Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo linaloweza kumkumba mwanaume kwa nyakati tofauti. Hali hii inaweza kusababisha msongo wa mawazo, kupungua kwa kujiamini, na matatizo katika mahusiano.
CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kuwa na mafuta mengi ya Lehemu ndani ya mwili (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo
Kuvuta sigara na unywaji wa pombe kupindukia. Yaani mtu unakuwa Huna kiasi Kila siku umelewa tu.
Uzito kupita kiasi na unene uliozidi sana.
Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi, hapa ndiyo mtihani.
Kisukari, wagonjwa wa muda mrefu.
Kuwa na mawazo na wasiwasi mwingi.
Matumizi ya madawa mbalimbali
Umri mkubwa hasa wazee zaidi ya 65+
Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili na hisia.
Kuwa na tatizo la kibofu cha mkojo.
Tabia za kujichua kwa mda mrefu. mrefu( masterbation)/ Punyeto.
Kutopata usingizi kamili usiku.
Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine
SOMA HII : Jinsi Ya Kutumia Bamia Kuongeza Ute Ukeni.
Dalili za Upungufu wa Nguvu za Kiume
1️⃣ Kushindwa kusimama kwa uume (Erectile Dysfunction – ED)
🔹 Hili ni tatizo kuu ambapo mwanaume anapata shida kusimamisha uume au kudumisha msimamo wake kwa muda mrefu wa kutosha kufanya tendo la ndoa.
2️⃣ Kushindwa kurudia tendo la ndoa mara ya pili
🔹 Baada ya kushiriki tendo la kwanza, unakosa nguvu au hamu ya kurudia mara ya pili.
3️⃣ Uume kuwa legelege wakati wa tendo
🔹 Hata kama unapata msisimko, uume hauwi mgumu wa kutosha kuendelea na tendo.
4️⃣ Kufika kileleni haraka (Premature Ejaculation)
🔹 Unapomaliza haraka mno, hata kabla ya mwenza wako kufurahia tendo.
5️⃣ Kukosa hamu ya tendo la ndoa (Low Libido)
🔹 Unapoteza hamu ya kushiriki ngono kwa muda mrefu.
6️⃣ Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa
🔹 Unahisi uchovu kupita kiasi baada ya kushiriki tendo, hata kama lilikuwa la muda mfupi.
7️⃣ Kuwa na mbegu chache au dhaifu
🔹 Mbegu za kiume kuwa chache au dhaifu, jambo linaloweza kusababisha ugumu wa kupata mtoto.
Jinsi ya Kujikinga Usipate Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume
Waswahili husema kinga ni bora Kuliko tiba chukua tahadhari Mapema kwa kufanya yafuatayo ili Usikumbwe na Tatizo la nguvu za kiume
1:Fanya mazoezi – Angalau dakika 30 kwa siku, chuchumaa na simama hata chumbani kwako Kila siku.
2:Kula vyakula asilia na usile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi sana ni hatari.
3:Tibu magonjwa yako yanayokuweka hatarini kama kisukari, moyo, punguza unene na mengine
4:Punguza (balansi) kiwango cha lehemu (choresterol) au mafuta yaliyozidi
5:Balansi uzito wako
6:Usivute sigara saaana
7:Punguza au acha kunywa pombe
8:Punguza mawazo
9:Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
10:Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa angalau 8 hadi 10.
11:Usitumie dawa zenye kemikali nyingi huathiri mfumo wa uzazi
12:Kunywa maji ya kutosha kwa siku ili kusaidia mwili kupona na kutoa takamwili.
Tiba za Asili na Njia za Kuimarisha Nguvu za Kiume
Zifuatazo ni baadhi ya njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume;

1. Kula Lishe Bora.
Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume(Low sperm count). Kama utarekebisha tu aina ya chakula unachokula kunaweza kupelekea kutibu changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume ambapo unashauriwa kupunguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano, badala yake ongeza zaidi matumizi ya matunda, mboga mboga. Hii inaweza kukusaidia kutibu tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume kwa haraka sana.

2. Epuka Matumizi Yaliyokithiri Ya Vyakula/Vinywaji Vyenye Kafeini Kwa Wingi.
Kama unasumbuliwa na tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume ni vyema ukaepuka matumizi yaliyokithiri ya vyakula au vinywaji vyote vyenye kafeini kwa wingi. Mfano wa vyakula/vinywaji vyenye kafeini kwa wingi ni pamoja na chai ya kahawa, soda nyeusi zote, malta, redbull, chokoleti n.k

3. Tumia Kitunguu Swaumu Kwa Wingi.
Kitunguu swaumu kina ‘Selenium’ na pia kinasaidia kuondoa sumu mwilini, mambo haya mawili muhimu yanasaidia kuongeza spidi ya mbegu za kiume. Pia kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume. Hivyo unashauriwa kuongeza matumizi ya kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika. Vile vile unaweza kutafuna punje 2 mpaka 3 za kitunguu swaumu kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata (chop) hizo punje 2 au 3 vipande vidogo vidogo kisha unywe na maji.

4. Ulaji Wa Ndizi.
Ndizi ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja kiitwacho ‘Bromelain’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa (testosterone). Pia ndizi zina Magnesium, vitamini B1 na vitamini C, vitu ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

5. Ulaji Wa Mbegu Za Maboga.
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya zinki ambayo ni muhimu katika kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosteroni. Pia mbegu za maboga zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni muhimu katika kuongeza idadi ya mbegu za kiume. Vile vile mbegu za maboga zina madini ya kalsiamu, Potasiamu, Phosphorasi na Niacin.

6. Ulaji Wa Mboga Za Majani Kwa Wingi.
Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mbegu za kiume.

7. Ulaji Wa Vyakula Vyenye Foliki Asidi Kwa Wingi.
Vyakula vyenye foliki asidi kwa wingi ni pamoja na karoti, Parachichi, Ufuta, maharage, papai, bamia. Hivvyo isipite siku bila kula parachichi walau moja na kutafuna karoti walau moja ikiwa unachangamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume walioongeza ulaji wa vyakula vyenye foliki asidi na zinki waliongeza uwingi wa mbegu zao za kiume kwa zaidi ya asilimia 74 kwa muda wa wiki 2 tu.

8. Kunywa Maji Mengi Kila Siku.
Hili ni suluhisho rahisi lisilohitaji gharama yoyote kwa wale wanaosumbuliwa na changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume. Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu za kiume. Hivyo kama utatekeleza njia zote zilizotajwa hapo juu halafu ukasahau kunywa maji hesabu umekosea sana. Kutegemeana na uzito wako unaweza kunywa maji walau lita 2 mpaka lita 3 kwa siku, hii itakusaidia kwani mbegu za kiume zimetengenezwa kwa maji, na pia zipo kwenye hali ya kimiminika.

9. Parachichi.
Parachichi lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamin E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume. Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkubwa wa kimapenzi.

10. Tikiti Maji.
Matunda haya pia yana uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume. Tikiti lnapaswa kuliwa pamoja na mbegu zake, angalau vipande viwili au vitatu kwa siku.

11. Komamanga.
Haya ni aina ya matunda ambayo ndani yake yana mbegu nyekundu. Koma manga lina tajwa kuwa na virutubisho muhimu vya kusisimua misuli ya uume na kuamsha hisia za kushiriki tendo la ndoa.

12. Pweza Na Chaza.
Aina hizi za viumbe wa baharini, huwa na madini ya zinki na chumvi ambayo ambayo yanatajwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinavyosababisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa. Unashauriwa kujenga utaratibu wa kunywa supu ya pweza mara kwa mara na matokeo yake utayaona.

13. Pilipili.
Pilipili zina uwezo mkubwa wa kumaliza changamoto ya upungufu wa mguvu za kiume. Unaweza kuchangaya pilipili kwenye chakula au ukala hivyo hivyo kwa kutafuna kiasi kidoogo mara kwa mara. Pilipili zina virutubisho ambavyo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume na kuamsha hisia za mapenzi.

14. Kunazi (Blueberries).
Haya ni matunda madogo madogo jamii ya zabibu ambayo huliwa na binadamu. Matunda haya yameelezwa kuwa na nguvu kama ilivyo dawa ya Viagra. Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa matunda haya yana vichocheo ambavyo hulainisha mishipa ya damu na kufanya damu isambae kwa kasi kuelekea kwenye viungo vya kiume.

15. Ufanyaji Wa Mazoezi Mara Kwa Mara.
Mazoezi ya nusu saa mara tatu kwa wiki kwa wanaume yana uwezo wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mujibu wa wanasayansi ambapo wanaume ambao wameendelea na zoezi la kukimbia kila wakati, mbegu zao za kiume huwa na afya njema kulinganan na watafiti wa jarida la maswala ya uzazi. Watafiti wanasema ni muhimu kufanya mazoezi hayo kwa kiwango cha wastani, kwa sababu mazoezi ya kupita kiasi hudhuru kiwango cha uzalishaji wa mbegu hizo za kiume.

Ziada : Zingatia yafuatayo:
1. Kula Vyakula Vinavyoongeza Nguvu za Kiume
✔ Ndizi – Husaidia kuongeza mzunguko wa damu.
✔ Karanga na mbegu za maboga – Hutoa madini ya Zinc yanayosaidia uzalishaji wa testosterone.
✔ Spinachi na mboga za majani – Zinaboresha mzunguko wa damu kwenye uume.
✔ Mayai na nyama nyekundu – Husaidia kuongeza protini na testosterone.
✔ Parachichi na tikiti maji – Vinasaidia kuongeza msisimko wa mwili.
2. Fanya Mazoezi Mara kwa Mara
💪 Mazoezi kama kukimbia, push-ups, na squats husaidia kuongeza mzunguko wa damu na kuzalisha testosterone kwa wingi.
3. Epuka Msongo wa Mawazo
🧘♂️ Tafuta muda wa kupumzika, meditations, na epuka mawazo mengi.
4. Punguza Pombe na Sigara
🚫 Pombe nyingi na sigara vinaathiri mzunguko wa damu na kupunguza nguvu za kiume.
5. Tumia Dawa za Asili
🌿 Asali na Tangawizi – Changanya kijiko kimoja cha tangawizi na asali na unywe mara mbili kwa siku.
🌿 Unga wa mbegu za maboga – Tumia kijiko kimoja na maziwa asubuhi na jioni.
🌿 Kitunguu saumu – Husaidia kuongeza mzunguko wa damu kwenye uume.
6. Pata Usingizi wa Kutosha
😴 Lala kwa saa 7-8 kila usiku ili mwili upate muda wa kuzalisha testosterone ya kutosha.