“Mdudu wa kidole” ni jina linalotumika na watu wengi kuelezea hali ya maambukizi au uvimbe unaotokea kwenye eneo la kucha au karibu na kucha, mara nyingi kwenye vidole vya mikono au miguu. Kitaalamu, hali hii hujulikana kama paronychia, na inaweza kusababishwa na bakteria au fangasi. Ugonjwa huu ni wa kawaida sana na mara nyingi hutokana na majeraha madogo kwenye ngozi ya kuzunguka kucha.
Dalili za Mdudu wa Kidole
Maumivu makali kwenye eneo la kucha
Uvimbe au kujaa usaha pembeni ya kucha
Ngozi kuwa nyekundu na ya moto
Kucha kujaa maji au usaha chini yake
Kucha kuachia au kubadilika rangi
Homa (kama maambukizi yameenea sana)
Kunaweza kuwepo na harufu mbaya kama kuna usaha mwingi
Sababu za Mdudu wa Kidole
Kukata kucha vibaya au kwa nguvu
Kung’ata kucha au ngozi pembeni ya kucha
Kuweka mikono kwenye maji mara kwa mara (husababisha fangasi)
Matumizi ya kemikali bila glovu
Kuchubuka au kuumia kwenye eneo la kucha
Maambukizi ya bakteria (kama staphylococcus aureus)
Maambukizi ya fangasi kama candidiasis
Kuvuta kucha za bandia au kutumia vifaa visafi saluni
Tiba ya Mdudu wa Kidole
1. Tiba ya Kawaida ya Nyumbani
Kutumbua usaha kidogo kwa sindano safi na kutumia maji ya uvuguvugu
Kuloweka kidole kwenye maji ya chumvi ya uvuguvugu mara 3–4 kwa siku ili kupunguza maumivu na kuvuta usaha
Kutumia asali kama dawa ya asili yenye antibacterial
Kupaka mafuta ya tea tree – yana uwezo wa kuua bakteria na fangasi
2. Dawa kutoka hospitali
Antibiotics za kumeza kama amoxicillin au cloxacillin kama kuna maambukizi ya bakteria
Dawa za kupaka zenye antibiotic kama mupirocin au fucidin
Antifungal creams kwa maambukizi ya fangasi
Drainage (kutoa usaha) na daktari kama usaha umejaa sana
Kuvuliwa kwa kucha ikiwa imeharibika sana
Jinsi ya Kuzuia Mdudu wa Kidole
Epuka kung’ata kucha au ngozi ya pembeni
Tumia glovu unapofanya kazi za maji au kemikali
Kata kucha kwa ustadi na usikate sana
Hakikisha vifaa vya kucha vinavyotumika salon ni safi
Kausha mikono vizuri kila baada ya kuiosha
Usishughulikie vidonda bila kutumia dawa au kuvaa plasta