Uchungu wa uzazi ni hatua ya kwanza ya kujifungua. Wakati wa uchungu wa uzazi misuli ya tumbo lako la uzazi (uterasi) inabana tena na tena ili kumsukuma mtoto wako nje. Mikazo hii huitwa uchungu wa kuzaa. Mikazo huacha na kuanza yenyewe. Huna udhibiti wowote juu yenyewe.
Zifuatazo ni Dalili za Mwanzoni za Kujifungua au Dalili za Mwanzoni za Uchungu.
1. Maumivu ya Mgongo na Kiuno Wakati fulani.
Wajawazito wengi hupata Maumivu haya kutokana na Ongezeko la Homoni ya Relaxin ambayo hulegeza Nyonga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Mtoto anaweza kupita kwenye Nyonga, wakati Mwingine hii Homoni huweza kuathiri Jointi na Ligamenti za Mwili mzima na Mjamzito hupata Maumivu Jointi nyingine za Mwili wake.
2. Mtoto Kushuka (Lightening).
Kuanzia Wiki ya 32 Mara nyingi Mtoto hushuka kwenda kwenye Nyonga tayari kwa ajili ya Kuzaliwa na Kutoka Duniani.
3. Kukojoa Mara kwa Mara.
Baada ya Mtoto Kushuka Mjamzito huanza kupata Dalili za Kukojoa Mara kwa Mara, Ni kwa sababu Kibofu Cha Mkojo hugandamizwa na sehemu ya Mtoto ambayo iko Chini kwenye Nyonga ya Mjamzito na kubanwa kwa Kibofu Kati ya sehemu hiyo ya Mtoto na Mfupa wa Kinena.
4. Kuchoka Mara kwa Mara na Kukosa Usingizi.
Maumivu katika kipindi cha Mwishoni mwa Ujauzito na Kukojoa Mara kwa Mara hii hupelekea Mjamzito kukosa Usingizi wa kutosha hivyo Muda mwingi huwa na Uchovu wa Mara kwa Mara.
5. Uzito kutoongezeka.
Kwa kawaida Mjamzito huongezeka Uzito wa Wastani wa 1kg katika kila Mwezi mmoja katika Kipindi cha Ujauzito lakini inapofika Mwishoni mwa Ujauzito Uzito huwa hauongezeki na wakati mwingine inawezekana kabisa Uzito hupungua ndio maana ni vema inapofikisha Wiki 42 ujifungue na hutakiwi kuzidisha Wiki 43 za Ujauzito.
6. Kuharisha.
Baadhi ya Wajawazito hupata Dalili ya Kuharisha hii ni Kutokana na Ongezeko la Homoni za Prostaglandins ambazo hupelekea Mfuko wa Uzazi kujikunja na kuweza kutoa Mtoto Wakati wa Kujifungua lakini pia huweza kupelekea Ongezeko kubwa la mjongeo wa Utumbo Mdogo hivyo huweza kupelekea Dalili za Kuharisha kwa Mjamzito.
Hutofautiana kati ya Mjamzito moja na mwingine.
7. Maumivu ya Kubana na Kuachia.
Maumivu ya kubana na kuachia hutokea katika kipindi chote Cha Ujauzito, Lakini endapo Maumivu hayo hayana Mpangilio maalumu basi huwa ni Dalili za Mwanzoni za Kujifungua tofauti na Uchungu Kamili ambapo Maumivu huongezeka kadiri Muda unavyoenda na huwa na Mpangilio maalumu.
8. Mtoto kupunguza kucheza.
Kwa kawaida Wajawazito huanza kuhisi Mtoto kucheza kuanzia Wiki ya 20 kwenda juu na Mtoto huongezeka kucheza kadiri umri wa Mimba unavyoongezeka na kufikia Wiki ya 32 Mtoto hucheza zaidi baada ya hapo Mtoto hupunguza Kucheza kwa sababu anakuwa ameshuka kwenye Nyonga tayari kwa ajili ya Kutoka na Kuzaliwa.
Soma hii :Faida Za Kufanya Mapenzi Wakati wa Ujauzito
Ni nini hufanyika wakati wa uchungu wa uzazi?
Mlango wako wa kizazi ni sehemu ya chini ya uterasi yako ambapo inaunganishwa na uke wako. Mlango wa kizazi una mwanya mdogo ambao hubaki ukiwa umefungwa kabisa unapokuwa mjamzito. Wakati wa uchungu wa uzazi, mikazo yako polepole huvuta mlango wa kizazi na kuufungua hadi upanuke vya kutosha kwa mtoto wako kutoka.
Uchungu wa uzazi una sehemu 2:
Uchungu wa uzazi wa mapema
Uchungu wa uzazi unaoendelea
Wakati wa uchungu wa uzazi wa mapema:
Shingi yako ya kizazi huanza kuwa nyembamba na kufunguka takriban inchi 1 hadi 2 (sentimita 2 hadi 5)
Mikazo huja na kuondoka na kupata nguvu na kugawanyika kwa usawa zaidi
Maumivu haya siyo mabaya sana
Wakati wa uchungu wa uzazi unaoendelea:
Mlango wako wa kizazi hufunguka kikamilifu, takriban inchi 4 (sentimita 10) na kubana kabisa.
Mtoto wako anashuka (husogea chini kwenye fupanyonga lako na kuwa tayari kuingia kwenye njia ya uzazi)
Unaanza kujisikia kama unahitaji kusukuma mtoto nje
Maumivu ni makali zaidi
kupasuka kwa chupa yako ya uzazi ni wakati mfuko wa amnioti hupasuka na kiowevu cha amnioti kutoka kwenye uke wako. Hii inaweza kutokea kabla ya kuanza kwa uchungu wa uzazi au wakati wa uchungu wa uzazi.