Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye shule za Advance Nchini Ambazo kila mwaka Hupokea wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano ambao hupangiwa shule na TAMISEMI Kupitia makala hii utafahamu jinsi ya kuangalia Majina ya waliochaguliwa Form Five Katavi.
Jinsi ya Kuangalia Selection za Form Five – Mkoani Katavi
Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2024 na kufaulu vizuri hupewa nafasi ya kujiunga na kidato cha tano kupitia mfumo wa TAMISEMI. Kupitia mfumo huu, majina ya waliopangiwa shule hutolewa kwa uwazi na upatikanaji wake ni rahisi kwa kila mwanafunzi.
Hatua za Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa:
Fungua tovuti rasmi ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tzBonyeza kiungo chenye maandishi: “Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano 2025”
Chagua Mkoa – Katavi
Chagua Halmashauri unayotaka, mfano: Mpanda TC, Mlele DC n.k.
Tafuta jina lako au angalia orodha ya wanafunzi waliopangiwa shule fulani
Unaweza pia kutafuta kwa kutumia jina la mwanafunzi au namba ya mtihani.
Halmashauri za Mkoa wa Katavi
Mkoa wa Katavi una halmashauri kadhaa ambazo ndizo zinazopokea na kusimamia shule za sekondari zinazopokea wanafunzi wa kidato cha tano. Halmashauri hizo ni:
Mpanda Town Council (Mpanda TC)
Mpanda District Council (Mpanda DC)
Mlele District Council
Tanganyika District Council
Nsimbo District Council
Katika halmashauri hizi, kuna shule mbalimbali ambazo zinatoa elimu ya sekondari ya juu (Form 5 & 6), zikiwemo:
Mpanda Secondary School
Milala Secondary School
Usevya Secondary School
Inyonga Secondary
Karema Secondary School
Shule hizi zimekuwa zikipokea wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali kutokana na matokeo mazuri ya kielimu na mazingira bora ya kusomea.
Jinsi ya Kupata Form Five Joining Instructions – Shule za Mkoani Katavi
Baada ya mwanafunzi kujua shule aliyopangiwa, hatua muhimu inayofuata ni kupata fomu ya maelekezo ya kujiunga (Joining Instructions) kutoka kwa TAMISEMI au tovuti ya shule husika. Fomu hii ina taarifa muhimu kama:
Muda wa kuripoti shule
Vitu vinavyotakiwa kubeba
Ada na michango
Mavazi rasmi ya shule
Sheria na kanuni za shule
Hatua za Kupata Joining Instructions:
Tembelea:
https://selform.tamisemi.go.tz/Content/selection-and-joining-instructionsChagua Mkoa – Katavi
Tafuta jina la shule ambayo mwanafunzi amepangiwa
Bonyeza link ya “Download” ili kupakua fomu
Chapisha (print) au hifadhi kwenye simu kwa matumizi ya baadaye
Ni muhimu mzazi au mlezi asome kwa makini fomu hii kwani inahusisha kila jambo muhimu kabla ya mwanafunzi kuripoti.