Beriberi ni ugonjwa unaotokana na upungufu wa vitamini B1 (Thiamine) mwilini. Thiamine ni virutubisho muhimu vinavyosaidia mwili kubadilisha chakula kuwa nishati na kusaidia kazi ya mishipa ya fahamu. Ugonjwa huu unaweza kuathiri moyo, mfumo wa neva, na misuli, na huathiri watu wa rika zote endapo hawapati kiasi cha kutosha cha vitamini B1 katika lishe yao.
Aina za Ugonjwa wa Beriberi
Kuna aina kuu mbili za beriberi:
Beriberi Kavu (Dry Beriberi) – Hii huathiri mfumo wa neva (nerves).
Beriberi Mvua (Wet Beriberi) – Hii huathiri moyo na mzunguko wa damu.
Dalili za Ugonjwa wa Beriberi
1. Dalili za Dry Beriberi:
Kudhoofika kwa misuli (hasa kwenye miguu)
Ganzi au kuwashwa kwenye mikono na miguu
Kukakamaa kwa misuli
Kupoteza uwezo wa kutembea au kushika vitu
Kizunguzungu
Kushindwa kudhibiti mkojo au haja ndogo
Kupotea kwa kumbukumbu
2. Dalili za Wet Beriberi:
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Kuvimba miguu, uso au tumbo (edema)
Kupumua kwa shida
Maumivu ya kifua
Moyo kudhoofika (heart failure)
Kuchoka haraka sana hata bila kufanya kazi ngumu
Sababu za Ugonjwa wa Beriberi
Ugonjwa huu hutokana na ukosefu wa vitamini B1 kwa muda mrefu, unaotokana na mambo yafuatayo:
Lishe duni – kutokula vyakula vyenye vitamini B1 kama mboga za majani, nafaka nzima, maharagwe, nyama, nk.
Unywaji wa pombe kupita kiasi – huathiri uwezo wa mwili kufyonza vitamini B1.
Matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji – kama magonjwa ya ini au utumbo.
Upasuaji wa kupunguza uzito (gastric bypass) – huathiri ufyonzaji wa vitamini.
Ujauzito – mahitaji ya vitamini B1 huongezeka.
Kula chakula kilichokobolewa sana – mfano mchele mweupe uliosafishwa mno.
Magonjwa ya kudumu kama kisukari na UKIMWI – yanaweza kusababisha upungufu wa vitamini B1.
Tiba ya Ugonjwa wa Beriberi
1. Matibabu ya Hospitali:
Kuanza kutumia vitamini B1 (Thiamine) mara moja kwa sindano au vidonge.
Daktari anaweza kuanzisha matibabu ya mdomo au ya sindano, kulingana na ukali wa ugonjwa.
Wagonjwa wenye hali mbaya huweza kulazwa kwa uangalizi wa karibu.
2. Marekebisho ya Lishe:
Kula vyakula vyenye wingi wa vitamini B1:
Mbegu za alizeti
Maharagwe
Samaki (hasa tuna na salmon)
Mayai
Mbogamboga za kijani kibichi
Ngano isiyokobolewa
Uji wa ulezi na mtama
Karanga na korosho
3. Matibabu ya Dalili:
Dawa za kusaidia moyo ikiwa umeathirika
Tiba ya mishipa na mazoezi ya kusaidia misuli iliyodhoofika
Kuweka lishe ya kudumu yenye virutubisho kamili
Hatari ya Kutotibu Beriberi kwa Wakati
Usipotibiwa, beriberi inaweza kusababisha:
Kushindwa kwa moyo
Ugonjwa wa Wernicke-Korsakoff (ugonjwa wa neva unaoathiri ubongo)
Kupooza au ulemavu wa kudumu
Kifo endapo hali itazidi bila matibabu
Njia za Kuzuia Ugonjwa wa Beriberi
Kula lishe kamili yenye vitamini B1 kila siku.
Epuka kunywa pombe kupita kiasi.
Wajawazito na wanaonyonyesha wachukue virutubisho vya B1 kama daktari atashauri.
Wagonjwa wa kisukari au wanaotumia dawa kwa muda mrefu wafanye vipimo vya vitamini.
Epuka mchele uliokobolewa sana – tumia mchele wa brown au wa kawaida.