Homa ya ini aina ya Hepatitis B ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Hepatitis B Virus (HBV). Ugonjwa huu huathiri ini kwa kiwango kikubwa na unaweza kuwa wa muda mfupi (acute) au wa muda mrefu (chronic). Hepatitis B ni moja kati ya magonjwa hatari sana duniani, hasa kutokana na ukweli kuwa mara nyingi huambukiza bila dalili za awali, lakini hushambulia ini taratibu hadi kusababisha madhara makubwa kama saratani ya ini au ini kushindwa kufanya kazi.
Dalili za Hepatitis B
Dalili za Hepatitis B zinaweza kuonekana kati ya wiki 1 hadi miezi 6 baada ya mtu kuambukizwa virusi. Zifuatazo ni dalili kuu:
1. Kichefuchefu na Kutapika
Mtu huhisi tumbo lina chemka, kukosa hamu ya kula na hata kutapika mara kwa mara.
2. Uchovu Mkali
Mgonjwa huhisi hana nguvu kabisa hata bila kufanya kazi nzito.
3. Maumivu upande wa juu wa tumbo (eneo la ini)
Ini lipo upande wa juu wa tumbo upande wa kulia, na maumivu hutokea kwenye eneo hilo.
4. Macho na ngozi kuwa ya njano (Jaundice)
Hii ni dalili maarufu inayohusishwa na kuathirika kwa ini.
5. Mkojo kuwa wa rangi ya giza
Mkojo huonekana kama mweusi au kahawia, tofauti na kawaida.
6. Kinyesi kuwa chepesi au kijivu
Mabadiliko haya ni ishara kuwa ini halifanyi kazi vizuri.
7. Homa ya mara kwa mara
Homa hupanda na kushuka, wakati mwingine bila sababu ya moja kwa moja.
8. Maumivu ya viungo na misuli
Husababishwa na mwili kujaribu kupambana na virusi.
9. Kichwa kuuma na mzunguko wa kichwa
Virusi vinapoathiri ini, vinaweza kuleta dalili kama za malaria au homa ya kawaida.
10. Kupungua kwa hamu ya kula
Mgonjwa hupoteza hamu ya kula chakula cha kawaida kabisa.
Dalili kwa Watoto
Watoto wengi walioambukizwa Hepatitis B hasa wakiwa wachanga hawana dalili yoyote. Lakini wanaweza kuendelea kuwa waenezaji wa virusi kwa miaka mingi bila kujua.
Dalili za Hepatitis B ya Muda Mrefu (Chronic)
Watu wenye Hepatitis B ya muda mrefu huweza kuishi bila dalili yoyote kwa miaka mingi. Hata hivyo, wanaweza kupata madhara makubwa baadaye kama vile:
Uvimbe wa ini
Ugonjwa sugu wa ini
Saratani ya ini
Kushindwa kwa ini kufanya kazi (liver failure)
Nini cha Kufanya Ukiona Dalili Hizi?
Muone daktari haraka kwa vipimo.
Fanya kipimo cha damu kuthibitisha kuwepo kwa virusi vya HBV.
Epuka kutumia dawa za kienyeji bila ushauri, kwani zinaweza kuharibu ini zaidi.