Wanaume wenye aibu mara nyingi hawawezi kusema moja kwa moja kuwa wanakupenda. Wanajificha nyuma ya tabasamu, macho yaliyokwezwa, au utani usio na maana. Lakini, ndani yao mioyo yao huwaka moto wa mapenzi – wanakuzimia vilivyo!
1. Anakuangalia Mara kwa Mara, Kisha Anageuza Macho Haraka
Mwanaume mwenye aibu hawezi kukutazama kwa muda mrefu kama wale wa “full confidence.” Atakuangalia kimya kimya, lakini mara ukigeuka kumuangalia, atageuza haraka macho kana kwamba hakuwa anakutazama.
2. Anakutafuta kwa Visingizio Visivyo na Maana
Atataka kuwa karibu nawe lakini atajificha kwenye visingizio. Mfano:
“Uliandika nini kwa assignment?”
“Uliniona jana shule?”
“Hivi uliona ile movie?”
Ni njia ya kukuanzishia mazungumzo bila kusema moja kwa moja kuwa anakupenda.
3. Huchanganyikiwa Unapomkaribia
Atakuwa na tabia ya kupoteza mpangilio wake wa kawaida – anaweza kucheka bila sababu, kusahau anachotaka kusema, au hata kushika vitu visivyohusika unapokaribia. Aibu hujaa mwilini mzima.
4. Anatabasamu Sana Ukiwa Karibu
Hata kama mko kimya, utaona tabasamu la ajabu usoni mwake. Siyo la kawaida, bali lile la mtu aliye na furaha ya kukaribia mtu anayemzimia.
5. Anaulizia Habari Zako Kupitia Marafiki
Hana ujasiri wa kukuuliza mwenyewe, lakini utasikia marafiki zake wakisema:
“Flani aliuliza kama ulienda kwenye ile event.”
“Alitaka kujua kama uko okay, maana hukuposti siku mbili.”
Ni njia yake ya kujua habari zako bila kukukaribia moja kwa moja.
6. Anakutafuta Mitandaoni – Lakini Kimya
Analike picha zako zote (hasa zile za zamani), anaangalia stories zako, anacomment kidogo kidogo kwa emoji au kitu kisicho cha moja kwa moja. Anataka ujue yupo, lakini hataki kujitoa kabisa.
7. Huwa Mpole Zaidi Ukiwa Karibu
Wakati akiwa na watu wengine anaweza kuwa muongeaji, mchangamfu na hata mcheshi. Lakini ukifika, ghafla anakuwa mtulivu au anaanza kujifanya yuko bize. Hii ni kwa sababu aibu inamtawala.
8. Anajitahidi Kukusaidia Bila Kukuomba Malipo
Ukihitaji msaada, yupo. Anakupa notes, anakutumia links za vitu unavyovipenda, anakufanyia mambo madogo madogo ya kusaidia. Yote hayo ni njia za kukukaribia bila kusema “nakupenda.”
9. Anaweza Kuwa Mwingi wa Wivu – Lakini Anajificha
Ukiwa karibu na mwanaume mwingine, ananyamaza au anabadilika ghafla. Unaweza kuhisi hali ya utofauti, hata kama hasemi. Hii ni ishara kuwa moyoni mwake anataka awe yeye tu anayekufaa.
10. Marafiki Zake Wanamtania Unapopita
Ukiona marafiki zake wanamcheka au kumtania kwa sauti ya chini ukiwa karibu, jua tayari wanajua anavyojisikia juu yako. Hii ni dalili kuwa wamegundua kuwa anakupenda sana ila hana ujasiri wa kusema.
Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQs)
Je, mwanaume mwenye aibu anaweza kumpenda msichana sana?
Ndiyo. Wanaume wenye aibu mara nyingi hupenda kwa dhati na kwa muda mrefu sana, hata zaidi ya wale wanaojieleza haraka.
Nitajuaje kama hanipendi bali ni aibu tu?
Tazama mwenendo wake kwa muda: kama anajitahidi kuwa karibu kwa visingizio, anakutazama mara kwa mara, au anatafuta habari zako, ni dalili za mapenzi yenye aibu.
Nawezaje kumsaidia aondoe aibu?
Mpe tabasamu, zungumza naye kwa utulivu, usimcheke wala kumkosoa hadharani. Aibu inapungua kwa heshima na uaminifu.
Ni sawa mwanamke kuanza kuchukua hatua kwa mwanaume mwenye aibu?
Ndiyo. Kama unampenda pia, unaweza kumweleza kwa njia ya upole kuwa hupingwi na hisia zake. Mwanaume mwenye aibu huthamini sana uelewa kama huo.
Je, wanaume wote wenye aibu huwa hawatongozagi?
Wengine hujitahidi kutongoza, lakini kwa njia ya heshima, kupitia ujumbe wa maandishi, au baada ya muda mrefu wa ukaribu.