Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ni chombo muhimu kinachowezesha wanafunzi wengi wa Tanzania kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu kwa kuwapa mikopo ili kusaidia kugharamia ada, vitabu, na mahitaji mengine ya kimasomo. Mikopo hii ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi ambao hawawezi kumudu gharama za masomo kwa njia nyingine. Hata hivyo, ili kupata mkopo huu, kuna sifa maalum ambazo kila mwanafunzi anapaswa kutimiza.
Makala hii itakuletea mwongozo kamili kuhusu sifa za kupata mkopo wa HESLB na jinsi unavyoweza kujiandaa ili uweze kufuzu kupata mkopo wa bodi hii.
Sifa Za Kupata Mkopo wa Bodi Ya Mikopo Tanzania HESLB
Ili kuhakikisha kuwa mikopo ya HESLB inawafikia walengwa sahihi, kuna sifa muhimu ambazo kila mwombaji anatakiwa kutimiza. Sifa hizi zimeainishwa katika Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo na zinahusisha vipengele vya jumla na vile vya msingi kwa wanafunzi wanaondelea na masomo.
Sifa za Jumla Kwa Wanafunzi wanaojiunga na Vyuo
- Uraia: Mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania.
- Umri: Mwombaji ashindwe miaka 35 wakati wa kuomba mkopo.
- Udahili: Ni sharti mwombaji awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu ya juu nchini Tanzania inayotambuliwa.
- Maombi kupitia OLAMS: Maombi yote ya mkopo yanafanywa kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS).
- Ukosefu wa kipato: Mwombaji hapaswi kuwa na chanzo kingine cha mapato, kama vile ajira au mkataba serikalini au sekta binafsi.
- Kurejesha mkopo uliopita: Kwa wale ambao wameshawahi kupokea mkopo wa HESLB, ni lazima wawe wamerejesha angalau asilimia 25 ya mkopo huo kabla ya kuomba tena.
- Ufaulu wa masomo: Waombaji wanatakiwa wawe wamehitimu elimu ya kidato cha sita au stashahada ndani ya miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi 2024.
Sifa za Msingi kwa Wanafunzi Wanaondelea na Masomo
Kwa wanafunzi ambao tayari wako vyuoni na wanataka kuendelea kupata mkopo, au wale wanaotaka kuomba mkopo kwa mara ya kwanza wakiwa wanaendelea na masomo, wanatakiwa kutimiza yafuatayo:
- Ufaulu: Ni lazima wawe wamefaulu mitihani yao ili waweze kuendelea na mwaka unaofuata wa masomo.
- Barua ya kurejea (kama inafaa): Kwa wale waliowahi kuahirisha masomo, wanapaswa kuwa na barua ya kurejea masomoni kutoka chuo husika.
- Kurudia mwaka: Wanafunzi hawaruhusiwi kurudia mwaka wa masomo zaidi ya mara moja katika kipindi chote cha masomo yao.
- Kuahirisha masomo: Hairuhusiwi kuahirisha masomo kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo.
- Namba ya Utambulisho ya Taifa (NIN) na namba ya usajili: Lazima wawasilishe namba hizi kabla ya kupokea fedha za mkopo katika mwaka wao wa tatu wa masomo.
SOMA HII :Fomu za Kujiunga Na Shule Kidato Cha Tano
Jinsi Ya Kutuma Maombi Ya Mkopo
Maombi yote ya mkopo yatafanyika kupitia Mfumo wa Maombi na Usimamizi wa Mikopo (OLAMS). Waombaji wote wa mikopo WANAKUMBUSHWA kutumia namba ileile ya Mtihani wa Kidato cha Nne iliyotumika wakati wa kuomba udahili.
Baada ya kukamilika kwa mchakato wa maombi kwenye mtandao, waombaji watapaswa kupakua (ku-print) nakala za fomu za maombi na Mkataba wa Mkopo kutoka kwenye mtandao, kugonga mihuri sehemu husika, kusaini fomu, kuambatisha nyaraka zinazohitajika na kuzipakia (upload) kwenye mfumo wa OLAMS kurasa zilizosainiwa