA KIPINDI CHA MIEZI MITATU YA MWISHO YA UJAUZITO.
Baadhi ya Maandiko yanaelezea kwamba Mjamzito ambaye hana changamoto tajwa hapo juu, anaposhiriki Tendo la Ndoa ipasavyo husaidia katika kuanzisha Uchungu na kuivisha Mlango wa Uzazi na hivyo huwezesha kuanzishwa kwa Uchungu kipindi ambacho Mjamzito anatakiwa kujifungua.
Hii ni kwa sababu:
1.Kwenye Ute uliochanganyika na Mbegu anazotoa Mwanaume kuna kiasi kidogo cha kemikali ya prostaglandini E ambayo huanzisha Uchungu mwishoni mwa Ujauzito.
- Tendo la Ndoa husababisha utolewaji wa Homoni ya Oksitosini ambayo huhusika katika kuhakikisha Mjamzito anapata Uchungu.
- Husaidia kuongeza nguvu ya kubana na kuachia ya mfuko wa Uzazi ili kuweza kumtoa Mtoto nje na kujifungua kwa Mjamzito.