JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Kila Mwanaume hutamani kumpata mwanamke mwwene tabia njema wa kumuoa hata kama mwaname anatabia mbaya,mlevi au malaya liapokuja swala la kuoa hutuliza kichwa na kutafuta wife material kwaaili yake na maadili ya wanawe.

Katia Pitapita zako kijana Ukibahatika kukutana na Mwanamke mwenye sifa hizi hiyo ni mali safi usimuache weka ndani utanishukuru.

Miongoni mwa misingi hiyo ni lazima uchagua mwanamke ambaye atakuwa na sifa hizi:

1. Mwanamke ambaye hana tamaa ya pesa.
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yuleyule wa siku zote, huyu ni ‘wife material’.

Soma hii :sms za mahaba usiku na sms za kutongoza

2. Mwanamke anayependa watoto 
Utajuaje kama mwanamke uliyenaye ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo, huyo ni wife material unatakiwa kumoa haraka.

3. Mwanamke ambaye ana heshima ya kweli. 
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia.

4. Mwenye uwezo wa kujishusha.
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa, yaani yeye hata akikosea anakuwa hayupo tayari kusema samahani msichana wa aina hii hafaai bali  Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, nawewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia.

5. Mtu ambaye anakushauri kwenye mema. 
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya. Kwa mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo.

Sifa za Nyongeza za Mwanamke wa kuoa

AKUPENDE KWA MAANA HALISI YA KUKUPENDA

Unapoingia kwenye maisha ya ndoa, unatarajia kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwenza wako. Wapo baadhi ya wanawake ambao wanaonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.Wanachotaka wao ni aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.Kwa nini ni vizuri kumpata mwanamke mwenye mapenzi ya dhati kutoka moyoni na si kwamba akupende kutokana na mali au fedha zako na muonekano wako? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru Mungu. Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yenu.

HILI LA TABIA NDO’ KILA KITU

Linapokuja suala na kuoa, tabia inakuwa kitu cha awali sana kuangaliwa. Hii ni kwa sababu, wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa sifa ya kuitwa mke kutokana na tabia zao chafu.Hakuna mwanaume anayeweza kudiriki kumpa nafasi msichana kuwa mke wake wakati ana tabia chafu. Endapo utaangalia uzuri wa sura kisha ukafanya maamuzi ya kuoa, utakuwa unajichimbia kaburi.

AOTE MAFANIKIO

Hivi karibuni kume-kuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi ‘golikipa’.Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa mafanikio kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijini na hata vijijini.Ile dhana ya kuoa mwanamke kwa ajili ya kukustarehesha tu imepitwa na wakati. Hizi ni zama za kutafuta mtu wa kushirikiana naye kwenye kusaka mafanikio.

UVUMILIVU

Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha. Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha. Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanaume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi wanapoumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine linaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mwenye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe. Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

HANA MAKUZI

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Wa kumuoa hatakiwi kuwa hivyo.Anatakiwa kuwa tayari kula dagaa pale inapobidi na kama uwezo wa kula nyama upo basi atakula. Awe tayari kutembea kwa miguu pale usafiri wa maana utakapokosekana, awe tayari kuvaa nguo za kawaida, awe tayari kutumia simu ya tochi.Kwa kifupi mwanamke ambaye ni ‘wife material’ anatakiwa kuwa tayari kuishi maisha ya aina zote

wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Wa kumuoa hatakiwi kuwa hivyo.Anatakiwa kuwa tayari kula dagaa pale inapobidi na kama uwezo wa kula nyama upo basi atakula. Awe tayari kutembea kwa miguu pale usafiri wa maana utakapokosekana, awe tayari kuvaa nguo za kawaida, awe tayari kutumia simu ya tochi.Kwa kifupi mwanamke ambaye ni ‘wife material’ anatakiwa kuwa tayari kuishi maisha ya aina Yoyote.

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Share.

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Leave A Reply