Mbeya ni jiji lenye Shule za nyingi na maarufu za Advance nchini Tanzania ambazo kila mwaka Hupokea Wanafunzi wapya wanaopangiwa shule za form 5 na Tamisemi Hapa tunakuletea Hatua za kufuata kujua jinsi ya kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mkoani Mbeya.
Jinsi ya Kuangalia Selection za Form Five – Mkoani Mbeya
Orodha ya wanafunzi waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano hutolewa rasmi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia tovuti yao. Mfumo huu ni wa kidigitali na rahisi kutumia kwa mzazi au mwanafunzi binafsi.
Hatua za Kuangalia Majina ya Waliopangiwa:
Tembelea tovuti ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tzBonyeza kiungo chenye maandishi: “Selection Kidato cha Tano 2025”
Chagua Mkoa – Mbeya
Kisha chagua Halmashauri unayotaka kama vile Mbeya City Council, Rungwe DC n.k.
Tafuta jina lako kwa kutumia:
Namba ya mtihani
Jina la mwanafunzi
Au shule aliyotoka
Mfumo huu pia hukuruhusu kuona shule aliyopangiwa mwanafunzi na fomu ya maelezo ya kujiunga.
Halmashauri za Mkoa wa Mbeya
Mkoa wa Mbeya una jumla ya halmashauri 9 ambazo zinasimamia shule mbalimbali za sekondari ya juu. Halmashauri hizi ndizo zinazopokea wanafunzi waliopangiwa shule katika maeneo yao.
Orodha ya Halmashauri za Mbeya:
Mbeya City Council
Mbeya District Council
Rungwe District Council
Kyela District Council
Chunya District Council
Mbarali District Council
Busokelo District Council
Tukuyu Town Council
Tunduma Town Council
Katika halmashauri hizi, kuna shule nyingi maarufu za kidato cha tano kama:
Iyunga Secondary School
Rungwe Secondary
Loleza Secondary
Mbeya Secondary School
Tukuyu High School
Mbalizi Secondary
Chunya Girls / Chunya Boys
Jinsi ya Kupata Form Five Joining Instructions – Shule za Mbeya
Baada ya mwanafunzi kujua shule aliyopangiwa, hatua muhimu inayofuata ni kupakua na kusoma Fomu ya Maelekezo ya Kujiunga (Joining Instructions). Fomu hii inaeleza kwa kina:
Tarehe ya kuripoti shule
Mahitaji muhimu kama sare, daftari, vifaa vya malazi
Ada na michango mingine ya shule
Taratibu za usajili
Sheria na kanuni za shule
Hatua za Kupata Fomu ya Joining Instructions:
Nenda kwenye tovuti ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tz/Content/selection-and-joining-instructionsChagua Mkoa – Mbeya
Tafuta jina la shule mwanafunzi aliyopangiwa
Bonyeza Download kupakua fomu ya shule husika
Chapisha (print) au ihifadhi kwa matumizi ya baadaye
Ni vyema mzazi au mlezi kusoma fomu hiyo mapema ili kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa wakati.