VVU (Virusi Vya Ukimwi) vinapopenya mwilini, huanza kushambulia mfumo wa kinga. Kwa wanawake, baadhi ya dalili hujitokeza mapema kupitia mabadiliko ya kiafya kwenye sehemu za siri, hasa ukeni.
Ingawa dalili hizi zinaweza kufanana na za magonjwa mengine ya kawaida ya uke, ni muhimu kuzijua mapema ili kuchukua hatua stahiki kama kupima VVU na kuanza matibabu mapema.
Dalili za UKIMWI Zinazoonekana Ukeni
1. Kuwashwa Sana Ukeni
Kuwashwa mara kwa mara hasa bila sababu ya wazi (hakuna fangasi au mzio).
Huambatana na hisia ya kuchoma au kukereketa sehemu za ndani za uke.
2. Utokaji Usio wa Kawaida wa Majimaji (Vaginal Discharge)
Majimaji kuwa na rangi ya kijani, njano au nyeupe yenye harufu mbaya.
Kuongezeka kwa ute unaotoka ukeni hata bila kuwa kwenye kipindi cha ovulation.
Hali hii huashiria maambukizi ya bakteria au fangasi ambayo huathiri sana wanawake wenye kinga iliyo chini.
3. Kuvuja Damu Nje ya Hedhi
Mwanamke anaweza kupata matone ya damu bila kuwa kwenye kipindi cha hedhi.
Hii inaweza kuwa dalili ya maambukizi ya ndani ya uke au mlango wa kizazi.
4. Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa
Uke kuwa na maumivu makali au kuchoma wakati wa kujamiiana.
Mara nyingine huchangiwa na uwepo wa vidonda vidogo ambavyo havionekani kwa macho.
5. Vidonda au Majeraha Ukeni
Vidonda vidogo vinavyouma au kutokwa na usaha.
Huashiria uwepo wa maambukizi sugu ambayo mwili hauna uwezo wa kuyapambana kutokana na kinga kushuka.
6. Maambukizi ya Mara kwa Mara (UTI & Fangasi)
Kurudia rudia kwa UTI au fangasi ukeni ni dalili inayohusiana na kushuka kwa kinga.
Maambukizi haya huwa magumu kutibika kabisa bila kurejea.
Kwa Nini Dalili Hizi Hutokea?
VVU hupunguza kinga ya mwili, hivyo uke – ambao ni sehemu nyeti – huwa rahisi kushambuliwa na vimelea.
Maambukizi ya bakteria, fangasi, virusi kama HPV na Herpes hutokea kwa urahisi na kusababisha matatizo mbalimbali ya uke.
Soma Hii :Dalili za ukimwi kwenye miguu
Ni Lini Unapaswa Kupima VVU?
Ni vyema kupima VVU endapo unakumbana na:
Kuwashwa mfululizo ukeni bila sababu maalum
Majimaji yasiyo ya kawaida kutoka ukeni
Vidonda visivyoisha ukeni au sehemu za karibu
Maumivu ya mara kwa mara wakati wa tendo la ndoa
UTI na fangasi zinazojirudia hata baada ya matibabu
Je, Matibabu Yanasaidia?
Ndiyo. Ukigunduliwa na VVU:
Dawa za kufubaza virusi (ARVs) husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
Matibabu ya haraka kwa maambukizi ya uke huleta nafuu na kurejesha afya ya uke.
Kwa wanawake wanaotumia ARVs ipasavyo, dalili hizi hupungua au kutoweka kabisa.