Harufu mbaya ukeni ni tatizo linalowakera wanawake wengi duniani kote. Ingawa ni jambo la kawaida kwa uke kuwa na harufu kidogo, harufu kali, mbaya, au isiyofurahisha inaweza kuashiria tatizo la kiafya ambalo linahitaji kutibiwa.
Sababu za Harufu Mbaya Ukeni
1. Maambukizi ya fangasi (Vaginal yeast infection)
Maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya Candida, ambayo huishi kawaida ndani ya uke bila matatizo. Lakini, wakati fangasi hao wanapoongezeka kupita kiasi, husababisha dalili kama harufu mbaya, maumivu, na ute mweupe wenye mvuto wa maziwa.
2. Maambukizi ya bakteria (Bacterial vaginosis)
Ni maambukizi yanayosababishwa na mabadiliko ya bakteria wa kawaida ndani ya uke. Hali hii husababisha harufu kali kama samaki na ute wenye rangi ya kijivu.
3. Magonjwa ya zinaa (STIs)
Baadhi ya magonjwa ya zinaa kama gonorrhea, chlamydia, na trichomoniasis huleta harufu mbaya ukeni, pamoja na dalili nyingine kama uchafu usio wa kawaida, maumivu wakati wa kukojoa, na maumivu wakati wa kujamiana.
4. Usafi duni wa uke
Kutosafisha sehemu za siri kwa usahihi au kutumia sabuni zenye kemikali kali kunaweza kuathiri usawa wa bakteria wa kawaida na kusababisha harufu mbaya.
5. Kutumia vyombo vya kuzuia mimba au dawa fulani
Baadhi ya vidonge vya kuzuia mimba, mionzi au dawa fulani zinaweza kubadilisha usawa wa bakteria na fangasi, na hivyo kusababisha harufu mbaya.
6. Mabadiliko ya homoni
Mabadiliko ya homoni hasa wakati wa hedhi, ujauzito, au baada ya kuacha kutumia vidonge vya kuzuia mimba yanaweza kuathiri harufu ya uke.
7. Ugonjwa wa kisukari
Sukari nyingi mwilini huongeza hatari ya maambukizi ya fangasi, na hivyo kusababisha harufu mbaya ukeni.
8. Kutosafisha vyema baada ya kukojoa au kutoka chooni
Hali hii huweza kusababisha bakteria kuingia kwenye uke na kusababisha harufu mbaya.
Dalili Zinazohusiana na Harufu Mbaya Ukeni
Ute wenye rangi na harufu isiyofurahisha
Itching au kuwasha kwenye sehemu za siri
Maumivu wakati wa kukojoa au kujamiana
Kuvimba au kuwasha kwa uke
Mionekano tofauti ya ute kama mweupe, kijivu, au machungwa
Jinsi ya Kuzuia na Kutibu Harufu Mbaya Ukeni
Kuwa na usafi wa mara kwa mara: Safisha sehemu za siri kwa maji safi na sabuni isiyo na harufu kali.
Epuka kutumia sabuni zenye kemikali kali au bidhaa zisizo rafiki kwa uke.
Tumia nguo za ndani zinazopumua na zisizokuwa tight sana.
Kula vyakula vinavyoongeza kinga mwilini kama matunda na mboga.
Epuka kuoga kwa maji moto sana au kwa mda mrefu.
Pima afya yako mara kwa mara kwa daktari wa wanawake, hasa ikiwa dalili zinaendelea.
Tibu maambukizi mapema ili kuepuka matatizo makubwa.