Decca College of Health and Allied Sciences (DECOHAS) ni miongoni mwa vyuo vinavyoongoza Tanzania katika kutoa mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi. Chuo kimekuwa chaguo la wanafunzi wengi kutokana na ubora wa elimu, miundombinu bora, na fursa pana za programu za afya na maendeleo ya jamii.
Kuhusu Chuo – Mkoa na Wilaya Kilipo
DECOHAS ipo katika jiji la Dodoma, ikiwa na kampasi kuu mbili:
CCT Campus (City Centre) – Iko karibu na Dodoma Regional Referral Hospital
Nala Campus – Iko takribani km 16 kutoka katikati ya jiji
Jiji la Dodoma ni salama, lipo katikati ya Tanzania, na lina mazingira mazuri kwa wanafunzi wa afya.
Kozi Zinazotolewa na DECOHAS
DECOHAS hutoa kozi za ngazi mbalimbali kuanzia Cheti (NTA 4), Diploma (NTA 5–6) na programu za mafunzo ya muda mfupi. Baadhi ya kozi zinapatikana ni:
Clinical Medicine
Nursing and Midwifery
Medical Laboratory Sciences
Pharmaceutical Sciences
Health Records and Information Technology (HRIT)
Food Technology and Human Nutrition
Veterinary Laboratory Technology
Animal Health and Production
Agriculture Production
Science and Laboratory Technology
Laboratory Assistant
Social Work
Community Development
Sifa za Kujiunga na DECOHAS
Sifa hutegemea kozi, lakini kwa ujumla:
Cheti cha Kidato cha Nne (O-Level) chenye ufaulu wa masomo ya Sayansi
Kwa Diploma, ufaulu wa kiwango kinachokubalika na NACTVET/TCU
Kuambatanisha nakala za vyeti, picha, na kitambulisho halali
Kukubaliana na taratibu za joining instructions baada ya kupokelewa
Kiwango cha Ada (Fee Structure)
Ada hutofautiana kulingana na kozi na aina ya mwanafunzi (Day scholar / Hostel & Meals). Kwa kawaida:
Kozi za Afya: kuanzia Tsh 945,000 – 1,145,000 kwa muhula kulingana na huduma
Kozi zingine kama Social Work zina gharama ya chini zaidi
Malipo yanaweza kufanywa kwa installments kama chuo kitakavyoelekeza
Inashauriwa kuangalia “Fee Structure” ya mwaka husika kwenye tovuti ya chuo.
Fomu za Kujiunga na Chuo
Fomu zinapatikana kupitia:
✔️ Kupakua PDF ya Application Form
✔️ Kujaza Online Application kupitia tovuti ya chuo
✔️ Kutuma kwa email, posta, au kupeleka moja kwa moja chuoni
Jinsi ya Ku-Apply (Hatua kwa Hatua)
Tembelea tovuti ya chuo: www.decohas.ac.tz
Fungua sehemu ya Application / Apply Online
Jaza taarifa zako sahihi
Ambatanisha vyeti na picha
Tuma maombi
Subiri ujumbe wa kukubaliwa (Admission Letter + Joining Instructions)
Students Portal – Jinsi ya Kuingia
DECOHAS Students Portal hutumika kwa:
Kuangalia matokeo
Malipo ya ada
Kuhifadhi taarifa binafsi
Kupata joining instructions
Kupitia tovuti ya chuo, chagua Student Portal, ingiza:
Username (kwa kawaida ni namba ya mtahiniwa)
Password
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa DECOHAS
Tembelea tovuti: www.decohas.ac.tz
Nenda kwenye Selection Status
Weka namba ya mtihani (NEC format)
Bofya Check
Utaona kama umechaguliwa, kozi, na tarehe ya kuripoti.
Mawasiliano ya Chuo (Contact Details)
Simu: +255 763 102 102 / +255 674 102 102
Simu ya ziada: +255 717 514 324
Email: decohas@gmail.com
Website: www.decohas.ac.tz
Anwani: P.O. Box 372, CCT, Dodoma

