Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » Fahamu Gharama za kusajili kampuni BRELA
Biashara

Fahamu Gharama za kusajili kampuni BRELA

BurhoneyBy BurhoneyMarch 18, 2025No Comments3 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
Fahamu Gharama za kusajili kampuni BRELA
Fahamu Gharama za kusajili kampuni BRELA
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)Wametanabaisha Gharama za usajili wa Kampuni Brela Gharama ambazo huweza kutofautiana kulingana na Ukubwa wa kampni.

Gharama za Usajili wa Kampuni

Ada ya Usajili:

    • Ada za usajili wa kampuni zinaanzia Tsh 20,000 hadi Tsh 50,000,000 kulingana na mtaji wa kampuni husika. Kampuni ndogo yenye mtaji mdogo inaweza kulipa ada ya chini zaidi, wakati kampuni kubwa yenye mtaji mkubwa italipa ada zaidi.

Ada za Kampuni za Kigeni:

    • Kwa kampuni za kigeni, ada ya usajili ni USD 1,190. Pia, kuna ada ya kufungua nyaraka (filing fee) ya Tsh 66,000 na ada ya stamp duty ya Tsh 6,200.

Ada za Huduma Nyingine:

    • Ada ya maombi ya kusajili notisi ya kusitisha biashara ni Tsh 10,000.
    • Ada ya maombi ya kusajili mabadiliko ya taarifa yoyote iliyosajiliwa ni Tsh 15,000.
    • Ada ya kukagua rejesta ni Tsh 2,000.
    • Nakala isiyo na ithibati ya waraka wowote chini ya uangalizi wa Ofisi ya Msajili, kwa ukurasa au sehemu ya ukurasa ni Tsh 3,000.

Gharama hizi zinajumuisha ada za msingi za usajili na zinaweza kuongezeka kulingana na huduma za ziada kama vile ushauri wa kisheria au huduma za wakala.

Soma Hii :Orodha ya Biashara Zinazoweza kukuingizia Faida ya elfu kumi kwa siku

Ada za Kampuni

1. Kampuni ambayo thamani ya hisa zake halisi ni:
– Zaidi ya Tsh.. 20,000/= lakini si zaidi ya Tsh.. 1,000,000/= Tsh. 95,000 /=
– Zaidi ya Tsh.. 1,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh.. 5,000,000/= Tsh. 175,000 /=
– Zaidi ya Tsh..5,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh..20,000,000/= Tsh. 260,000 /=
– Zaidi ya Tsh.. 20,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh.. 50,000,000/= Tsh. 290,000 /=
– Zaidi ya Tsh..50,000,000/= Tsh. 440,000 /=
2. Usajili wa kampuni ambayo haina mtaji wa hisa ambapo idadi ya washirika ni kama ilivyoelezwa katika Malengo na Katiba ya Kampuni: Tsh. 300,000 /=
3. Ada ya kufungua jalada kwa ajili ya maombi, maana yake Tsh.. 22,000/= kwa kila waraka, yaani Malengo na Katiba ya Kampuni. Tsh. 66,000 /=
4. Gharama ya kila Ushuru wa stempu katika kila nakala ya Malengo na Katiba ya Kampuni ni Tsh. 10,000 /=
5. Gharama za ushuru wa stempu katika Fomu na. 14b Tsh. 1,200 /=
6. Kulinda jina la kampuni ni Tsh. 50,000 /=
7. Kubadilisha jina la kampuni Tsh. 22,000 /=
8. Gharma za upokeaji na/au usajili wa waraka wowote kwa Msajili chini ya Sheria ni Tsh. 22,000 /=
9. Gharama za kuchelewa kufungua faili/usajili wa waraka wowote zinalipwa kwa Msajili (kwa mwezi au sehemu ya siku za mwezi) TSHS 2,500 /=
10. Gharama za kujaza taarifa ya mwaka Tsh. 22,000 /=
11. Gharama za ithibati ya waraka wowote kwa ukurasa ni Tsh. 3,000 /=
12. Gharama za kutafuta jalada lolote/au kupekua kitu chochote ni Tsh. 3,000 /=
13. Gharama kwa ajili ya ripoti ya utafutaji kwa faili ni Tsh. 22,000 /=
14. Ada zinazolipwa na kampuni ambapo Kifungu XII cha Sheria kinahusika
– Gharama za usajili wa nakala yenye ithibati ya mkataba, sheria au malengo na katiba ya kampuni, au muongozo mwingine au kufafanua katiba ya kampuni ni Dola za Kimarekani 750 /=
– Gharama za ujazaji wa waraka wowote unaohitajika kupelekwa kwa Msajili chini ya Kifungu XII cha Sheria hii/mbali na mizania ni Dola za Kimarekani 220 /=
– Gharama kwa ajili ya kufungua jalada la mizania Dola za Kimarekani 220 /=
– Ada ya kuchelewa kufungua jalada/usajili wa waraka wowote inalipwa kwa Msajili (kwa mwezi au sehemu ya siku za mwezi) ni Dola za Kimarekani 25 /=
15. Gharama ya kupata nakala ya Cheti cha Usajili  Tsh. 4,000 /=

.

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Related Posts

Bei Ya Mafuta Ya Parachichi

April 15, 2025

Wauzaji wa ng’ombe wa maziwa Tanzania

April 15, 2025

Bei Ya Ng’ombe Wa Maziwa

April 15, 2025

Gharama za kusafirisha mizigo kwa treni

April 15, 2025

Gharama za kusafirisha mzigo au Bidhaa kutoka Zanzibar

April 15, 2025

Bei ya Simu za Oppo na Sifa zake (Specifications)

April 15, 2025
Leave A Reply Cancel Reply

Latest Posts

Nafasi 137 za Kazi Kutoka UTUMISHI – Taasisi Mbalimbali Juni 2025

June 13, 2025

Nafasi 83 za Kazi Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) June 2025

June 12, 2025

Nafasi za Kazi – NARCO (Kampuni ya Ranchi za Taifa) – Juni 2025

June 12, 2025

Majina ya Walioitwa kazini Ajira Portal Utumishi PSRS 2025 PDF Download

June 12, 2025

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI na Ajira Portal 2025

June 12, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.