Hatua kwa Hatua fahamu Jinsi unvyoeza kuangalia Shule za form five Mkoani Ruvuma na Halmashauri za wilaya zake walizopangiwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2024.
Jinsi ya Kuangalia Selection za Form Five Mkoani Ruvuma
TAMISEMI ndio chombo rasmi kinachosimamia upangaji wa wanafunzi wa kidato cha tano. Kupitia tovuti yao, unaweza kuona shule uliyochaguliwa kwa kutumia jina lako au namba ya mtihani.
Hatua kwa Hatua:
Tembelea tovuti ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tzBonyeza sehemu iliyoandikwa “Selection Kidato cha Tano 2025”
Chagua Mkoa – Ruvuma
Teua Halmashauri unayotaka kuangalia
Tafuta jina la mwanafunzi kwa kutumia:
Namba ya Mtihani
Jina Kamili la Mwanafunzi
Mfumo huu utakuonesha shule aliyopangiwa mwanafunzi, tahasusi (combination), na mahali ilipo shule hiyo.
Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma una halmashauri mbalimbali zinazoratibu utoaji wa elimu ya sekondari. Halmashauri hizi ndizo husimamia shughuli zote za shule za sekondari, ikiwemo kupanga wanafunzi na utoaji wa taarifa muhimu kwa wazazi.
Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma:
Songea Municipal Council
Songea District Council
Mbinga Town Council
Mbinga District Council
Nyasa District Council
Tunduru District Council
Namtumbo District Council
Shule za Advance (Kidato cha Tano) Mkoani Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma una shule kadhaa za sekondari zinazotoa masomo ya tahasusi kwa kidato cha tano na sita (A-Level). Baadhi ya shule hizi ni za serikali na zingine binafsi, na zinahudumia wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.
Baadhi ya Shule Maarufu za Advance Mkoani Ruvuma:
Songea Boys High School
Songea Girls Secondary School
Mbinga Secondary School
Tunduru Secondary School
Likuyuseka Secondary School
Lituhi Secondary School
Mtipwili Secondary School
Lusewa Secondary School
Kila shule ina mchanganyiko tofauti wa tahasusi kulingana na uwezo wake na idadi ya wanafunzi inayoweza kuhudumia.
Jinsi ya Kupata Form Five Joining Instruction – Shule za Mkoa wa Ruvuma
Fomu ya kujiunga (Joining Instructions) ni muhimu sana kwa mwanafunzi anayepangiwa shule mpya. Fomu hii ina maelezo ya:
Tarehe ya kuripoti
Mahitaji ya shule (sare, vifaa vya masomo n.k.)
Ada na michango
Taratibu za usajili na maelekezo mengine muhimu
Hatua za Kupakua Joining Instruction:
Tembelea tovuti ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tz/Content/selection-and-joining-instructionsChagua Mkoa – Ruvuma
Chagua Shule aliyopangiwa mwanafunzi
Bonyeza Download kupakua nyaraka hiyo
Ni muhimu kusoma kwa makini maelekezo yaliyomo kwenye fomu kabla ya mwanafunzi kujiunga shuleni.